Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Wakuu Habari
Baada ya ziara ya Samia ya kwenda Kenya na kuondoa mtanziko wa kibiashara na kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili na malori ya Tanzania kuruhusiwa kupeleka bidhaa zetu huko nilisoma maoni ya baadhi ya Watanzania ndipo nikajua Magufuli aliharibu hii nchi kiasi gani.
Kwanza kitendo hiki cha Samia badala ya kupongezwa na kila Mtanzania kuna watu wngi nawajua ni wasomi wenye akili kabisa walikuwa wakiponda eti hii ni ziara ya kujipendekeza na ameingia mtegoni, ukiwauliza sababu hawana, yaani wao wanaona kufanya biashara na nchi jirani ni hasara kwa sababu Magufuli alina haifai.
Pili kaui ya Samia ya kuwaasa TRA kukusanya kodi kwa njia ambayo ni sustainable, ambayo itawezesha Serikali kupata mapato na hapo hapo sekta binafsi kuendelea kukua na kutoa ajira na kukuzauchumi, hili likaonekana tena ni udhaifu
Tatu Serikali ilipoagiza vibanda vya machinga viondolewe katikati ya barabara, jambo ambalo ni la mantiki kabisa kwa kuwa huwezi kufanya biashara barabarani, watu amba0o hata sio machinga nao walipinga vikali wakisema watamkumbuka Magufuli.
Nne Samia alipomsimamisha Sabaya baada ya tuhuma nyingi ambapo pia na yeye alikiri kutumia mabavu badala ya sheria kwenye mahaojiano yake na Clouds Tv, Samia amemsimamisha watu wengi wanalalamika eti kamuondoa kiongozi imara alitakiwa ampandishe cheo.
Tano Samia alipotangaza ataunda tume huru ya wataalamu wetu wa ndani (kwa kigezo cha Magufuli kuwa wazungu wanataka kutuua na chanjo) ili kujua ukweli wa hili , watu hawa pia walipinga vikali wakidai tamko la Magufuli kuwa chanjo hifai ndio linatakiwa kufuatwa japo halikuwa na msingi wowote wa Kisayansi.
Na leo wataalamu hao walipotoa majibu hayo na ku prove nadharia za Magufuli kuwa ni za uongo, nao wanashambuliwa vikali na Rais Samia pia anashambuliwa, kwa sababu tu wanaenda kinyume na tamko la Magufuli kuwa chanjo hazifai.
Kwa kweli Samia anatakiwa awe aggressive kudeal na haya magenge ya apotoshaji la sivyo atapata tabu mno.