Hayati Magufuli alijenga vituo vya afya 44 kwa miaka mitatu, Rais Samia anajenga 220 kwa miezi mitatu

Magufuli aliweka tozo na kutumia tozo, tumia parameters sahihi kufananisha watu. Hivi Magufuli angetumia huu mfumo tozo mtozoe SGR na Bwawa ingekuwa mukidemukide. Hao wamechota hazina sasa namna bora ya kujiendesha ni utopolo wa kitozo tozo
Huwezi weka tozo huku unaharibu uchumi,mama kaweka tozo kwa sababu uchumi unaenda juu,Mazao yanatoka kuanzia mbaazi hadi pamba ,vyote hivyo vilianguka kipindi cha Magu.

Magu alichojua ni kuzozana na majirani tuu kama Kenya mwisho wa siku parachichi,mahindi nk vikadoda sokoni huku anajitutumua na propaganda za kijinga eti vita vya kiuchumi.

Sasa hivyo vita vya kiuchumi vinakupeleka chini zaidi vina faida gani?
 
Watengeneza video na tv ya wizara tuoneshwe kama ReliTv ya mwanantala, isiwe maneno
 
Hivi mnajenga maboma au mnakamilisha hadi vifaa tiba na kuweka watumishi?
 
bila ya tozo amejenga vingapi
Hawa watu wapuuzi sana, wakati wana introduces VAT wakasema inaendaa kujenga shule hospital, wakalet Road tall wakasema wanaenda kujenga shule hospital, wakaleta Road licence maneno yaleyale. Leo wameleta tozo za miamala wanaenda kujenga yaleyaΔΊe, wameshatuona watanzania hamnazo
 

Polenta CCM kwa Msiba
 
Huwa najiuliza hivi Kituo cha Afya ni nini?? Majengo? Majengo + vifaa tiba + madawa + watumishi??? Je vituo 220 kama viko tayari vitaanza kufanya kazi lini hasa?? Yaani vinapokamika huwa ni pamoja na vifaa vyote + allocation ya madawa yote + allocation ya watumishi wote??? Naomba kuelimishwa hapa...
 
Haviwezi kuanza kufanya Kazi mwaka huu labda hadi bajeti ijayo ndio watenge pesa ya Vifaa tiba,vitenganishi,madawa,ajira mpya nk ila kwa mwaka huu lazima wakamilishe majengo ya awali kuwezesha huduma kutolewa.
 
Kwahiyo unadhani mimi niko malawi kwamba sijui kuna vituo vya afya vipya vinavyotoa huduma?
 
Kuwa na madeni hakuhusiani na kupata faida au hasara kama unalipa kwa utaratibu uliopangwa. Hata m,ashirika mengi yanayopata faida, yana madeni mengi tu, lakini yanayalipa kama ilivyopangwa katika kila mwaka.
 
Hiii ndio JF ya MAXMELO HATARI SANA WATU KAMA KINYONGA PLATFORM YA WATU WENYE MATUMAINI NA KULIA LIA LEO SAMIA ANAUPIGA MWINGI KESHO SAMIA HAWAMUELEWI
 
Za kuambiwa changanya na za kwako
 
Tujiulize hivi vituo,zahanati na hospitali zilizopo je zina madawa,vifaa na wataalamu vinatosheleza au ndio kujenga mabanda mengi ili ionekane tuna kuku wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…