Hayati Magufuli alijenga vituo vya afya 44 kwa miaka mitatu, Rais Samia anajenga 220 kwa miezi mitatu

Haviwezi kuanza kufanya Kazi mwaka huu labda hadi bajeti ijayo ndio watenge pesa ya Vifaa tiba,vitenganishi,madawa,ajira mpya nk ila kwa mwaka huu lazima wakamilishe majengo ya awali kuwezesha huduma kutolewa.
Sasa hiyo ni planning ya wapi? Yaani ujenge vituo 220 halafu popo hawamie mpaka utakapo pata pesa nyingine? Kwa nini usijenge vituo 100 full furnished with vifaa tiba na wataalamu?? Hapo ndiyo unaanza ku smell matango pori...
 
Kiongozi ungetulia kidogo ukaweka taarifa kwa utulivu, umeharakisha sana na matokeo yake umechanganya changanya sana.
Umeandika Magu alijenga kwa miaka mitatu.
Samia anajenga kwa miezi mitatu.
Samia atajenga kwa miezi mitatu.
Lete ufafanuzi mzuri, amesha jenga na kukamilisha kwa hiyo miezi mitatu, ama atajenga na kukamilisha kwa hiyo miezi mitatu?
Nimeomba ufafanuzi kwa sababu hata wakati wa uhai wa Magu mlituaminisha mambo lukuki, lakini baada ya kifo chake mkatueleza mambo tofauti.
 

Hilo ni rahisi kama utakua simvivu wa kutafuta ukweli vituo vya afya sikitu cha kukaa mfukoni kwa mtu. Vituo vya afya havikai ktk mafaili kutoviona labda uwe kipofu hii tanzania ni yako anza safari ya kuzuunguka na kuhesabu utapata ukweli wala hutomuomba mtu ruhusa ya kuhesabu vituo vya afya ili ujiridhishe
 
Sasa hiyo ni planning ya wapi? Yaani ujenge vituo 220 halafu popo hawamie mpaka utakapo pata pesa nyingine? Kwa nini usijenge vituo 100 full furnished with vifaa tiba na wataalamu?? Hapo ndiyo unaanza ku smell matango pori...
Ndio plan ya Serikali kwani wewe uliona wapi vyote vinafanyika kwa pamoja?
 
Hivyo vituo 220 ambavyo hata misingi haijachimbwa viko wapi?,tuletee picha ya vituo 5 tu kati ya hivyo 220 unavyosema vimejengwa
Hahahahah Wadanganyika at their best 😅 wanashabikia vituo hewa! Hio billion 60 kama itafanya mambo ni billion 20 tu hio 40 tusubirie story za sandarusi kwa CAG
 
Hahahahah Wadanganyika at their best 😅 wanashabikia vituo hewa! Hio billion 60 kama itafanya mambo ni billion 20 tu hio 40 tusubirie story za sandarusi kwa CAG
Unaishi kwa mawazo finyu na hasi,orodha ya mahali vituo vitajengwa imewekwa sasa wewe shida yako ni nini?

Watu wa Dar mna shida sana
 
Rais Samia ni mpango halisi wa Mungu,Mungu wetu hakawii wala hawai ni huyuhuyu tumepewa tumlinde,
 
Bajeti ya serikali ni TZS trilioni 27 kutoka kwa walipa kodi na misaada/Mikopo.
Sina shida na Ujenzi wa vituo vya afya na madarasa kwa watoto wetu.
Ninapata shida Serikali inapoendelea kuwekeza kwenye biashara ya usafiri anga (kwa kununua ndege kwa fedha taslimu).
Ni vema serikali ikaacha kujihusisha na kufanya biashara , ndiyo maana Serikali ya awamu ya tatu, ilibinafusisha Mashitika zaidi ya 400 ambayo yalianzishwa na Baba wa Taifa.
Serikali iweke mazingira wezeshi ya wananchi wake kufanya biashara na kulipa kodi.
Serikali inapaswa kufahamu kuwa mradi huu ni white elephant na sioni Kama mabilioni yanayowekezwa yataleta faida kwa taifa kwa miaka ya karibuni.
Tunawekeza kisiasa,hizi ndege 11 sina uhakika kama zimeanza kuleta faida,kwa maana tunaambiwa mapato bila kuambiwa upande wa pili wa matumizi.
 
Ndio maana POLEPOLE anataka kumkwamisha maana anafuta yoote ya JIWE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…