Dan Zwangendaba
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 5,814
- 8,118
Mtu huyo ni Rais Samia!
Nashawishika kabisa kuamini kuwa huyu Samia alichaguliwa kutokana na jinsia yake tu [kama ilivyojuwa kwa Kamala Harris…the word salad queen…kule Marekani].
Kamala yeye alichaguliwa na Biden kuwa mgombea mwenza kwa sababu ni mwanamke mweusi [ingawa kiuhalisia ni chotara wa Kihindi na Kijamaica].
Kamala ni mweupe kabisa. Yaani hovyo to the nth degree. Anaongeaga mashudu tu [word salads].
Hana kabisa uwezo wa kuongoza. Yeye ni kucheka cheka tu na kuongea mambo yasiyoeleweka.
Ukimwangalia Biden, unaona kabisa jamaa anapaswa awe nyumbani. Kazi ya urais wa Marekani kwa sasa haiwezi.
He is a creepy old guy. Hebu angalia hapa
Hivi alikuwa anafanya nini hapo kwa hako katoto? Na hiyo ni wiki iliyopita alipokuwa Finland baada ya kutoka Lithuania kwenye mkutano wa NATO.
Biden muda wowote anaondoka. Iwe kwa kujiuzulu, kuamua kutogombea tena muhula wa pili, au hata kufa [ingawa kifo hakina mwenyewe].
Wazo la Kamala kuja kuwa Rais wa Marekani endapo Biden ataondoka, linatisha watu wengi sana.
Haya, tuje kwa huyu wa kwetu hapa.
Huyu naye alichaguliwa kwa sababu ya identity politics tu. Ni mwanamke na ni Mzanzibari.
Kwa ninayoyaona, ni mtu asiye na uwezo wa kiuongozi ngazi ya Rais wa nchi.
Hakuchaguliwa kutokana na sifa zake za kiuongozi.
Inavyoonekana Magufuli alikuwa anataka sifa ya kuwa na mgombea wa kwanza wa CCM kumchagua mwanamke kuwa mgombea mwenza wake.
Haiwezekani kabisa kuwa Samia alichaguliwa kutokana na sifa zake kiutendaji [kwa sababu hana].
Jahazi limeshamshinda hivi sasa. Kabaki kutoa vitisho na kutumia dola kukabiliana na wanaompinga.
Na ukiongeza na inferiority complex aliyonayo kutokana na jinsia yake, ndo kabisa anakuwa paranoid kwamba kila anayempinga, anafanya hivyo kwa kusukumwa na chuki dhidi yake kwa sababu yeye ni mwanamke!
Rais Magufuli hakuwa kiongozi mzuri. Nilishasema mara nyingi tu kuwa yeye alikuwa msimamizi/ mnyapara mzuri.
Yeye mpe kazi au mradi ausimamie, halafu umpe mamlaka ya kutosha kuweza kufanya maamuzi ndani ya ukomo fulani, utampenda maana hakuwa wa mchezo mchezo.
Sidhani kabisa kuwa Magufuli aliwaza kuhusu yeye kuishia njiani na kumwacha Samia ndo awe Rais.
Nadhani alidhani kuwa atamaliza vipindi vyote viwili na kustaafu kama walivyofanya waliomtangulia.
Lakini haikuwa hivyo. Tumeachiwa huyu Samia.
Makamu wa Rais, Dkt. Mpango, kwa mtazamo wangu, ni bora mara 100 kuliko Samia [I got bars too 😀].
Chuki ni ugonjwa mkubwa nchi hii.
Nimekuwepo tangu Nyerere lakini sijaona Rais mwenye ubunifu kwenye maendeleo kama Samia. Nchi kubwa tu duniani kwa Sasa Zina struggle uchumi wao ila huyu mama mambo yanakwenda.
Miradi ya maji huko vijijini haijawahi kutekelezwa tangu Tanzania iumbwe.
Ward za ICU zilikuwa kwenye hospital za Muhimbili, KCMC, Bugando, Mkapa, na ile ya Moyo. Miaka miwili ya huyu usiyompenda ward za ICU ziko katika hospital zote za rufaa tena zikiwa na vifaa full.
Hakuwahi kutokea Rais yeyote kubuni mradi wa kujenga shule za kisasa zaidi ya Samia ambaye kila Wilaya anajenga shule ya standard kuanzia form 1 -6.
Ni huyuhuyu Samia ndiye Rais wa Kwanza kuja na mpango bora kabisa wa kulima kisasa.
Ni huyuhuyu unayemuona wewe kilaza, ndiye Rais aliyemaliza chaguo la pili la watoto kujiunga form one.
Ni huyuhuyu Samia ndiye Rais wa Kwanza kupeleka vitabu kwa kila mwanafunzi, kila somo tena kwa wakati kiasi kila shule sasa zimeanza kuwa na chumba maalum cha maktaba.
Tunakujuza tu huku Lindi tayari ujenzi wa vyuo vikuu viwili umeanza. Chuo Kikuu cha DSM na Chuo Kikuu cha Teknolojia Lindi.
Mwezi wa 9, anaanza kujenga Bandari ya Bagamoyo.
Scheme ya umwagiliaji Mbarali ilianzishwa na wakoloni around 1910s, hakuna Rais aliyewaza kujenga scheme mbadala wa hiyo. Kwa ubunifu wa huyu unayemuona kilaza, kwa kujua eneo lile tayari limezidiwa na pia kuna uharibufu wa mazingira anaipunguzia mzigo hiyo scheme na kujenga scheme kubwa kabisa ya umwagiliaji Rufiji ili kutopoteza maji ya Mto Rufiji kuingia baharini. Nakushauri tu, wahi Rufiji wenzenu wanachukua maeneo huko. Uzalishaji ushaanza na soon tutakuwa na "mchele wa Rufiji".
Hakuna Rais aliyeanzisha program ya kujenga kilomita zaidi ya 2000 za lami kwa wakati mmoja. Nenda vijijini tukaangalie wakandarasi wanafanya nini.
Yote haya yanafanyika bila kusimamisha miradi ya mtangulizi wake.
In short, nenda vijijini uzungumze mabaya ya Samia kama watakuelewa.
Hili la Bandari hakuna kurudi nyuma. Tutaliondoa chaka lenu la kutolipa kodi. DPW is here for port improvement. Mtake msitake.