Hayati Magufuli alikuja kuharibu maisha ya vijana, Mimi ni mmoja wa wahanga

Hayati Magufuli alikuja kuharibu maisha ya vijana, Mimi ni mmoja wa wahanga

Acha siamba Mkuu, watu wote tumejionea ajira hazikuwa kipaumbele awamu iliyopita.

Kuhusu umaskini wa nchi hii hoja haina mashiko ukumbuke ilisemekana hii nchi ni "tajiri" alias "Dona Kantre" tatizo kubwa tuliwaza maendeleo ya vitu zaidi na kusahau maendeleo ya watu.

Binafsi I don't get it kwanini hizi project Nyerere dam na SGR ziliendeshwa pamoja kwanini tusingeanza na Nyerere dam ambapo ingechochea maendeleo ya viwanda huku ajira nazo zikiendelea then the next project ije kuwa SGR huku ajira na nyongeza za watumishi zikiendelea? Ku run maproject makubwa makubwa kama haya at once ni sawa na kukanyaga Brakes and Accelerator at once.
Ni hayo Mkuu
Kwani awamu hii ajira ni kipaumbele?
 
Kuna sababu ya kuwa na career advices walau kila shule yenye A Level students na universities.

Na umuhimu wa kufundisha entrepreneurship module universities kwenye kila degree sambamba na fursa za kozi usika katika kujiajiri.

Kuna mada unasoma kama wewe ni katibu mkuu wizara ya elimu na mwanasiasa unaona huu sio mtazamo sahihi kwa wahitimu.

Yaani mtu anamaliza chuo na kudhania ni jukumu la serikali kumuajiri au kulegeza qualification criteria’s ili abaingize sector nyingine.

Kama ndio wanafunzi wanamaliza chuo na mtazamo huo; hawa watoto awaandaliwi vizuri kupambana na maisha.

Inabidi kuwe na career advice za kuwaambia ukweli kabla ya kwenda kusoma degrees zao realistic chances za kuajiriwa kwenye job market baadae ili wanafunzi wachague masomo yanayoongeza fursa za kupata ajira; sio kusukumwa na goals ambazo ni ngumu baadae.

Huo mtazamo wa mleta mada unasikitisha sana kama vijana wanaenda shule na kutegemea wakimaliza serikali iwaajiri; ni Tanzania tu inawezekana watu ndio wanafikiria ivyo.

On a serious note wahusika inabidi wanadili hiyo social attitude; serikali aina guarantee ya kukuajiri ukishahitimu ipo ivyo duniani kote sio Tanzania tu. Hakikisha unachukua masomo ambayo chances za kupata ajira private ni kubwa au skills unazopata unaweza jiajiri.
 
Kuna sababu ya kuwa na career advices walau kila shule yenye A Level students na universities.

Na umuhimu wa kufundisha entrepreneurship module university kwenye kila degree sambamba na fursa za kozi usika.

Kuna mada unasoma kama wewe ni katibu mkuu wizara ya elimu na mwanasiasa unaona huu sio mtazamo sahihi kwa wahitimu.

Yaani mtu anamaliza chuo na kudhania ni jukumu la serikali kumuajiri au kulegeza qualification criteria’s ili abaingize sector nyingine.

Kama ndio watu wanamaliza chuo na mtazamo hawa watoto awaandaliwi vizuri kupambana na maisha.

Inabidi kuwe na career advice za kuwaambia ukweli kabla ya kwenda kusoma degrees zao realistic chances za kuajiriwa kwenye job market baadae ili wanafunzi wachague masomo yanayoongeza fursa za kupata ajira.

Huo mtazamo wa mleta mada unasikitisha sana kama vijana wanaenda shule na kutegemea wakimaliza serikali iwaajiri; ni Tanzania tu inawezekana watu ndio wanafikiria ivyo.

On a serious note wahusika inabidi wanadili hiyo social attitude; serikali aina guarantee ya kukuajiri ukishahitimu ipo ivyo duniani kote sio Tanzania tu. Hakikisha unachukua masomo ambayo chances za kupata ajira private ni kubwa au skills unazopata unaweza jiajiri.
Na hii Mentality ndo inawafanya ht wakiajiriwa wasione fursa nyingine waishie kulalamika mishahara midogo au mishahara haijapanda.
 
Na hii Mentality ndo inawafanya ht wakiajiriwa wasione fursa nyingine waishie kulalamika mishahara midogo au mishahara haijapanda.
Kwa kweli inasikitisha kama huo ndio mtazamo wa maisha; yaani mtu ana plan moja tu. Ikibuma hajui afanye nini.

Hawa jamaa inabidi waweke desk la career advice mashuleni vijana wawe na uelewa wa realistic goals za maisha yao ya baadae.
 
Kaniharibia kiasi fulani mpaka... nikachelewa kuajiriwa nikachelewa kuoa nikachelewa kufikia/kutimiza malengo yangu

Lakini hatahivyo, nimepata ajira kwenye utawala wake!
JE UNADHANI SAMIA ATAENDELEA KUAJILI KILA MWAKA GRADUATES KAMA ALIVYOFANYA SASA?
 
huku ajira na nyongeza za watumishi zikiendelea?
Tatizo liko hapo! Nchi hii ni masikini na hamtaki kuuishi huo ukweli! Msoga aliwadanganya na sasa mnaendeleza hiyo legacy yake.

Miaka 10 ya msoga mlipokuwa mnajichotea mapesa, hayo hayakuwa maisha ya mtu binafsi, walafi na washenzi walioi-paralyse nchi? Mlipiga hatua gani? Nchi ikiwa na mpaka waajiriwa hewa na mishahara yao!

Mwaka 2022, karne ya 21 ishaanza kuzeeka, unazungumzia kufanya project moja at a time? Kweli? Unafahamu kuwa Mtanzania mmoja mmoja ameficha pesa kiasi gani nje ya nchi? Ulisikia mtumishi mmoja wa nchi hii akiwa na zaidi ya 3trillion hapo SA tu? Zingetosha kufanya project ngapi?

Ulimsikia Ngoi akisema mwananchi mmoja muajiriwa wa serikali akiwa na zaidi ya apartment 200 UK huko? Alizipataje?

Unashangaa nchi kufanya project nyingi kwa wakati mmoja?

Ukilipwa mshahara wako halali na stahiki zote, ukaambiwa uishi kwa uwezo huo, unaanza kulia lia kuwa wamekata safari, vikao, OC, wamebana mianya, increment(tena hapa hoja inakuwa ni miaka na si output yako)n.k wakiachia mle kwa urefu wa kamba zenu, mnaibuka mkiwa mmelewa kwamba hayo ndo maisha!

Ukiwa mbinafsi na mlafi, maisha ya bongo movie ndio linakuwa chaguo la mtu! Maisha haya sio halisi, tuishi kwenye uhalisia ili kila mtu achukie umaskini kwanza.
 
Nasikitika sana!

Mimi ni kijana mmoja wapo kati ya vijana wengi walioharibiwa maisha yao!

Siku zote ukweli hujitenga na uongo, sisemi uongo utawala wote wa awamu ya tano nimehangaika sana.

Nilihitimu chuo 2015 kada ya afya!

Kutokana na uhaba wa ajira nilikaa sana kitaa nikifanya mishe mishe mpaka nikaamua kwenda kuomba kufundisha shule ya private kwakuwa nilikua ninaufaulu mzuri wa masomo ya physics na hesabu, japo mshahara ulikuwa kiduchu lakini niliendelea kukomaa.

Nimefanya kazi pale baadae ukatoka waraka kuwa shule zote zifundishwe na walimu proffesionally sisi hatutakiwi! Mkurugenzi wa shule alinishauri nikasomee ualimu nikirudi atanipa nafasi tena, sikuamua kufanya hivyo kwakuwa tayari nilikua nina fani ya Afya na ugumu wa ajira ndio ulionileta hapo! Baasi nikapewa barua ya kuachishwa kazi, tulikua wawili wote tuliachishwa kazi kwa kigezo hicho kilichotoka Serikalini!

Nilikaaa bila ramani na baada ya muda nilijikita kwenye mambo ya habari nilifungua blog baada ya kuvutiwa na blog ya jamaa yangu aliyekua anavuta hela kupitia blog yake!

Kweli nilijitahidi sana mpaka nilianza kupata matangazo nakumbuka tangazo la kwanza kabisa nilipewa kutangaza ibada za hija na kanisa flani hivi, na tangazo la pili nilipewa kutangaza cables na dawa za mitishamba kupitia blog yangu!

Kiasi flani nilikua napata pata pesa japo zilikuwa kidogo.

Sikuchukua muda sana Serikali ya awamu ya tano ikazuia kuchapisha maudhui bila leseni na leseni ilikuwa mpaka 3M. Hapo ndo ukawa mwisho wa blog yangu nikajielekeza pengine kutafuta kipato!

Kiufupi ni kuwa mitego yangu yote awamu ya tano iligoma! JPM ametuharibia maisha wengi.

Nashukuru kwa sasa naendelea vizuri na ajira za mama nimebahatika hivyo naanza maisha upya.

Asante SSH, wakumbuke vijana wengi wanaishi maisha ya shida sana.
Shuzi mmoja alisikika akisema
 
Kwaiyo unatakaje mkuu au kavipi jamaa afukuliwe aongezewe marefu na mapana ya kaburi na azikwe tena
 
Kaniharibia kiasi fulani mpaka... nikachelewa kuajiriwa nikachelewa kuoa nikachelewa kufikia/kutimiza malengo yangu

Lakini hatahivyo, nimepata ajira kwenye utawala wake!
u were so lucky, binafsi aliniharibia sana
 
Vijana wa late 90's and 2000s laini laini sana, lazma mtafte wa kumpa lawama...

Mnapaswa mjue serikali haiwezi ajiri graduates wote, now mama kaaajiri next yr hawezi kuajiri tena the same amount of people maana nafasi zipo covered...
bomu la ajira halikuanza na JPM ni vile tu mmepata wa kumshushia lawama, Mzee Edo aliliongea sana kwenye kampeni 2015, JPM angewaajiri Nyote wapi mkafanye kazi wapi?

JPM kajenga miundo mbinu ya afya now mama hapati shida pa kuwapeleka.

Mi mkongwe, nimemaiza Chuo enzi za Mkwere sugua sana soli na bahasha yangu ya khaki, mtaani wananicheka sana nimeliza chuo na nnazurura tuna mtaani(Mama Davi Mungu akulipe popote ulipo, sijaisahau kampeni yako), mwisho nikaona nikielemaa ntakuja kufa njaa na dharau zitazidi,potelea mbali nikaamua kuingia kwa Muhindi salary 300k per month na Jiwe langu la Udsm.

2017 Dogo kamaliza Mzumbe akaanza kuchagua kazi namuangalia tu, mwaka umekatatika nikawambia inatosha, twende kwa Muhindi wangu upate pa kuanzia kila mtu ajijue mpango wake. So far he is doing great.

Moral of the story, no one will put food on silver plate for you to just eat...stop complaining go out there and take what is yours...
Mkuu nakuunga mkono kwa 100%. Ingawa Magu alikuwa kiongozi dhalimu ila vijana nao ni wapuuzi mno. Wanafikiria kiwepesi sana na hawashauriki. Mimi nafanya biashara na vijana wengi huwa wananifuata kuomba ushauri ila nilichogundua wengi huwa wanaanzisha biashara ili kupata tu sifa kwa marafiki zao na miezi michache baadae biashara hufa. Pia wale wanaoomba ajira huwa wanazikosa sana kwa kutanguliza swali "Mshahara Tsh ngapi?"....
 
Wewe ni Diaspora?
Hapana, ingekuwa ni kipaumbele kweli.
Nilitarajia kuona kama enzi za Kikwete.

Sasa ajira zenyewe za Elimu na Afya zilitangazwa hata hazifiki 20k kwa mwaka. Afu uniambie kuna kipaumbele hapo.
Hapo big no.
 
..ulikuwa na umri gani miaka ya mwisho ya utawala wa awamu ya kwanza?

..sera ya ubinafsishaji awamu ya 2 na 3 haikuchangia kushusha uchumi wetu.

..tulichelewa kubinafsisha viwanda vyetu kiasi kwamba vingi vilikuwa vimekufa kabla ya zoezi hilo kuanza.

..Jpm aliahidi Tanzania ya viwanda lakini hakuonyesha commitment yoyote kutekeleza ahadi hiyo.

Mm nadhan ni Bora kuheshimu na kudhamini mchango wa magu hata kama haujakugusa moja Kwa moja

Hakuna Rais ambae tafanya kila Jambo Kwa kuwagusa watu wote milion 45!

Jk alifanya mema na yahovyo, Magu alifanya mema na yahovyo, mama nae atafanya mema na ya hovyo!

Hata ww kwenye family yako, unafanya mema na yahovyo
 
Back
Top Bottom