Unyama, Ukatili na ufedhuli waliofanyiwa Wafanyabiashara wenye asili ya kiasia na Mashariki ya kati waliopo Dar haujawahi kufanyika kabisa
Watu walirudi kwenye 'Mkeka' wakashtaki kwa Hakimu asie na upendeleo na Majibu yakatoka kwa wakati
1983 ilipita dhulma mbaya sana watu wakavamiwa mjini wakaporwa mali zao fedha zao kwa kigezo cha uhujumu uchumi, watu walirudi kwenye 'Mkeka' wakalia kwa Mtenda haki Mkuu …less than 12 months later ajali ikatokea 'Goli likasawazishwa'
Tuache Dhulma…dhulma ni mbaya sana inaangamiza hadi kizazi…
kuna Mwingine kizazi chake kimejaa Vichaa kwa sababu ya dhulma aliyowafanyia watu…
kuna mwingine alikuwa Mwamba kichizi kuonea watu akitamba chezea Ndevu usichezee Serikali lakin leo hii hata choo cha chumbani kwake hawezi kukalia sink bila ya kushikwa Mkono na kukalishwa
Mafundisho ya kiislam yanatufundisha Dhambi ya Dhulma toba yake inaanza kwa kutaka msamaha kwa uliemdhulumu kabla ya kuomba kwa Mola wake, imagine umedhulumu uhai wa mtu hapo unamuombaje msamaha