Mtu Asiyejulikana
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 2,254
- 5,161
Toka Mnyika ni Mbunge wakati huo JPM alikuw Wizara ya Ujenzi. Mara nyingi alipenda kuongea na Mnyika akiwa Mbunge na kuchukua hoja zake kuzifanyia kazi.
Magufuli aligundua kuwa Mnyika alikuwa na uchungu hasa wa maendeleo ya watanzania. Na hili lilimfanya mara nyingi atamani Mnyika aje CCM.
CDM waligundua hili ndo kisa cha baadaye kumpa cheo alicho nacho sasa. Ushawishi ulikuwa mwingi lakini Mnyika aliendelea kushikilia msimamo wake wa kuwa Mpinzani.
JPM alipoingia madarakani alidokezwa jinsi ya kuishi na watu flani ambao ni wapinzani. Hawa aliwaambia wasibanwe sana. Wawe wanapewa kiasi flani cha pesa ili wasimkosoe sana.
Huu ni utaratibu ambao ulikuwepo ingawa si rasmi. Tunafahamu mara kadhaa ambazo Zitto alikuwa akiibuka na hoja flani alikuwa akipewa na Serikali ya kipindi kile kwa malengo flani.
Baada ya JPM kuingia madarakani walitegemea hivyo hasa Zitto Kabwe kuwa angeendelea kulelewa. Hata wenzie walipotoka Bungeni mnakumbuka Zitto alibaki na kuunga mkono Serikali ya Magufuli.
Alipoona kuwa nayeye pia hapewi Kamisheni yake alikwazika sana na hatimaye kuamua Rasmi kuasi. JPM aliitwa na kuambiwa "hawa mimi nlikuwa naishi nao hivi" yeye akasema hawezi ishi nao kinafiki na hatowapa hata Shilling moja ya watanzania.Ugomvi ukaanzia hapo.
JPM hakuwa akiwaamini wapinzani na alifikia hatua kuwachukia kutokana na undumilakuwili waliokuwa nao. But nadhani alipaswa aheshimu maisha waliyochagua wao.
Sasa wapinzani wanatafuta namna ya kumwingia Mama Samia. Lengo ni kuwa waweze anza pata mgao wao kama kawaida na kuepuka kusumbua Utawala wake. Mnavyoona akina Zitto wanahangaika n.k ni katika kutengeneza njia nzuri ya kuja pata pesa. Akitaka aende nao vizuri asiwe mkaidi. Awapatie chao kama jinsi ilivyokuwa watapunguza Upinzani kwake.
Hii nchi ina mambo mengi na waathirika wakubwa ni ninyi Watanzania Maskini ambao mnatumika sana na Wanasiasa. Sisi tulioko huku juu wakati mwingine tunawatizama na kusikitika sana.
Kazi Iendelee.