Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
HAYATTI MAGUFULI ALIKUWA NA UELEWA MDOGO WA MASUALA YA DINI, ASILAUMIWE.
Na, Robert Heriel.
Leo kijiweni kuna mada Moto ilikuwa ikiendelea inayohusu masuala ya UVAAJI WA BARAKOA, baadhi ya wachangiaji wa mada walimtumia zaidi Hayati Magufuli katika kutetea hoja zao kuwa hakuna ulazima wa kuvaa Barakoa, isipokuwa kumwomba Mungu pekee inatosha.
Vijana hawa niligundua wamepata elimu hiyo kutoka kwenye hotuba alizokuwa akizitoa Mzee wetu, Hayatti.
Hicho ndicho kimenifanya niandike andiko hili.
Kwanza nianze Kwa kusema kuwa, Hayati Magufuli kutokana na Hotuba zake alizokuwa akizitoa na matamshi yake, nachelea kusema Hakuwa na Uelewa, Elimu, ujuzi na maarifa ya mambo ya kiroho, Magufuli Hakuwa anaujua vizuri dini licha ya kuwa alikuwa akipenda Sana kumtaja mwenyezi MUNGU.
Na mtu yeyote ambaye anaufahamu mdogo, ujuzi hafifu, Uelewa Finyu na Elimu duni ya Kidini na Kiroho basi lazima mtu huyo awe Mpotoshaji.
Hii ni kusema Hayati alikuwa Mpotoshaji hasa wa masuala ya kiroho kwani Hakuwa na Uelewa mkubwa wa mambo hayo.
Sio ajabu ndio maana alikuwa akiwanyamba baadhi ya viongozi WA dini waliokuwa wakivaa Barakoa mpaka Kanisani. Tena alikuwa akiwadhihaki na kuwakejeli Jambo ambalo Kama angejua walau hata robo ya elimu ya Dini au mambo ya kiroho asingefanya hivyo.
Andiko hili limekusudia kuwaonya Wale wote waliokuwa wakimuamini Magufuli hasa kwenye kukataza matumizi ya Barakoa au Chanjo Kwa kutumia mgongo wa Kidini ati wamtegemee Mungu. Acheni Fikra hizo, huyo uliyemuamini Hakuwa na elimu ya Kidini wala kiroho.
Mungu hategemewi na wajinga, Mungu hategemewi na watu wasiomfahamu, wasiomjua, wasio na Uelewa naye, wasio na elimu yake, wasio na maarifa naye, Mungu hawezi kutegemewa na watu wa namna hiyo.
Neno la Mungu kasema; MJUE SANA MUNGU ILI UWE NA AMANI
Pia linaongeza kuwa Watu wangu wanaangamia Kwa kukosa Maarifa.
Kisha unaeleza pia, ya kaisari mpe kaisari; ya Mungu mpe Mungu.
Magufuli anaweza kuwa Bora kwenye Maeneo mengi tuu ambayo nilishawahi kuyaeleza lakini haimuondolei udhaifu wake wa kutokujua Elimu ya Kidini na Kiroho ambao huo ni udhaifu.
Hivyo Wale mnaofuata mafundisho yake na falsafa yake ya kutokuvaa Barakoa Kwa kutumia VIGEZO vya kiimani, VIGEZO vya Kidini mkae mkijua Mzee alikuwa anaelimu duni ya Kidini na Uelewa hafifu.
Hivyo msije mkaangamia Kwa kukosa Maarifa.
Pia nitoe onyo Kwa viongozi wengine wakisiasa, Kama huna elimu ya Jambo Fulani msipende kujifanya mnazielezea elimu msizozijua vyema, mnaathiri jamii.
Robert Herieli
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro