Hayati Magufuli alikuwa na uelewa mdogo wa masuala ya dini, asilaumiwe

Hayati Magufuli alikuwa na uelewa mdogo wa masuala ya dini, asilaumiwe

HAYATTI MAGUFULI ALIKUWA NA UELEWA MDOGO WA MASUALA YA DINI, ASILAUMIWE.

Na, Robert Heriel.

Leo kijiweni kuna mada Moto ilikuwa ikiendelea inayohusu masuala ya UVAAJI WA BARAKOA, baadhi ya wachangiaji wa mada walimtumia zaidi Hayati Magufuli katika kutetea hoja zao kuwa hakuna ulazima wa kuvaa Barakoa, isipokuwa kumwomba Mungu pekee inatosha.

Vijana hawa niligundua wamepata elimu hiyo kutoka kwenye hotuba alizokuwa akizitoa Mzee wetu, Hayatti.

Hicho ndicho kimenifanya niandike andiko hili.

Kwanza nianze Kwa kusema kuwa, Hayati Magufuli kutokana na Hotuba zake alizokuwa akizitoa na matamshi yake, nachelea kusema Hakuwa na Uelewa, Elimu, ujuzi na maarifa ya mambo ya kiroho, Magufuli Hakuwa anaujua vizuri dini licha ya kuwa alikuwa akipenda Sana kumtaja mwenyezi MUNGU.

Na mtu yeyote ambaye anaufahamu mdogo, ujuzi hafifu, Uelewa Finyu na Elimu duni ya Kidini na Kiroho basi lazima mtu huyo awe Mpotoshaji.

Hii ni kusema Hayati alikuwa Mpotoshaji hasa wa masuala ya kiroho kwani Hakuwa na Uelewa mkubwa wa mambo hayo.

Sio ajabu ndio maana alikuwa akiwanyamba baadhi ya viongozi WA dini waliokuwa wakivaa Barakoa mpaka Kanisani. Tena alikuwa akiwadhihaki na kuwakejeli Jambo ambalo Kama angejua walau hata robo ya elimu ya Dini au mambo ya kiroho asingefanya hivyo.

Andiko hili limekusudia kuwaonya Wale wote waliokuwa wakimuamini Magufuli hasa kwenye kukataza matumizi ya Barakoa au Chanjo Kwa kutumia mgongo wa Kidini ati wamtegemee Mungu. Acheni Fikra hizo, huyo uliyemuamini Hakuwa na elimu ya Kidini wala kiroho.

Mungu hategemewi na wajinga, Mungu hategemewi na watu wasiomfahamu, wasiomjua, wasio na Uelewa naye, wasio na elimu yake, wasio na maarifa naye, Mungu hawezi kutegemewa na watu wa namna hiyo.

Neno la Mungu kasema; MJUE SANA MUNGU ILI UWE NA AMANI

Pia linaongeza kuwa Watu wangu wanaangamia Kwa kukosa Maarifa.

Kisha unaeleza pia, ya kaisari mpe kaisari; ya Mungu mpe Mungu.

Magufuli anaweza kuwa Bora kwenye Maeneo mengi tuu ambayo nilishawahi kuyaeleza lakini haimuondolei udhaifu wake wa kutokujua Elimu ya Kidini na Kiroho ambao huo ni udhaifu.

Hivyo Wale mnaofuata mafundisho yake na falsafa yake ya kutokuvaa Barakoa Kwa kutumia VIGEZO vya kiimani, VIGEZO vya Kidini mkae mkijua Mzee alikuwa anaelimu duni ya Kidini na Uelewa hafifu.

Hivyo msije mkaangamia Kwa kukosa Maarifa.

Pia nitoe onyo Kwa viongozi wengine wakisiasa, Kama huna elimu ya Jambo Fulani msipende kujifanya mnazielezea elimu msizozijua vyema, mnaathiri jamii.

Robert Herieli
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
Usisahau kumalizia kwa kusema hayo ni maoni yako
 
Rais Magufuli alijitofautisha sana na Marais waliopita naamini ata kwa wanaokuja, Nisime Rais Magufuli alitumia 90% ya ubongo wake kuamua masuala ya kitaifa kuliko Marais wengine. Rais Magufuli hakuwa mtu wa kumpelekea karatasi asome na asaini hapana! Alikuwa mtu anaesoma asopopata majibu yakulidhisha alikuwa anatafuta majibu kwa njia zake.

Kuhusu issue ya Corona sioni sehemu yoyote yakumlumu cos angekuwa amekosea basi 60% ya wananchi wa ili Taifa tungekuwa hatuko Duniani, Ugonjwa wa Corona ni ugonjwa uliombatana na propaganda na ndiyo maana alipiga stop farmigation kuwa haiui kirusi lakini wakati anasema mkamtungia mpaka wimbo kumcheka kupitia wakina Roma mpaka WHO walipokuja kisema kuwa kweli farmigation hakiui kirusi cha Covid, alikataa Lockdown ata barakao alisisitiza kama kuvaa vaa uliyotengeneza hapa nchini. Leo ukiniambia Rais Magufuli alifail kwenye issue ya Covid nitakuomba unipe ulinganifu nani alifauru zaidi yake?

World Bank juzi amewahakikishia bara la Ulaya muwa atahakikisha kufikia 60% ya waafrika watakuwa wamepata chanjo ya Covid, Rais magufuli hakukataa kabisa chanjo ila alisema lazima tujilidhishe hipi ni sahihi kwetu! Sio mtu analeta chanjo huku anakupa mkopo alafu anakuambia kama unataka hii hela lazima uchukue chanjo ya Covid..! Na ndiyo maana ata ilani ya chama 2020-2025 iliona ielekeze serikali kutenga bajeti ya kutosha kwaajili ya utafiti NIMR.

Hayati Rais Magufuli alikuwa akituambia wazi tuendelee kuchapa kazi ila tujifukize, tungwe tangawizi ikibidi na mazoezi na kweli mi binafsi nilipata hicho kitu kinaitwa Covid wimbi la kwanza na niliponea kwa Tangawizi na malimao + kitunguu swaumu na sikuwai kulala ata siku moja eti nisiende kibaruani
 
Siyo Magu tu hakuwa na uelewa wa dini hata wewe hujui hata chembe, Afrika tuko sehemu mbaya sana ya kupokea kilakitu cha kigeni, ndiyo maana rafiki yake Nyerere baba wa taifa Mazedong au Maisetun yeye alifanya operesheni ya kinyama na ya kikatili haijawai kuonekana dunia ya kubomoa makanisa yote na na misikiti akisema kuondoa dini za kipagani nchini na wote tunaona wanabarikiwa na Mungu.
Acha kutaja dini mpaka tutakapotolewa utumwani ndiyo utaelewa.
 
Shida alikuwa much know,

Kujifanya kujua kila kitu, au kufanya kila kitu,.

Makinikia yeye
Korosha yeye
Wanafunzi wenye mimba yeye
Mungu yeye
Media yeye
Jeshi yeye
Bunge yeye

Hapo ndio tatizo lilipoanzia
... jack of all, master of nothing!
😅
1629108675427.png
🎯
 
Back
Top Bottom