Hayati Magufuli alivyoalika wazee wa kimila Ikulu kupiga dua(kutambika) ili mvua zinyeshe

Niliwahi kuwa na mtazamo kama wako ila baada ya kuishi Njombe na Iringa nahitimisha kuwa uchawi upo na mvua inachezewa tu na wazee wataalamu.

Sasa ww si ni muumini wa ushirikina, utaachaje kuamini hiyo mitazamo?
 
Tanzania bila story za uongo uongo kama hii haiendi
 


Unamtaka Mama aingize wachawi Ikulu??!!.

Nasikia Rais Mobutu Seseseko kuku ng'wendu wazabanga alipofanya mapinduzi ya kinyama Zaire (DRC) alikusanya Wachawi/Waganga mashuhuri kutoka kila pande ya Zaire kwenda Ikulu Kinshasa ili kila mmoja kwa wakati wake amfanyie tambiko la kukinga utawawala wake usiangushwe, Mobutu alikuwa mtu wa ajabu sana kwani inasemwa; baada ya kila mganga kufanya tambiko na kupewa ujira wake alimfuatilia kwa siri na baada tu ya miezi kadhaa karibu hao Waganga wote walioshiriki tambiko aliwaua kwa njama/assassination ili wasitoe siri za matambiko yao.

Mambo ya viongozi kushadidia matambiko tena ndani ya Ikulu aghalabu viongozi hao huelekea kuwa madikteta wabaya, mambo ya matambiko yalifanywa na madikteta karibu wote, sasa usitarajie Mama yetu awe dikteta kutokana na kuinajisi Ikulu kwa kuingiza Waganga na wachawi, kuingiza Wachawi ikulu kwa jambo lolote ni kukata tamaa za rehma za Mungu na kutegemea "rehma" za wachawi kitendo ambacho kitaamsha hasira za Mungu hasira zilizowakumba madikteta wote.

Cha kufanya ni; kila dini kwa wakati wake ipange siku fulani wafuasi wake wamuombe Mungu alete mvua, jambo ambalo liliwahi kufanyika katika utawala wa Alhaji Ally Hassan Mwinyi na tukayaona matokeo, hizi sio zama za giza tena bali zama za nuru.
 
Rudi Kwa Mungu toa neno uchawi weka Mungu


Then ujijibu mbn Mungu yupo mvua Amna nk
Mungu amemwumba mwanadamu akampa utashi na akili. Akamwekea kila rasilimali. Alikupa hivyo ili uvitumie kuyamudu maisha yako.

Mvua inanyesha, maji yanapotelea ardhini. Mito inatiririka, maji yanapotelea baharini. Maziwa yametapakaa, yamebakia kuwa makazi ya samaki na vyura.

Kuna wakati Mungu huruhusu magumu yatokee ili akili ya mwanadamu ifanye kazi.
 
Alipelekwa baharini?🤣🤣🤣
 
Pia na Kwa WACHAWI hivyo hulivyo wanaruhusu yatokeee
 
Kwenye ile sherehe mzee mmoja akaomba kilo tatu za nyama. Mwenye sherehe akasem huyo babu mpeni kilo nne za nyama. Wahinjaji wakamyima eti ni mchoyo. Sherehe ikaanza saa 6mchana nyie tulinyeshewa nvua non stop.

Mwenye sherehe akauliza kwani yule mzee hakupewa nyama? Wakajibu mchoyo yule aje ale na wengine, aiseee mwenye sherehe alichukuwa kilo tano fasta akakimbia kwa yule babu saa 10 jion mvua ikakata na miziki ikaanza.
Aiiiiiiii walokuja na nguo zao mpya ungeziona nyie msicheze na hawa wazee.
 
Mmmmh unapingana na necha? Kile kiti kinawaka moto. embu jaribu kuuliza wakubwa zako wakueleze siri sirini chief mwenyewe anakijua kilivyo cha moto wewe endelea kuimba hapa.
 
Wazee wa kimila ni neno la kupunguza ukakasi ru ila walitakiwa kuitwa wachawi tu
Nimecheka kama nawaona mlivyonyeshewa mvua
 
Kile chama Cha wale Gamboshi kilisema akijiyokeza mtu kumpinga Magufuli watamuua . Do you know what happened!
 
Mmmmh unapingana na necha? Kile kiti kinawaka moto. embu jaribu kuuliza wakubwa zako wakueleze siri sirini chief mwenyewe anakijua kilivyo cha moto wewe endelea kuimba hapa.
Huwezi kukalia kile kiti hata wiki bila kamati ya ufundi
 
Usirudie tena kuwaita wazee wankimila eti wachawi...jinga kabisa
 
Kama ni jiwe poa, mwamba si jiwe gumu? Yeye alikuwa Ile miamba mitatu uliyosoma katika jiografia inayoshikilia Dunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…