Ushirikina ni imani. Na imani kama hizo zinatumika sana kuwapumbaza watu.
Nimezaluwa kijijini, na mpaka leo, naenda kijijini si chini ya mara 2 kwa mwaka. Sijawahi kushuhudia habari ya eti kuroga ili mvua ije, lakini Nyanda za Juu Kusini, ndiyo eneo linalipata mvua nyingi kuliko maeneo mengi ya Tanzania. Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ukijumuisha na mkoa wa Tuvuma (Kanda ya Kusini), ndiyo eneo linalozalisha zaidi ya 70% ya chakula chote Tanzania. Zamani mikoa hii iliitwa, the BIG FOUR (Iringa, Mbeya, Rukwa na Ruvuma).
Mikoa hiyo, hata sasa, pamoja na shida ya upungufu wa mvua nchi nzima, inaendelea kupata mvua, na bila shaka, itapata mavuno ya kuridhisha. Kwenye hiyo mikoa yote, hakuna habari ya kuroga eti ili mvua inyeshe.
Kuroga ni ushirikina. Kiimani, huenda mikoa hiyo inayotegemea sana ushirikina, inaweza kuwa inakosa mvua kutokana na ushirikina uliokithiri. Ukweli ni kwamba maeneo mengi ambayo wakazi wake wengi ni washirikina, huwa hakuna maendeleo.
Kisayansi, yawezekana maeneo yenye matatizo makubwa ya mvua yapo katika maeneo ambayo kutokana na mgandamizo wa hewa, pepo zenye unyevu hazivumi kuelekea huko. Lakini pia yawezekana ni kutokana na ukataji mkubwa wa miti.
Uchawi ni fikra. Uchawi hauwezi kukupa mafanikio ya kudumu. Mobutu, timu ya Taifa ya DRC ilipopata nafasi ya kucheza Kombe la Dunia, alikusanya wachawi 200 maarufu kwenye nchi yake ili wakaroge, wapate ushindi. Na wakamhakikishia kuwa hiyo ni kazi ndogo. Timu yao ikafungwa magoli 11. Kama wachawi wangekuwa na uwezo ambao baadhi ya wenye imani za kishirikina wanaamini, basi Afrika tungeishinda Dunia katika kila jambo. Kama uchawi unafabya kazi, basi kazi hiyo ni kumwangamiza mwandamu, ndiyo matatizo ya kila aina hujirundika Afrika.