Hayati Magufuli alivyomtimua mpishi wa Ikulu usiku baada ya kuzidisha chumvi kwenye chakula

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Leo nimeukmbuka wimbo wa Super Rainbow ulioimbwa na Eddy Sheggs ¶akafatia na kuweka chumvi kwenye chai,tulikuwa na wageni wakatoka bila kuaga,akafatia na kuweka sukari kwenye mboga tukaona haviliki tukalala na njaa.¶

Back to the topic...uajua waafrika wengi ukifikisha umri wa kustaafu Miaka 56-60 magonjwa ya presha na kisukari huwa hayachezi mbali.

Sina uhakika kwa JPM ikuwaje ila ninachojuaalikuwa ameshauriwa apunguze matumizi ya chumvi kwenye chakula .

Niwarudishe nyuma kidogo.
Kopindi cha Hayati JK Nyerere ni kama kulikuwa na Ikulu mbili,ya msasani na ile ya magogoni,kuna baadhi ya shughuli alizifanyia msasani,moja ya hizo shughuli ni kuitwa kwa viongozi walioboronga kwenda kujieleza.
Enzi hizo kiongozi akiambiwa anaitwa Msasani anajua kama sio kufokewa basi ni kutumbuliwa,ilikuwa ni bora uitwe magogoni,viongozi wengi walikuwa wakisikia neno msasani mapigo ya moyo yanaongezeka,wengi walienda na LandRover au Peugeot za serikali wakarudi kwa miguu mpaka nyumbani..

Jibxo basi kulikuwa na wapishi pande zote msadani na magogoni,sio wapishi tu bali wahudumu wa Ikulu kiujumla.

Mara nyingi lunch alikula magogoni na dinner akalia msasani..

Sijui kuhusu mwinyi ila Mkapa alipoingia madarakani alijenga makazi rasmi ya Rais pembeni ya jengo kubwa la Ikulu.
Wapishi na wahudumu wote waliishia huko.hilo jengo lipo ndani ya fence ya ikulu kama unaelekea kwa mkemia mkuu au hospitali ya OceanRoad.

Sasa basi baada ya JPM kuingia madarakani kazi ya kumpikia chakula ikaanza.siku ya kwanza akanote kuwa chakula kina chumvi nyingi akatoa maagizo kuwa chimvi ipunguzwe.
Ikumbukwe ikulu kuna mtu analipwa mamilioni kwa kazi ya kuonja chakula cha mkuu dakika kadhaa kabla ya mkuu kula na hujulikana kwa jina la Tester.

Kwa hiyo huxu Tester nae alikuwa aware na hiyo order.
Siku chache za mwanzo mambo yakawa safi,ila kuna siku ndani ya wiki mbili tangu kuapishwa,chumvi ikazidi kwenye chakula,JPM akawaita wasaidizi wake wamuite mpishi wa zamu na Tester,yule mpishi machale yalishamcheza e kuambiwa unaitwa tu mapigo ya moyo yakaenda mbio mbio mpaka JPM akawa anayasikia.
Ila kwa vile Jom alikuwa mtu wa huruma akaagiza huyo mpishi na tester watafutiwe kazi nyingine.
Kesho yake akatangaza kwenye vyombo vya habari kuwa anaivunja timu ya waoishi na atapikiwa na mke wake nama yetu Janet,sababu alizotoa ni kuwa ni kubana matumizi.nadhani mnakumbuka hii kitu

Ila ukweli halisi aliongea vole kwa hasira tu,kitengo cha wapishi hakikuvunjwa na haiwezekani kuvunjwa,kiliendelea kuwepo mpaka mauti ilipomkuta ila walikuwa makini sana na chumvi kwenye chakula.

Mke wa Rais anaweza kumpikia mumewe ila sio mara zote maana na yeye xuko busy sana.

Sikumbuki yule baba mpishi alipelekwa kitendo gani baba wa watu
 
Huyo jamaa alikuwa na laana, nakumbuka alimfukuza mtunza tausi kisa tu JK alimchomekea kwa utani kwamba tausi hawaongezeki.

Huyo mtu ana laana, ndio maana mvua hainyeshi, labda Mungu kaamua kumuunguza na ardhi kabla ya moto
 
Kwenye Bwawa la Nyerere? Maji yatajaa tu wala usijali.
 
Huyo jamaa alikuwa na laana, nakumbuka alimfukuza mtunza tausi kisa tu JK alimchomekea kwa utani kwamba tausi hawaongezeki.

Huyo mtu ana laana, ndio maana mvua hainyeshi, labda Mungu kaamua kumuunguza na ardhi kabla ya moto
Ila unafurahia alivyoanzisha na sasa mnaendeleza!
 
Huyo jamaa alikuwa na laana, nakumbuka alimfukuza mtunza tausi kisa tu JK alimchomekea kwa utani kwamba tausi hawaongezeki.

Huyo mtu ana laana, ndio maana mvua hainyeshi, labda Mungu kaamua kumuunguza na ardhi kabla ya moto
Mwenye laana ni yule aliyechomeka uongo au aliyefukuza?, wewe ni KINEMBE KWELI,
 
Huyo jamaa alikuwa na laana, nakumbuka alimfukuza mtunza tausi kisa tu JK alimchomekea kwa utani kwamba tausi hawaongezeki.

Huyo mtu ana laana, ndio maana mvua hainyeshi, labda Mungu kaamua kumuunguza na ardhi kabla ya moto
Na sasa mikoa yote hakuna mvua na mazao yanakauka! Msio na laana sjui mtatuambia nini hili!

Aliyekuwa na laana mvua hazikukata
 
......
 
Attachments

  • _20230130_200043_1.JPG
    _20230130_200043_1.JPG
    19.1 KB · Views: 6
Ningependa kujua hayo makazi ya Mkapa yalikuwa wapi exactly. Nachojua Mkapa alikuwa na makazi yake rasmi ya siku nyingi sana hapo Sea View kama kilomita mbili tu kutoka Ikulu.

Lakini pia hilo la mpishi nafikiri ni kitengo kizima (au program ya Lishe?) ilivunjwa. Kuna taarifa ya gazeti hapo chini;
__________
RAIS John Magufuli amezifumua na kuziunda upya baadhi ya ofisi za Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam pamoja na kuwaondoa baadhi ya watumishi ambao hawana ulazima katika mfumo wa utumishi wa Ikulu. Taarifa za uhakika zilizolifikia MTANZANIA Jumamosi kutoka ndani ya Ikulu zimeeleza kuwa Rais Magufuli alianza kufanya ukaguzi wa ofisi moja baada ya nyingine zilizo Ikulu huku akitaka maelezo ya kina kuhusu shughuli zake na aina ya watendaji waliopo. Mmoja wa maofisa waandamizi wa Ikulu aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la jina lake kuhifadhiwa, alisema katika ukaguzi huo, Rais Magufuli aliamuru kufungwa mara moja kwa baadhi ya ofisi alizobaini kuwa hazina tija na kwamba zina watumishi ambao ni mizigo.

Ofisa huyo alizitaja baadhi ya ofisi zilizofungwa kuwa ni pamoja na iliyokuwa ikishughulikia chakula cha rais na ile iliyokuwa ikijihusisha na kupokea wageni binafsi wa rais. ?Rais Magufuli alipoingia tu Ikulu alifanya ziara ya kukagua ofisi zote zilizopo Ikulu, alitaka kujua utendaji kazi wa ofisi hizo lakini alipofika kwenye kitengo maalumu cha lishe ya rais alisema haoni umuhimu wa kuwepo kwa ofisi hiyo kwa sababu suala la lishe yake siku zote linasimamiwa na mkewe Janeth. Akaamuru ifungwe na watumishi wake warejeshwe walikotoka. Ofisi nyingine aliyoamuru ifungwe ni kupokea wageni binafsi wa rais. Alisema haoni tija ya kuwepo kwa ofisi hiyo kwa sababu mgeni anatakiwa kufika Ikulu baada ya kutoa taarifa, nayo aliamuru ifungwe,? alisema ofisa huyo.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa aliyekuwa mkuu wa kitengo cha lishe Ikulu amerudishwa katika ajira yake ya awali Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, huku watumishi wengine wakipelekwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Alipotafutwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kupitia simu ya kiganjani kuzungumzia hatua hiyo, simu yake iliita muda mrefu bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno ulionyesha kupokelewa kwenye simu yake lakini haukujibiwa. Alipoulizwa Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi, Premi Kibanga kuhusu kuwepo kwa hatua hizo alisema ni kweli Rais Magufuli alipoingia ofisini alianza kuipanga upya Ikulu kulingana na matakwa yake wakati wa utawala wake. Premi ambaye alizungumza na MTANZANIA Jumamosi kupitia simu yake ya kiganjani alisema wakati wa utawala wa Serikali ya awamu ya nne kulikuwa na ofisi maalumu ya lishe Ikulu ambayo hata hivyo ilikuwa haihusiani na uandaaji wa chakula cha rais.

Alisema ofisi hiyo ilikuwa mahususi kwa ajili ya ushauri kuhusu programu ya kimataifa ya urutubishaji wa vyakula kwa lengo la kupunguza tatizo la udumavu wa watoto. ?Ofisi hiyo ilikuwa inaongozwa na mtaalamu wa masuala ya lishe hata hivyo kabla ya Rais Kikwete kumaliza muda wake mtaalamu huyo aliacha kazi yake na kwenda kugombea ubunge huko kwao sasa ukiniambia amerudishwa Wizara ya Afya sitakuwa na jibu la uhakika kwa sababu sifahamu,? alisema Premi. Alipoulizwa kuhusu kufungwa kwa ofisi ya wageni binafsi wa Rais, Premi alisema ilikuwa na kazi ya kupokea malalamiko ya wananchi lakini Rais Magufuli ameamua kuiondoa kwa sababu ameweka utaratibu wa malalamiko ya wananchi kupokewa kuanzia ngazi za chini. ?Kama unavyojua Rais amekuja na dira yake ya ?hapa kazi tu,? hivyo anataka watendaji wa ngazi zote wawajibike kwa ufanisi.

Wakati wa utawala wa Rais Kikwete alifungua dawati hilo kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya wananchi, watu walitoka mikoa ya mbali kuleta kero zao hapa Ikulu lakini Rais Magufuli ameamua malalamiko ya wananchi yasikilizwe kuanzia ngazi za chini. ?Rais Magufuli anataka watendaji wote wa Serikali wawajibike kupokea kero za wananchi na kuzifanyia kazi. Zipo ofisi za madiwani, wabunge, wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ambao wote wanalo jukumu la kuwasikiliza wananchi na kuwatatulia kero zao,? alisema Premi.
 
Back
Top Bottom