Hayati Magufuli aliwezaje kukopa kwa Wazungu ikiwa aliharibu uhusiano na nchi za Ulaya?

Magufuli alikuwa anakopa zaidi pesa kutoka benki za kibiashara ambapo riba huwa kubwa na huko hawana tatizo na mkopaji, maana ni suala la kibiashara na sio kisiasa.
Lakini hata hivyo tuliingia uchumi wa kati na sasa tumeshuka ghafla.
Je, nani kichwa, anayekopa kwa riba kubwa halafu Nchi inaingia uchumi wa kati au yule anayekopa kwa riba ndogo lakini uchumi na mambo mengine yote Nchini yanaporomoka?
 
Economic leakage ni
1. Taxation
2. Savings
3. imports
While Economic Injections ni
1. Government Expenditure
2. investments
3. Exports
 
Wanasema Jpm alikopa halafu hela ikabaki nayo Serikali ,wapigaji hivi leo wanasifia wanasema Mama anakopa halafu pesa inafika kwako;-

Wanasema Jpm alitumia Contractionary economic Policies ndio zimeongeza umaskini kwa Watanzania..,
Sababu serikali ilikuwa inaondoa pesa kwenye mzunguko na kuzifungia benki kuu kuziachia katika mtiririko usio na usawa, hivyo pesa kuishia mikononi mwa Serikali haikufika kwa wapigaji,madowntown,misheni town na
Walamba asali
 
Kwani hakuna Miradi iliyojengwa kwa fedha za ndani? Unafahamu kama kuna Miradi ilifanyika kwa kuahirishwa shughuli fulani za Serikali na pesa kupelekwa kwenye hiyo Miradi?
Acha kukoleza uongo, mtu ambaye alidhulumu mpaka pesa za maafa kule Kagera ndiyo afanye miradi kwa pesa za ndani?
 
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Reactions: Tsh
Wakati wa JPM sera ilikuwa ni kupunguza kukopa na kutumia fedha zetu za ndani,na kwa mifani tuliona China ikichukua dhamana ya nchi ilizozikopesha ikaonekana China si mwema sana maana hana nia nzuri na Afrika,basi tupunguze kukopa China ili kuepukana na dhamana tutakayoweka kuja kuchukuliwa kama ilivyotokea kwa Sri Lanka, Zambia na Bandari ya Mombasa,Kenya baada ya kushindwa kulipa mkopo wa SGR.
 
Mwaka 1970 China walitusaidia kujenga reli ya Tazara,huku China kwa kipindi iko ikipitia kipindi kigumu cha uchumi mbaya katika nchi yao,Rais wa China, Mwenyekiti Mao alimwambia Mwalimu Nyerere "Ninyi mna matatizo kama sisi tu,lakini matatizo yenu ni tofauti na ya kwetu,lakini tutawasaidia kujenga reli ya Tazara hata kama sisi tutachelewa kuanza kujenga reli yetu,hivi leo Watanzania na Wazambia tumeshindwa kuiendesha reli hiyo ya Tazara,tunapaswa kujifunza kuitunza miradi mikubwa tunayojenga kwa mikopo na hili ndio lilifanya JPM achague kujenga SGR kwa kodi za zetu Watanzania bila kukopa kwa kipande cha Dar hadi Morogoro.
 
Tatizo la sasa awamu hii ni kwamba si nani anatukopesha bali anatukopeshaje,kwa masharti gani,tunaitumia mikopo hiyo kufanya nini,na pia tunapoona China ikiichukua Zambia au Kenya kwa kushindwa kulipa mkopo kazima tujifunze,maana madini yetu Watanzania yatachukuliwa yote kwa kushindwa kulipa mikopo,maliasili zetu zitakuwa mashakani kutwaliwa na Wachina kwa kushindwa kulipa mikopo yao,pengine pa kuangalia ni kusaini mikataba ya kimangungo wa Msovelo kwenda kusaini Ulaya na Dubai ndani ya jakuzi huku umelewa mvinyo matokeo yake unasaini kuiuza nchi yetu kwa kipande cha mkate,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…