Mkuu sang'udi, Kama uwezo upo ni sahihi kabisa, na sina tatizo kupata kiongozi mwenye uthubutu wa kiwango hicho na kwa hilo [emoji122][emoji122][emoji106][emoji106] kwa JPM(RIP)
Nitaandika kwa urefu ila tafadhali kama hutojali soma ili uelewe hoja yangu.
Pamoja na hayo aliyofanya, biashara hazikupaswa zifungwe, account za wafanyabiashara hazikupaswa zifungwe, mishahara kwa kiasi fulani ilipaswa iongezwe, huduma za uuzaji mazao hazikupaswa kuondolewa kwa wafanya biashara na kufanya ni state business na mengine mengi.
Nasema hivi kwasababu hivi ndivyo vitu vinavyomwezesha raia wa kawaida kufanya maendeleo binafsi na kurithisha vizazi vya mbele wakati yeye akiendelea kupokea pension ya uraisi na kushuhudia vizazi vyake vikifurahia urithi alioacha na akiendelea kupokea sifa za treni na ndege alizoacha.
NITAKUPA MFANO HAI WA MAMBO YALIYOTOKEA CHINI YA SERIKALI YA JPM:
Wote tunajua sheria zetu wakati mwingine huwa zinakuwa na mapungufu ya kuzitekeleza, mfano sheria za kuwataka wenye kampuni za consultancy wajisajili na VAT na waandae mahesabu bila kujali uwezo wa mtaji.
Kama mtu ana kakampuni kake ka sheria, kameajiri watu 5, sheria inamtaka aandae mahesabu kila mwaka na ajiunge VAT. Gharama ya kuandaa mahesabu si chini ya Tsh 500,000 mpaka 1,000,000 nje ya gharama za uhasibu, gharama ya kufile VAT si chini ya 50,000 mpaka 100,000 kila mwezi.
Sasa huyu mwenye kakampuni hakuwa akifile hesabu za mwisho kwa kutokujua au kwa kupuuza kwa sababu ya gharama za ukaguzi na uhasibu, na akawa anaenda kufanya makadirio kila mwaka kisha analipa kodi anaendelea na biashara kama presumptive tax payers wanavyofanya ilihali yeye ni corporate.
Sasa serikali kwa sababu ina marejesho ya mkopo wa reli ikatumia sheria ya kutokupeleka hesabu TRA ya adhabu ya Tsh 225,000 kila mwezi, na ikatumia sheria ya kutoa assessment kukadiria kodi ambayo huenda ingepatikana kwa kufanya examination of books of accounts.
Ikachukua % ya turnover ya miaka 5 ikaiita profit ikacharge penalty na interest kila mwezi ikapata makisio ya kodi ikajumlisha na zile 225,000 kila mwezi za miaka 5 na kumtaka mfanya biashara alipe plus interest each month for 5 years na kuzuia akaunti yake ya biashara huenda yenye pesa za wateja ikimlazimisha kodi ilipwe, mfanyabiashara akashindwa, biashara ikafungwa. Ukumbuke kwa huo mfumo uliotumika inaweza kuja hata kodi ya M40-M50, pesa ambayo mfanya biashara huyo hajawahi kuota kuishika kwa pamoja.
Kisheria raisi alikuwa sahihi na atakuwa alipata rejesho, ila katika uhalisia aliwanyima raia wake haki ya kufanya maendeleo binafsi kwa kuchukua mishahara yao huenda ya miaka 10 mbele ambayo wangelipwa kama angetumia busara na hako kakampuni kakaendelea kuwepo.
Sawa atapeleka rejesho ila, wale watu 5 ambao mshahara wao ameuchukua? Watoto wao mbeleni itakuwa vipi watakapokuta baba zao walilipia treni ila hawana pa kulala?
Sasa ukute baba anahako kakampuni na mama ni mwajiriwa kwenye kahoteli kalikokuwa kanategemea vikao vya wafanyakazi wa serikali vilivyopigwa marafuku kufanyika kwenye mahoteli hako kahoteli kakafungwa huku mzee wao akiwa anacheti cha darasa la saba akaondolewa kazini akiwa na miaka 57.