Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Salamuni wanangu janvini.
Japo Hayati John Pombe Magufuli hatarudi kujitetea tokana na madongo anayorushiwa na wasahaulifu wa nchi yetu, anao watetezi yaani legacy yake na Watanzania wenye mapenzi mema na taifa lao. Hivyo, hata kama hawezi kujitetea, wapo watakaomtetea hadi kieleweke.
Naleta uzi huu kusisitiza hili bila kujali nani watachukia au kukwazwa. Hivyo, wanaopoteza muda kumkandia na kumpa majina na sifa mbaya mwendazake, wajue na kufahamu, hawatafanikiwa. Miradi aliyoanzisha itamsemea. Watanzania watamsemea, wenye akili watamsemea wakati waso nazo wakimzomea. Madege aliyonunua yatamsemea.
Madaraja aliyojenga yatamsemea. Mabarabara yatamsemea, Meli zitamsemea, Umeme utamsemea. Hospitali na zahanati zitamsemea. Flyover zitamsemea na kuwazomea wanaomzomea. Tanzania, Afrina na Dunia watamsemea. Majengo hata ndege watamsemea. Wote watamtetea na kuwazomea wanaomzomea. Wengi watamkumbuka si leo wala kesho bali kwa muda mrefu.
Mpende au mchukie, Magufuli ameacha legacy isiyo ya kawaida kama alivyosema alhaj Ali Hassan Mwinyi mzee wetu au rais wetu SSH aliyewakemea wabunge kuacha ubuge na ujinga wa kumlinganisha na bosi wake. Mwenye akili na tie akilini. Menye macho na aone. Na mwenye masikio na asikie. Siombi radhi kwa haya nilonena hapa. Asanteni sana.
Naomba kuwasilisha kwa wenye akili.