MTK
JF-Expert Member
- Apr 19, 2012
- 8,924
- 6,854
Wanaomtetea dikteta ni dhahiri bin shayiri mnajaribu kuficha jambo! Kwani mbona hapajawahi kuwepo mjadala kuhusu awamu nyingine zote zilizopita? Mataga mnafikiri hazikuwa na mapungufu? Yalikuwepo lakini ya DIKTETA yamezidi kwa WINGI na UZITO wa UBAYA wake, ndio maana mataga mnashindana kutoa povu! Kwa mfano hakuna mtangulizi wa DIKTETA hata mmoja aliyewahi kuitwa DIKTETA, hakuna hata mmoja aliyewahi kupata tuhuma za kupoteza watu (hili alilikiri mwenyewe kwenye kikao cha uteuzi wake Dodoma na akalifanya kweli!!!), Watu kuuwawa, kupigwa risasi, ubadhirifu wa hatari, kuchafua diplomasia, kuwagawa watanzania, kusigina katiba, haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari, kuchekesha dunia kwa kuikana sayansi wakati kasomea sayansi! Na mengi mengineyo, haya ya miundo mbinu kuyapigia chapuo ni uzwazwa kwa sababu alichaguliwa kuwa akafanye hayo, na watangulizi wake walifanya mengi mengine, Dikteta hakuikuta nchi kama enzi za ujima aka "old stone age"! Mataga utetezi mnaofanya ni kama mnachota maji kwa Tenga? MNADEMKA vizuri sana!,View attachment 1758814Salamuni wanangu janvini. Japo Hayati John Pombe Magufuli hatarudi kujitetea tokana na madongo anayorushiwa na wasahaulifu wa nchi yetu, anao watetezi yaani legacy yake na watanzania wenye mapenzi mema na taifa lao. Hivyo, hata kama hawezi kujitetea, wapo watakaomtetea hadi kieleweke. Naleta uzi huu kusisitiza hili bila kujali nani watachukia au kukwazwa. Hivyo, wanaopoteza muda kumkandia na kumpa majina na sifa mbaya mwendazake, wajue na kufahamu, hawatafanikiwa. Miradi aliyoanzisha itamsemea. Watanzania watamsemea, wenye akili watamsemea wakati waso nazo wakimzomea. Madege aliyonunua yatamsemea. Madaraja aliyojenga yatamsemea. Mabarabara yatamsemea, Meli zitamsemea, Umeme utamsemea. Hospitali na zahanati zitamsemea. Flyover zitamsemea na kuwazomea wanaomzomea. Tanzania, Afrina na Dunia watamsemea. Majengo hata ndege watamsemea. Wote watamtetea na kuwazomea wanaomzomea. Wengi watamkumbuka si leo wala kesho bali kwa muda mrefu. Mopende au mchukie, Magufuli ameacha legacy isiyo ya kawaida kama alivyosema alhaj Ali Hassan Mwinyi mzee wetu au rais wetu SSH aliyewakemea wabunge kuacha ubuge na ujinga wa kumlinganisha na bosi wake. Mwenye akili na tie akilini. Menye macho na aone. Na mwenye masikio na asikie. Siombi radhi kwa haya nilonena hapa. Asanteni sana. Naomba kuwasilisha kwa wenye akili.