Hayati Magufuli anapaswa kupewa Heshima ya Baba wa Pili wa Taifa la Tanzania

Habari za wakati huu, ni matumaini yangu wote ni wazima wa Afya na mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa Tanzania.

Tukirejea kwenye mada...Aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Magufuli alikuwa ni kiongozi wa namna yake na kwa wakati muafaka ambao amekaa madarakani amefanya vitu vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine vimeleta mageuzi na mabadiliko makubwa kiuwajibikaji, kiuchumi na kijamii na kuwa chachu kubwa kwa ustawi wa kimaendeleo wa Taifa la Tanzania.

Hakika hakuna asie na makosa, nami nakiri kuna mahali ambako aliyumba lakini bado haiondoi uhalisia na ukweli kuwa alifanya hivyo kwa dhamira kuu ya kutetea na kupigania maslahi mapana ya Taifa letu sema kuna sehemu matokeo hayakuwa chanya japo lengo lake lilikuwa jema.

Tukijaribu kuweka katika mizani yale Mazuri na mabaya, kwa hakika mazuri ni mengi sana na mfumo wa utawala wake umejenga msingi imara kwa viongozi wengi waliopo sasa na watakaokuja baadae.

Inawezekana sio wote, ila wengi wetu ni mashahidi na tumeshuhudia mageuzi makubwa kwenye kuleta mabadiliko ya uwajibikaji serikalini, kuzuia rushwa na udanganyifu, Mfumo usio na upendeleo katika kutoa ajira, ujenzi na uboreshaji wa miundombinu yenye kuleta tija kiuchumi kama Bwawa la Nyerere na Reli ya SGR,Umeme vijijini, Uboreshaji wa huduma za Afya, Ongezeko la ukusanywaji wa kodi, uboreshaji wa mikataba ya madini na gesi na vinginevyo vingi ambayo vimefanikisha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati wa chini mapema tofauti na ilivyotarajiwa.

Kwa hakika umefika wakati wa Hayati John Magufuli kupewa Heshima ya Baba wa pili wa Taifa la Tanzania, baada ya waasisi wa Taifa na Muungano ili kuyaenzi daima yale mema yote aliyoyafanya kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na hatotukuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo kwani hata Korea Kaskazini wana Baba wawili wa Taifa, ila yote kwa yote neno langu sio Sheria, ni mawazo yangu tu, hivyo nawasilisha.
Ukimpa wewe heshima hiyo yatosha, sio lazima apewe na watu wote!

Nina maana hii; kipimo ulichompimia wewe na kuona kuwa anastahili hiyo heshima, binafsi sinacho na ninaamini walio wengi nao hawana hivyo, hawatamuona Kama ulivyomuona wewe.

We differ in perception!
 
Habari za wakati huu, ni matumaini yangu wote ni wazima wa Afya na mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa Tanzania.

Tukirejea kwenye mada...Aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Magufuli alikuwa ni kiongozi wa namna yake na kwa wakati muafaka ambao amekaa madarakani amefanya vitu vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine vimeleta mageuzi na mabadiliko makubwa kiuwajibikaji, kiuchumi na kijamii na kuwa chachu kubwa kwa ustawi wa kimaendeleo wa Taifa la Tanzania.

Hakika hakuna asie na makosa, nami nakiri kuna mahali ambako aliyumba lakini bado haiondoi uhalisia na ukweli kuwa alifanya hivyo kwa dhamira kuu ya kutetea na kupigania maslahi mapana ya Taifa letu sema kuna sehemu matokeo hayakuwa chanya japo lengo lake lilikuwa jema.

Tukijaribu kuweka katika mizani yale Mazuri na mabaya, kwa hakika mazuri ni mengi sana na mfumo wa utawala wake umejenga msingi imara kwa viongozi wengi waliopo sasa na watakaokuja baadae.

Inawezekana sio wote, ila wengi wetu ni mashahidi na tumeshuhudia mageuzi makubwa kwenye kuleta mabadiliko ya uwajibikaji serikalini, kuzuia rushwa na udanganyifu, Mfumo usio na upendeleo katika kutoa ajira, ujenzi na uboreshaji wa miundombinu yenye kuleta tija kiuchumi kama Bwawa la Nyerere na Reli ya SGR,Umeme vijijini, Uboreshaji wa huduma za Afya, Ongezeko la ukusanywaji wa kodi, uboreshaji wa mikataba ya madini na gesi na vinginevyo vingi ambayo vimefanikisha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati wa chini mapema tofauti na ilivyotarajiwa.

Kwa hakika umefika wakati wa Hayati John Magufuli kupewa Heshima ya Baba wa pili wa Taifa la Tanzania, baada ya waasisi wa Taifa na Muungano ili kuyaenzi daima yale mema yote aliyoyafanya kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na hatotukuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo kwani hata Korea Kaskazini wana Baba wawili wa Taifa, ila yote kwa yote neno langu sio Sheria, ni mawazo yangu tu, hivyo nawasilisha.
Mara zote Baba anakuwa mmoja tu.Hayati Magufuli alitekeleza Ilani ya CCM iliyomwelekeza afanye nini.Huwezi kumlinganisha hata kidogo na Hayati Baba original waTaifa Mwalimu Nyerere.Labda wengine walikuwa hawajazaliwa ndio maana hawajui aliyoyafanya MwalimuNyerere.Ukweli Hayati Magufuli hajafanya hata nusu yake.Mwalimu Nyerere atabakia kuwa Baba wa Taifa Pekee.
 
Nchi haiwezi kuwa na wababa wawili kama ilivyo familia kutoweza kuwa na wababa wawili. That's it!
Hakuna kisichoshindikana hata Korea Kaskazini wana Baba wawili wa Taifa, ni heshima anayopewa kwa kazi kubwa aliyoifanya ili iwe kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.
 
Habari za wakati huu, ni matumaini yangu wote ni wazima wa Afya na mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa Tanzania.

Tukirejea kwenye mada...Aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Magufuli alikuwa ni kiongozi wa namna yake na kwa wakati muafaka ambao amekaa madarakani amefanya vitu vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine vimeleta mageuzi na mabadiliko makubwa kiuwajibikaji, kiuchumi na kijamii na kuwa chachu kubwa kwa ustawi wa kimaendeleo wa Taifa la Tanzania.

Hakika hakuna asie na makosa, nami nakiri kuna mahali ambako aliyumba lakini bado haiondoi uhalisia na ukweli kuwa alifanya hivyo kwa dhamira kuu ya kutetea na kupigania maslahi mapana ya Taifa letu sema kuna sehemu matokeo hayakuwa chanya japo lengo lake lilikuwa jema.

Tukijaribu kuweka katika mizani yale Mazuri na mabaya, kwa hakika mazuri ni mengi sana na mfumo wa utawala wake umejenga msingi imara kwa viongozi wengi waliopo sasa na watakaokuja baadae.

Inawezekana sio wote, ila wengi wetu ni mashahidi na tumeshuhudia mageuzi makubwa kwenye kuleta mabadiliko ya uwajibikaji serikalini, kuzuia rushwa na udanganyifu, Mfumo usio na upendeleo katika kutoa ajira, ujenzi na uboreshaji wa miundombinu yenye kuleta tija kiuchumi kama Bwawa la Nyerere na Reli ya SGR,Umeme vijijini, Uboreshaji wa huduma za Afya, Ongezeko la ukusanywaji wa kodi, uboreshaji wa mikataba ya madini na gesi na vinginevyo vingi ambayo vimefanikisha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati wa chini mapema tofauti na ilivyotarajiwa.

Kwa hakika umefika wakati wa Hayati John Magufuli kupewa Heshima ya Baba wa pili wa Taifa la Tanzania, baada ya waasisi wa Taifa na Muungano ili kuyaenzi daima yale mema yote aliyoyafanya kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na hatotukuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo kwani hata Korea Kaskazini wana Baba wawili wa Taifa, ila yote kwa yote neno langu sio Sheria, ni mawazo yangu tu, hivyo nawasilisha.

Unaonaje Kaburu Pieter Botha akawa baba wa taifa wa Afrika kusini kutokana na maendeleo aliyofanya kwenye nchi ile?
 
Hili Jambo linamfanya JPM kuwa Raisi wa hovyo , hata wanaomshabikia hawaelewi kitu , Kikwete asifananishwe na Raisi mwingine aisee may be akina Nyerere hao ....changamoto yake hakuwa solid kwenye usimamizi

Kikwete aliajiri kila mwaka , Zaid ya wahitimu 100000 waliajiriwa direct from colleges ..... Barabara zilijengwa , watu waliiba mabillion ya pesa , na wenye juhudi walitajirika, na hakukuwa na Kodi za namna hii kama ya leo .....

JPM tunasmifia Kwa lipi wakuu? Tuwe wakweli , Ajira zipo totally stagnant, mzunguko wa hela mtaani ni terrible , Kodi zipo za kila aina, na deni la Taifa Kwa miaka mitano Tu iliyopita limezidi la kipindi kuanzia Mkapa mpak Kikwete combined together...... wastaaf wanataabika, wafanyakazi hawana hamu, matajiri na wafanya biashara wakubwa na wakati wote walikuwa hawana Amani wengine mpak walifunga biashara , akina dangote sjui hata wako wapi, ...... Hii ina maana hata barabara na miundo mbinu iliyojengwa ni ya mikopo , ...mtu kila sku kujitapa kwenye majukwaa na kutukana wazungu ......

Ukweli ni kuwa hela wanazo wazungu , Sisi huku tunadanganyana na kukamuana huku tukipeana matumaini hewa tuu....Baba amejifungia ndani kufokea wanawe, hamna kitu wakuu.... na hili kikwete alilijua , thus why mwamba alikuwa anaranda randa huku na kule kuleta pesa ....nimeishi nikiwa mtu mzima kwenye tawala zote mbili nachelewa kusema Kikwete ni the best president aiseee..... Ila kama tulilidhika na unyonge na tulitamani tuwe wanyonge forever basi tumsifu huyo JPM Ila Mimi hapana......labda kafanikiwa kuwatia hofu wafanyakazi ....

Alaf unanilazimishaje Mimi niishi nikitaabika Kwa ajili ya Tanzania ya Kesho ? Yaani nife kwenye umaskini Kwa ajili ya Tanzania ya Kesho ?? What a shit.... Tanzania ya Kesho itajengwa na wa kesho let us enjoy today .....
 
Ndugu mleta mada, wewe ni miongoni mwa watu wanaoweza kuleta mpasuko katika Taifa letu na jamii yake .
Hayo mawazo yako hayana busara hata kidogo.
Kila Rais aliyetumikia Taifa hili alifanya kazi iliyotukuka kwa muda wake aliomaliza.
Kila awamu imepiga hatua kubwa ya maendeleo, acha uzandiki kwa ajili ya kuendekeza njaa yako kwa mihemuko ya ku underrate viongozi wa awamu ya pili, ya tatu na ya nne, huo ni ubazazi.

Mungu ibariki Tanzania
 
Mleta mada
Ushauri kwako.... hamia Chato ukaunge ukoo
Usitupangie
Baba wa Taifa ni mmoja
Mbona Mkapa hamkuja na hili pendekezo? Maana alikuwa bora mara elfu kuliko huyu mnayempigia debe
 
Habari za wakati huu, ni matumaini yangu wote ni wazima wa Afya na mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa Tanzania.

Tukirejea kwenye mada...Aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Magufuli alikuwa ni kiongozi wa namna yake na kwa wakati muafaka ambao amekaa madarakani amefanya vitu vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine vimeleta mageuzi na mabadiliko makubwa kiuwajibikaji, kiuchumi na kijamii na kuwa chachu kubwa kwa ustawi wa kimaendeleo wa Taifa la Tanzania.

Hakika hakuna asie na makosa, nami nakiri kuna mahali ambako aliyumba lakini bado haiondoi uhalisia na ukweli kuwa alifanya hivyo kwa dhamira kuu ya kutetea na kupigania maslahi mapana ya Taifa letu sema kuna sehemu matokeo hayakuwa chanya japo lengo lake lilikuwa jema.

Tukijaribu kuweka katika mizani yale Mazuri na mabaya, kwa hakika mazuri ni mengi sana na mfumo wa utawala wake umejenga msingi imara kwa viongozi wengi waliopo sasa na watakaokuja baadae.

Inawezekana sio wote, ila wengi wetu ni mashahidi na tumeshuhudia mageuzi makubwa kwenye kuleta mabadiliko ya uwajibikaji serikalini, kuzuia rushwa na udanganyifu, Mfumo usio na upendeleo katika kutoa ajira, ujenzi na uboreshaji wa miundombinu yenye kuleta tija kiuchumi kama Bwawa la Nyerere na Reli ya SGR,Umeme vijijini, Uboreshaji wa huduma za Afya, Ongezeko la ukusanywaji wa kodi, uboreshaji wa mikataba ya madini na gesi na vinginevyo vingi ambayo vimefanikisha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati wa chini mapema tofauti na ilivyotarajiwa.

Kwa hakika umefika wakati wa Hayati John Magufuli kupewa Heshima ya Baba wa pili wa Taifa la Tanzania, baada ya waasisi wa Taifa na Muungano ili kuyaenzi daima yale mema yote aliyoyafanya kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na hatotukuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo kwani hata Korea Kaskazini wana Baba wawili wa Taifa, ila yote kwa yote neno langu sio Sheria, ni mawazo yangu tu, hivyo nawasilisha.

Tema mate chini
 
Ni fikra tu na maamuzi, National people's Congress walivyopiga kura kuibadili katiba na kuamua Rais Xi Jinping awe Rais wa Maisha mwaka 2018 na kuondoa ukomo wa mihula miwili ya Urais sio kama hawana viongozi makini wa kuliendesha Taifa hilo bali waliona kazi yake na wakamtofautisha na wengine wengi waliomtangulia (rejea historia ya China) Kwenye nchi yenye idadi ya watu Takribani Bilioni 1.5.

Vivyo hivyo lengo la uzi huu ni kutambua mchango mkubwa wa Hayati Magufuli kwenye Nchi yetu ambayo kwa kipindi kifupi alichokaa ameonesha tofauti kubwa kuzidi wengi waliomtangulia.
 
Back
Top Bottom