Koffi Yardley
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 620
- 496
Wewe tayari una Baba wawili na unahisi ni poa sio? KOMA😡😡😡😡😡
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ukiona sikuja na wazo hili basi tambua hajatosha kuvaa hivyo viatuMleta mada
Ushauri kwako.... hamia Chato ukaunge ukoo
Usitupangie
Baba wa Taifa ni mmoja
Mbona Mkapa hamkuja na hili pendekezo? Maana alikuwa bora mara elfu kuliko huyu mnayempigia debe
Ukilinganisha Nchi na familia unakosea, kuwa na Baba wa Taifa ni tofauti na Baba wa familia.Wewe tayari una Baba wawili na unahisi ni poa sio? KOMA😡😡😡😡😡
Hakika hakuna kitu kama Tanzania ya Kesho itajengwa na wa Kesho bali hakika itajengwa na wa Leo na itafaidiwa na wa keshoHili Jambo linamfanya JPM kuwa Raisi wa hovyo , hata wanaomshabikia hawaelewi kitu , Kikwete asifananishwe na Raisi mwingine aisee may be akina Nyerere hao ....changamoto yake hakuwa solid kwenye usimamizi
Kikwete aliajiri kila mwaka , Zaid ya wahitimu 100000 waliajiriwa direct from colleges ..... Barabara zilijengwa , watu waliiba mabillion ya pesa , na wenye juhudi walitajirika, na hakukuwa na Kodi za namna hii kama ya leo .....
JPM tunasmifia Kwa lipi wakuu? Tuwe wakweli , Ajira zipo totally stagnant, mzunguko wa hela mtaani ni terrible , Kodi zipo za kila aina, na deni la Taifa Kwa miaka mitano Tu iliyopita limezidi la kipindi kuanzia Mkapa mpak Kikwete combined together...... wastaaf wanataabika, wafanyakazi hawana hamu, matajiri na wafanya biashara wakubwa na wakati wote walikuwa hawana Amani wengine mpak walifunga biashara , akina dangote sjui hata wako wapi, ...... Hii ina maana hata barabara na miundo mbinu iliyojengwa ni ya mikopo , ...mtu kila sku kujitapa kwenye majukwaa na kutukana wazungu ......
Ukweli ni kuwa hela wanazo wazungu , Sisi huku tunadanganyana na kukamuana huku tukipeana matumaini hewa tuu....Baba amejifungia ndani kufokea wanawe, hamna kitu wakuu.... na hili kikwete alilijua , thus why mwamba alikuwa anaranda randa huku na kule kuleta pesa ....nimeishi nikiwa mtu mzima kwenye tawala zote mbili nachelewa kusema Kikwete ni the best president aiseee..... Ila kama tulilidhika na unyonge na tulitamani tuwe wanyonge forever basi tumsifu huyo JPM Ila Mimi hapana......labda kafanikiwa kuwatia hofu wafanyakazi ....
Alaf unanilazimishaje Mimi niishi nikitaabika Kwa ajili ya Tanzania ya Kesho ? Yaani nife kwenye umaskini Kwa ajili ya Tanzania ya Kesho ?? What a shit.... Tanzania ya Kesho itajengwa na wa kesho let us enjoy today .....
Ushamba ni jaribu!Sisii ni washamba. Ila tunaolinja Rais,Serikali Tanzania. Mabeyo, Sirro. Wanamlinda Samia Suluhu Hasaan.
Hamna kitu... Kujisifia tu ila kiuhalisia kaharibuAliyoyafanya ni mengi sana hakika ukiacha Baba wa Taifa, ni mengi aliyoyafanya kuzidi waliomtangulia.
Ukishakubali kuwa kuna mema na mabaya . Basi ujue daima UBAYA unafunika MEMA .Habari za wakati huu, ni matumaini yangu wote ni wazima wa Afya na mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa Tanzania.
Tukirejea kwenye mada...Aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Magufuli alikuwa ni kiongozi wa namna yake na kwa wakati muafaka ambao amekaa madarakani amefanya vitu vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine vimeleta mageuzi na mabadiliko makubwa kiuwajibikaji, kiuchumi na kijamii na kuwa chachu kubwa kwa ustawi wa kimaendeleo wa Taifa la Tanzania.
Hakika hakuna asie na makosa, nami nakiri kuna mahali ambako aliyumba lakini bado haiondoi uhalisia na ukweli kuwa alifanya hivyo kwa dhamira kuu ya kutetea na kupigania maslahi mapana ya Taifa letu sema kuna sehemu matokeo hayakuwa chanya japo lengo lake lilikuwa jema.
Tukijaribu kuweka katika mizani yale Mazuri na mabaya, kwa hakika mazuri ni mengi sana na mfumo wa utawala wake umejenga msingi imara kwa viongozi wengi waliopo sasa na watakaokuja baadae.
Inawezekana sio wote, ila wengi wetu ni mashahidi na tumeshuhudia mageuzi makubwa kwenye kuleta mabadiliko ya uwajibikaji serikalini, kuzuia rushwa na udanganyifu, Mfumo usio na upendeleo katika kutoa ajira, ujenzi na uboreshaji wa miundombinu yenye kuleta tija kiuchumi kama Bwawa la Nyerere na Reli ya SGR,Umeme vijijini, Uboreshaji wa huduma za Afya, Ongezeko la ukusanywaji wa kodi, uboreshaji wa mikataba ya madini na gesi na vinginevyo vingi ambayo vimefanikisha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati wa chini mapema tofauti na ilivyotarajiwa.
Kwa hakika umefika wakati wa Hayati John Magufuli kupewa Heshima ya Baba wa pili wa Taifa la Tanzania, baada ya waasisi wa Taifa na Muungano ili kuyaenzi daima yale mema yote aliyoyafanya kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na hatotukuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo kwani hata Korea Kaskazini wana Baba wawili wa Taifa, ila yote kwa yote neno langu sio Sheria, ni mawazo yangu tu, hivyo nawasilisha.
🚮Habari za wakati huu, ni matumaini yangu wote ni wazima wa Afya na mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa Tanzania.

Dikteta hana heshima.Heshima kaburini.Unamaanisha awe baba mvurugaji wa taifa?
Dikteta hana heshima.Heshima kaburini.Unamaanisha awe baba mvurugaji wa taifa?
Labda huna baba hau hujui maana ya baba. Kwa nini nyerere anaitwa baba wa taifa? Kwa sababu alipigania Uhuru wa nchi hii likazaliwa taifa linaloitwa leo Tanzania. Sasa huyo pombe amezalisha taifa gani?
Usituletee utumbo wako hapa. Kama unataka mfanye awe baba yako wa pili!Labda apewe hadhi ya baba yako mzazi!