Hayati Magufuli anashambuliwa kila kona. Siyo kesi, ila mambo yaende; yasipoenda wananchi watawazomea kila kona

Unahisi mambo gani yalikua yanaenda kwa kasi wakati wa Magufuli na yatakwama baada ya wakati wa Magufuli?

Spika ameshauri wasitishe ununuaji wa ndege kwanza maana zinaleta hasara.
 
Unahisi mambo gani yalikua yanaenda kwa kasi wakati wa Magufuli na yatakwama baada ya wakati wa Magufuli?
Sio swala la kuhisi .Muda ni mwalimu mzuri mno .Let us wait and see
 
Magufuli alikuwa mwizi na fisadi period
 
Utawala mpya unapaswa kupambana kuliondoa tabaka aliloliacha linakuwa kwa kasi la wanyonge kulitoa katika unyonge na kulipa maisha bora, hilo ndilo tabaka lake lililompenda sana
Unafikiri utaletewa hela nyumbani kwako? Kwenye miaka hii mitano watu wamenunua magari, wamejenga na kufanya mambo mengi ila lazima ufanye kazi
 
Tatizo kubwa ni kwamba, aliyoyafanya aliyasema kwa uwazi kwenye majukwaa na hotuba zake, lakini alivibana vyombo vya takwimu, vya habari, wapinzani, etc... HENCE WANANCHI TUKAKOSA WA KUTUAMBIA MAKOROKOCHO YAKE...

Leo hii imekuwa kama ilivyokuwa wakati anaumwa... hakuna aliyesema kwamba anaumwa na wengine walikamatwa kwa "KUZUSHA" mitandaoni kwamba anaumwa... GHAFRA TUKAJA KUPEWA TAARIFA YA KIFO, AS IF KAFA KWA AJALI, KUMBE WAPI...

The same to hili la leo.. hakukuwa na wa kusema WIZI, AU MADHAMBI YOYOTE YALIYOTOKEA SERIKALINI, na mbaya zaidi wengine walitudanganya kwa kutoa magawio kwa serikali. Na wengine (ATCL) wakasema Mwaka 2018 walipata faida ya Tshs 28B, lakini, lakini CAG kasema ATCL imepata hasara kwa miaka mitano mfululizo UKIWEMO HUO MWAKA 2018 ambao tuliambiwa walipata faida.......

Matokeo yake, madhambi yote yameekwa hadharani GHAFRA, halafu mengi kishenzi kwa wakati mmoja Yaani ATCL, TANESCO, SIJUI HATI CHAFU, etc... Unategemea nini?? Yaani ukilinganisha na aliyokuwa anayahubiri, NA HUU WIZI ULIOKUWA UKIENDELEA ndani ya serikali, LAZIMA USHANGAE... utakuwa wa ajabu sana kama utaona ni sawa wizi huu kutokea, KISA UMEONA FLYOVER YA UBUNGO.... hivi bila wizi, zingejengwa flyover ngapi kwa hela zilizopigwa???

Miradi aliyoianzisha ikiwekwa hadharani, tutakimbiana hapa.. SASA HII ILIWEKWA WAZI MINGINE ILIPITIA BUNGENI.. NIAMBIE ILE YA JUUKWAJU IPOJE? eg Uwanja wa Ndege Chato haukupita Bungeni etc
 

Vituo vyote vya afya nchini, hospitali nk havijavuka 500b, elimu bure kwa muda wote wa miaka mitano ni 1.4t, hiyo ni 2t. Meli, vivuko na ndege zate kwa pamoja ni 2t, hiyo ni 4t mpaka hapo. Miradi mikubwa yote miwili ya SGR & SG hajalipa mpaka sasa 7t maana hakuna mradi haya mmoja ulifikia nusu ya malengo. Hiyo ni 11t. Barabara zote hazijafika 2t, majengo ya taasisi nyingine zote kwa pamoja kama mahakama, shule, vyuo na jiji la Dodoma hajavuka 1t, hiyo ni 14. Miradi yote ya maji nchini havijavuka 3, hapa nimechanganya na aliyokuta kwa JK. Hiyo ni 17t.

Sasa tuje kwenye makusanyo, alisema anakusanya 1.3t@month. kama makusanyo yake ni hayo iweje deni lipande kiasi hicho wakati hajatoa ajira mpya? Upikaji wa data ulikuwa ni mkubwa, na mambo madogo ama ya wastani yalisifiwa sana ili kuhadaa umma kuwa ni mafanikio ya hatari.
 
To be fair kwa Magufuli na Samia nadhani ni vyema haya yakafanyika;

1. Rais aondoe team yote ya Magufuli , hii itamuwezesha kuja na watu anaowaamini na anaoona watafit kwenye vision yake na pia itawapunguzia mzigo team ya awamu ya tano kutengeneza mitazamo kinzani kwenye jambo moja.

2. Rais asimamishe miradi yote kwanza;

Aunde tume zake kama ile ya covid , ili zimshauri ni miradi gani ina tija na pia atuambie kama ataendelea nayo au la.

3. Atuambie yeye mwenyewe ana mipango gani ya maendeleo kwa Taifa.

Baada ya haya kufanyika , tutaendelea pale tulipoishia.
 
Marehemu alikua mwizi sana hata CAG anajua
 
Ndio Mana hata Mungu hawapendi wanyonge
 
Tunataka majizi aliyokua anawaimba, na wapiga dili wako walikua wa hawam ipi hii au enzi ipi? Nyie na huyu MZEE mmewachea akili mbaya watanzania, MUNGU shahidi ,Sasa ni je mangapi watz bado hawajajua,? Mawaziri wake wameishi mama peponi, vipi yeye aliishi vipi? Unanunua mandenge,wakati wananchi wako wafa njaa alafu yanatengeneza hasara, hii umekaa vipi mpaka kuandika haya, aisee MUNGU anawaona na malipo ni hapa dunian,na nasema wazulumaji wote wa serikali iliyopita mjipange MUNGU ataongea nanyi siku zaja, atalipa roho ya kila mtanzania ,na ndivyo ilivyo sio maneno ya if,
 
Mambo yataendaje wakati nchi imeachwa na madeni hadi CAG anapendekeza tusikope tena, yaani mtu ukope ili kujonyesha shujaa, waje walipe wengine waonekana wamekwama? Tutawaelewesha wananchi chanzo cha kukwama ikitokea tumekwama
 
Hebu tumuacheni jpm apumzike
Amejitahidi kufanya kwa level yake
Licha ya mapungufu lakini kuna mambo
Kwenye utawala yake yalifanyika

Ova
 
Umemshauri vizuri kwani bila hivyo itaonekana yeye ndiyo anayempinga kumbe ni kwakua watu wale wale wanafanya the opposite of what was there before
 

Watu wengi vijijini ndio wenye maisha magumu sana hapa nchini, sasa kama asilimia 80 ndio waliona matunda yake, mbona nchi hii ni masikini? Magufuli hakutegemea kura za wananchi, labda ukamdanganye bwege, kilichotokea kwenye uchaguzi kila mtu alikiona, ndio maana kwa kuujua ukweli huo akina Ndugai wanawataka wabunge wajadili ukweli wa hasara ya ndege na mradi wa Bagamoyo urejeshwe, maana wanajua kiongozi aliyepita alikuwa muongo na mpika data. Sasa kama aliishi kwa kupika data, angeshindwa nini kupika idadi ya kura?
 
Nilisema hapa kila siku kuwa “vita vya kiuchumi” na sijui “mabeberu” zilikuwa ni propaganda tu!! Sisi wenyewe ndio tukikuwa maadui wetu wenyewe, hatukufanya mambo inavopasikana - wazalendo ndio wanayaibua sasa.

Je hata maamuzi na uficho wa taarifa hizi alaumiwe beberu au jirani anayetuonea wivu??
 
Magufuli alikuwa kwenye ujenz wa nchi, hakutaka kelele kelele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…