Hayati Magufuli atakumbukwa kwa msimamo na maono yake kwa Taifa

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Pamoja na hoja nyingi zinazotolewa kuhusu aliyekuwa rais wa JMT hayati JPM, ukweli utabaki kuwa ukweli.
Magufuli alipigania maslahi ya taifa.
Alitetea wananchi wa hali ya chini (wanyonge)
Alikuwa mzalendo kwa taifa lake.
Alikubali kuonekana kama mtu asiyefaa ili mradi tu asimamie maslahi ya taifa.
Hakika tutamkumbuka daima kwa misimamo na maono yake bila kujali wangapi wangempinga!

Je, vijana wa leo, tunaweza kusimamia maono tuliyonayo hata kama wengi watatupinga? Au tutaamua kwenda kama dunia inavyotaka hata kama haituongozi kule tunakoelekea?

Screenshot_20220316-224128_1647460009532.jpg
 
Mwaka umekatika bt it look like yesterday...
Kuna mengi yamebadilika ambayo nahisi angekuepo yangefanyika tofauti na kwa kasi kubwa...

Kasi ya Utendaji imepungua na Kasi ya kupiga domo imeongezeka...zama hizi naweza kuchora ramani ya nyumba na nikajivunia kua ni mafanikio...[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Enzi za mawaziri kukimbizana site zimeisha..

Enzi za kujivunia uchapakazi na miradi mmoja baada ya mwingine sizioni tena now tupo bze mikutano, makongamano, warsha na Safari...

From hard workers to Mediocre in just one yr.

Yapo Mengi ya kukumbuka bt niseme tu God is good all the time, hawezi kuliacha jambo lifanyike bila kua na sababu zake...
Lifes goes on.....
Rest in Power A true Son of of Africa.
 
Kwa mauaji, utesaji na ukatili anaodaiwa kuufanya Magufuli basi hakuna kizazi kitamsahau au kupita bila kumlaani. Wapo watu ipo siku wataenda kulichapa viboko kaburi lake.

Hivi kama Magufuli alishajua kuwa huenda muda mfupi atakufa, kwanini hakutubu mbele ya watanzania ili watu wasamehe ukatili uliowahi kuufanya?
 
Naunga Mkono Hoja!.
P
Unaunga mkono hoja kuwa alikuwa ni mtu wa upendeleo? Watu wa Kimara wavunjiwe nyumba lakini wa Mwanza wasivunjiwe kwavile walimpigia kura!!! Alianza vizuri lakini pale alipoanza kuwapa kichwa wakina Bashite na Sabaya kufanya uhalifu kwa Jina lake , hapo ndipo alipojiharibia!

Magufuli became a changed man in his management approach immediately after returning from his RWANDA state visit!! He must have copied a thing or two from Kagame!!
 
Wapi Ben Saanane?wana JF mna pretend mno na maisha haya ni ya kinafiki mno, Ben Saanane alikua mwenzetu humu, binadamu mwenzetu, mtanzania mwenzetu na mwenye familia yake, nani humu anaweza ishi bila ya kuwa na familia yake around?,nimemwona Mr.Kingai naye akitoka nyumba takatifu!historia na wakati vitakuja kutuhukumu
 
Kwa mauaji, utesaji na ukatili anaodaiwa kuufanya Magufuli basi hakuna kizazi kitamsahau au kupita bila kumlaani. Wapo watu ipo siku wataenda kulichapa viboko kaburi lake.

Hivi kama Magufuli alishajua kuwa huenda muda mfupi atakufa, kwanini hakutubu mbele ya watanzania ili watu wasamehe ukatili uliowahi kuufanya?
Isingekua 17/03/2021, katiba ingebadilishwa na saba ya nyongeza ingepita na wanyonge la kufanya tusinge kuwa nalo.
 
Wapi Ben Saanane?wana JF mna pretend mno na maisha haya ni ya kinafiki mno, Ben Saanane alikua mwenzetu humu, binadamu mwenzetu, mtanzania mwenzetu na mwenye familia yake, nani humu anaweza ishi bila ya kuwa na familia yake around?,nimemwona Mr.Kingai naye akitoka nyumba takatifu!historia na wakati vitakuja kutuhukumu
Kingai ametufundisha kitu kunaitwa PGO.
 
Kwa mauaji, utesaji na ukatili anaodaiwa kuufanya Magufuli basi hakuna kizazi kitamsahau au kupita bila kumlaani. Wapo watu ipo siku wataenda kulichapa viboko kaburi lake.

Hivi kama Magufuli alishajua kuwa huenda muda mfupi atakufa, kwanini hakutubu mbele ya watanzania ili watu wasamehe ukatili uliowahi kuufanya?
Kwanini wakati huo rais alituhumiwa moja kwa moja tofauti na sasa?

Kuna vijana wanapotea, wengine wanauawa ama kufungwa kwa madai ya ugaidi; kwanini hatajwi rais kuhusika?

Au ndio kusema, tusiyoyajua ni mengi kuliko tuyajuayo? Na kwamba siasa za nchi yetu zimejaa propaganda nyingi kuliko ukweli/ uhalisia? [emoji848]
 
Ukigusa maslahi ya 'beberu' lazima ushughulikiwe kikamilifu, na njia mojawapo ni kutumia vyombo vya habari kupiga propaganda chafu. Hebu fikiri kiwango cha shutuma na lawama ambazo zingevuma kwenye vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa alichofanyiwa Mbowe (kuwekwa gerezani) awamu hii, kingefanyika awamu iliyopita.
 
Pamoja na hoja nyingi zinazotolewa kuhusu aliyekuwa rais wa JMT hayati JPM, ukweli utabaki kuwa ukweli.
Magufuli alipigania maslahi ya taifa.
Alitetea wananchi wa hali ya chini (wanyonge)
Alikuwa mzalendo kwa taifa lake.
Alikubali kuonekana kama mtu asiyefaa ili mradi tu asimamie maslahi ya taifa.
Hakika tutamkumbuka daima kwa misimamo na maono yake bila kujali wangapi wangempinga!

Je vijana wa leo, tunaweza kusimamia maono tuliyonayo hata kama wengi watatupinga? Au tutaamua kwenda kama dunia inavyotaka hata kama haituongozi kule tunakoelekea?View attachment 2153375

Kazalisha Sabaya,Makonda ..........bora aliondoka aliharibu nchi.
 
Kwa mauaji, utesaji na ukatili anaodaiwa kuufanya Magufuli basi hakuna kizazi kitamsahau au kupita bila kumlaani. Wapo watu ipo siku wataenda kulichapa viboko kaburi lake.

Hivi kama Magufuli alishajua kuwa huenda muda mfupi atakufa, kwanini hakutubu mbele ya watanzania ili watu wasamehe ukatili uliowahi kuufanya?
Umenena vyema watanzania sasa tuna amani ujue watu waliishi kwa woga sana nimeona hata mke wake amenenepa aisee kumbe alikuwa anapumulia jujuu kama sisi.Pole mama Janet Mungu akutie nguvu
 
Pamoja na hoja nyingi zinazotolewa kuhusu aliyekuwa rais wa JMT hayati JPM, ukweli utabaki kuwa ukweli.
Magufuli alipigania maslahi ya taifa.
Alitetea wananchi wa hali ya chini (wanyonge)
Alikuwa mzalendo kwa taifa lake.
Alikubali kuonekana kama mtu asiyefaa ili mradi tu asimamie maslahi ya taifa.
Hakika tutamkumbuka daima kwa misimamo na maono yake bila kujali wangapi wangempinga!

Je vijana wa leo, tunaweza kusimamia maono tuliyonayo hata kama wengi watatupinga? Au tutaamua kwenda kama dunia inavyotaka hata kama haituongozi kule tunakoelekea?View attachment 2153375

Mauaji,Utekaji,Wasiojulikana,Upendeleo,Ukabila,Kujisifia,Wizi wa Kura,Kubambikia wapinzani kesi,Kununua Wapinzani,Kuongea hovyo hovyo ni baadhi ya mambo tutakayokosa.

1. Chato International Airport
2. Chato National Park
3. Chato CRDB
4. Chato Bohari ya madawa ya kanda
5. Chato VETA
6. Chato Hotel TANAPA
7. Chato Zimamoto
8. Chato Hospital rufaa
9. Chato Mahakama
10. Chato 🚦
11. Chato .....

Bwana yule alichezea kodi zetu,bora kaondoka hana maana kabisa.
 
Back
Top Bottom