Hayati Magufuli atakumbukwa kwa msimamo na maono yake kwa Taifa

Pengo lake halina spea, serikali yake ilisifika kwa utekelezaji serikali ya sasa hivi inasifika kwa maneno na malalamiko mengi bila utekelezaji.

Wale wenye mimba zako za chuki kwenye vichwa na mawazo yao, waliodai "hamna uhuru wa kujieleza ",baada ya kuingia Mama wakadai sasa hivi kuna uhuru wa kujieleza, cha ajabu.

Pamoja na uhuru wakujieleza.
1.Mgao wa umeme kimya
2.Mgao wa maji kimya.
3.Tozo kimya.
4.Bei ya mafuta imepanda tokea mwaka jana mwishoni, amabayo imegusa bidhaa nyingine kimya.
5.Watu wanajipigia hela plus utendaji na uwajibikaji wa watumishi umepungua kimya.

Unajiuliza sasa uhuru wa kuongea walikuwa wanaudai katika mambo gani, ikiwa mambo yanayo yagusa wananchi hawaongei labda may be uliwabana sana kwenye issues zao za Magendo.

Bahati kwa nature ya kazi yangu nimezunguka sana baadhi ya mikoa,nimeshudia hospitali ulizojenga kila wilaya, mahakama kila wilaya barabara za kisasa,nimeshuhudia majengo mapya ya ofisi za wakuu wa wilaya na wakurugenzi na zaidi nilishuhudia barabara ya km 50 ya zege kuelekea Ludewa.

Pumzika tu ila pengo lako halina spea, vitu ulivyo vifanya vinaonekana huitaji kutumia nguvu.

RIP Chuma John Pombe Magufuli.
 
Uchafuzi na wizi wa chaguzi ndìo hitimisho la huyo "mwamba". Mzee wa sauti moja tu, nyingine fyekelea mbali.
 
Mimi kwa JPM nampongeza tu kwa uthubutu wake tu lakini akili ya uongozi hakua nayo na swala eti alipigania wanyonge hakuna kitu kama hicho kwa Sababu yeye ndo kaongeza umasikini kwa wanyonge zaidi ya hapo alikua bingwa wa kusema uongo na wajinga wakaona uongo wake ndo ukweli.Kama asingekufa basi nchi yetu ilikua unaenda kuangamia .
 
Ametuachia bunge la Kijani
 
Usisahau katuachia na bunge la Kijani
 

atakumbukwa sana mpaka sasa hivi kwenye ligi ya urais makufuli anaongoza akifuatiwa na nyerere
 
Aturudishie Kwanza aliowapoteza
Hata yeye hivi sasa hayupo tena ! Lakini maisha yanaendelea na pia Mimi na wewe iko siku tutaondoka na maisha yataendelea kama kawaida !! Kila MTU ana mabaya yake na mazuri yake tujitahidi kujifunza kuchukua yale mema ya watu katika jamii na kuyaendeleza na pia kujifunza na kuyaacha yale yote mabaya ya Hao watu katika jamii !! Iwe ni kwa viongozi au kwa watu wa kawaida hakuna aliyekamilika !! "
 
Naunga mkojo hoja
 
now tupo bze mikutano, makongamano, warsha na Safari...
Mkuu huku kuna pesa ee acha asee...

YYaani ndiyo maana watu hawakumpenda yule mzee, posho ahahaaaa acha kabisa.
 
Acha propaganda hizo wewe?
 
Mungu alituepusha na hiki kikombe Cha uovu!!, Leo Bungeni ingekuwa tiali muswaada umepitishwa Rais wa wanyonge atawala milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…