Hayati Magufuli baada ya kivuli chako kufichwa ghafla

Nimekuuliza hamumwamini sieijii?

Mlikua brainwashed na yule mchawi?
 
Na muamini Bwana Yesu tu sio CAG mwenye historia ya kufurushwa TRA. Anaweza kutumiwa kirahisi sana tu.
Teh teh teh unajua CAG ni nafasi ya kuaminiwa sana? Yule mchawi alieviligwa kwenye kigozi kule chato aliwaharibu vibaya mnooo
 
Teh teh teh unajua CAG ni nafasi ya kuaminiwa sana? Yule mchawi alieviligwa kwenye kigozi kule chato aliwaharibu vibaya mnooo

Subiri huu ni mnara wa Babeli bwashee unaendelea kujengwa na hawa wanaoujenga hakuna mwenye akili kumzidi Nimrod.
 
Taarifa ya CAG haiwezi kufuta maona na uthubutu wa JPM. Ngoja tumpe muda mama.
 
Nenda, Baba,JPM. Sasa unapigwa mawe kila kona. Najua, watakupiga sana mawe sasa, lakini baadaye mawe hayo hayo yatarudi na kuwadhuru wao wenyewe.
Kazi Mungu huwa haidhihakiwi.
 
JPM hakuwa mtu wa kawaida kama wanavyodhani.
JPM alikuwa ni mtu wa pekee sana.
Hata wakimchafua kwa mbinu zote wanazozijua, kamwe hawawezi kumfikia JPM hata kwa moja ya elfu moja.
Spirit ya JPM imeingia kwenye damu za Watanzania wazalendo kwa hiyo huwezi kufuta kumbukumbu ya JPM kwa trick za hali ya chini kama hizo.
 
Vetting uliyoisema kwa makamu wa Rais huwa haipo sirias sana kwa kuwa kwanza
1:- kama alivosema mkuu wa mkoa wa Mbeya,alijua Rais akiwa madarakani hawezi kufa, kwa hiyo wanajua makamu wake atakuwepo kama pambo tu,

2:- katiba nayo imemchukulia makamu mtu poa tu nadhani ni kwa sababu kama hiyo hapo juu ya mkuu wa mkoa

nakumbuka ziara mbalimbali mikoani,watumishi walikuwa wanaogopa akienda waziri mkuu lakini siyo makamu wa Rais

mchakato wa kumpata mgombea urais kwa vyama kama ccm,huwa tunaona unachukua miezi kadhaa,kumpata mtu sahihi aliejiandaa na ameenda na ajenda zake za kuwafanyia watanzania...ila kumpata mgombea mwenza wanaingia wazee wa ccm kwenye kachumba hivi ndani ya dakika 5 wanarudo na jina, sababu kubwa ni kama aliyoisema mkuu wa mkoa wa Mbeya

Hapo ndiyo linapotokea la kutokea mnakuja kupata Rais ambaye wala hakuwa na mpango na huo urais,so anaweza kuwa anadandia ajenda yoyote maana hakuwa na ajenda tangu mwanzo.naunga mkono vetting kali ifanyike
 
Hawa jamaa waache wacheze na akili za watz walioamka, watayakimbia madaraka yao wenyewe wasipojirekebisha, muda ni hakimu mzuri 💪!
 
Hii inaweza kuwa imeongezewa vikorombwezo vingibe ili kukidhi mahitaji ya kisiasa yaliyopo hapa nchini sasa na baadaye. Moja likiwepo la kushindana na marehemu aliyelala kaburini. Siasa ni mchezo mchafu zingatia sana hilo akilini.
Mataga poleni sana!!kubalini tu, kuwa yameshatokea!!hiyo ripoti ya CAG, yaongezwe ili iweje, kwani ya 2018/2019, nayo si ilikuwa hivyo hivyo akaimaliza kitemi kwa kumtimua CAG?jipya ni lipi, ?
 
Kwani mwendazake alikuwa na mpango na urais!?ndio maana alishasema kuwa alikuwa anajaribu tu," AKAVUTIWAMO"na matokeo yake tumeyaona, bora hata huyu mama hakuwa na mpango huo lakini anaonyesha dalili njema!!huyo wenu alikuwa na agenda gani ya kueleweka zaidi ya kuifanya nchi isiyo TABIRIKA"kwani hamfuati sheria tena bali ni mawazo yake!!!
 
Umesikia lakini ripoti ya CAG leo?

Acheni ujinga , huwezi kuzuia watu wasiseme halafu ukawa ni msafi.
Kwani hiyo ripoti Ni ya kwanza? Halafu huwezi kumlaumu Rais kwa makosa ya watendaji. Kama angekuwepo angewawajibisha, Kama jinsi aliyepo atakavyowawajibisha!!
 
Natamani hadi hicho kivuli kisionekane kabisa,wajinga nyie.
Kifo kimemdhibiti huyu mwizi. Ameiba kila sekta
Magufuli kufa kabisa nisisikie hata hili jina
Je wewe utaishia wapi? Mungu akusamehe kwa kuwa hujui ulisemalo! Lulu iliyokuwa inang'aa mataifa mengine yanatushangaa tunavyobeza!! Leo hii Walibya wanamkumbuka na kumlilia Gadafi! Lakini alipouawa walishangilia!!
 
Nenda baba tutakukumbuka.
Tutakukumbuka kwa mema Wala si kwa mabaya Kama ulivyosema! Natamani isiwepo namna ya wewe kuwasikia Wanavyosema uliowaamini, waliokuwa wanakusifu, waliokulilia kumbe yalikuwa ni machozi ya mamba! Wanashindana kukufunua nguo!!
 
Mkuu umeandika Ninaçhowaza,tutakuja kukumbushana hapahapa after 2 years.
🙏😰RIP MAGUFULI
 
Ukweli huwa hauna tabia ya kujificha hata ingetumika nguvu kubwa kiasi gani... uongo huwa hauna tabia ya kujificha siku zote...
Kwanini waitwao "wanyonge" wana maduka makubwa barabarani na nje ya maduka ya walipa kodi? Je nchi inapaswa kuishi pasipo utaratibu? Je ripoti ya CAG na kauli ya Spika haioneshi kuwa u miongoni mwa WAPOTOSHAJI
 
Subiri kidogo bado tupo busy tunakula nondo za ripoti ya CAG.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…