Hayati Magufuli, kama sio leo basi ni suala la muda tu kupewa tuzo ya heshima kama Rais aliyesimamia vema rasilimali na kupunguza kero kwa wananchi

Hayati Magufuli, kama sio leo basi ni suala la muda tu kupewa tuzo ya heshima kama Rais aliyesimamia vema rasilimali na kupunguza kero kwa wananchi

Kizazi cha kupatana na ccm akili zao zinawarudi sasa

Sasa wanausema ukweli kwamba hakuna kama Magufuli linapokuja suala la ufisadi
 
Ulinzi wa rasilimali zetu, sasa ni dhahiri serikali iliyopo imeshindwa kuzilinda, matokeo yake inagawa tu sasa

Bandari zetu nazo zinageiwa wawekezaji tena ktoka nchi moja tu kwa Bandari zote nchini
 
Huu ndio wakati sahihi wa kuutambua mchango wa JPM katika Taifa hili

Nini sasa kinachoendelea baada tu ya miaka miwili kutokuwepo kwake
 
Nina mengi sana nimejifunza kwa JPM kweli hebu kila mtu kwa nafasi yake atende mema,aishi kweli yake

hutoambiwa/hawatosema sifa zako ukiwa hai ila sifa zako zitakufata huko uliko,Hakika JPM huko aliko anapokea

ving'ora vya tuzo asee,huwezi eleweka sasa ila ni swala la Muda tu,tutendeni mema na kweli,Haki yetu tutaipata hata tukiwa chini ndani ya Ardhi.
 
Kama alivyowahi kunukuliwa akisema, Jengo la Tanesko ubungo, akitokea kiongozi mwenye kusimamia sheria, litavunjwa tuu, na hatimaye akaja kushika mwenyewe na likavunjwa,

Na sasa, akija kutokea Rais asiye na unafki ndani yake, lazima JPM atapewa tuzo!

Tunaposema JPM (hayati) anastahili tuzo ya heshima kuhusu kulinda rasilimali na kufanikiwa sana kupunguza kero Kwa wananchi tuna maanisha

Kipimo ni hizi hizi tawala zilizokuwepo na zilizopo!

Staki nirudi nyuma huko kwenye Richimondi, Epa, escrow n.k

Huko nyuma kulinuka wizi nchi nzima, huduma za hovyo kila pahala, viongozi watu waliitwa majina mengi, miongoni mwao ni wazee wa kuchekacheka n.k

Tukija hapa tulipo, bila shaka hakuna hata mmoja asiyepata majeraha makali ya tozo na kodi zisizo na majina, huduma mbovu mahospitalini, ukipeleka wagonjwa unakutana na madaktari walioko chuo wakisoma bado na wengine wakiwa field, utampangaje zamu dakitari anayesoma bado kuhudumia mgonjwa siriaz? Matokeo yake ni wagonjwa kufariki ama kuzidiwa Kwa sababu ya mambo ya kizembe kama hayo

Ukija kwenye suala la nishati ya umeme, Hayati alipondwa Kwa maneno yote kwamba alikuwa mkamuaji tu wa maziwa bila kumlisha ng"ombe ili anenepe na kuendelea kutoa maziwa mengi, tukadhani ni kweli wasemacho, na tulipewa miezi miwili ya ukarabati wa miundombinu yote ya Mitambo ya TaNesco, miezi hiyo ikaisha, kilichofuata, kila mtanzania ni shahidi

Tukirudi kwenye uwekezaji wa uzalishaji wa Umeme JKHP, kulisemwa lugha mbalimbali baada tu ya kuingia wajuvi, tukaamini labda huwenda ni kweli,

Kabla ya wajuvu kuingia, tulikuwa tumepewa na tarehe ya kujazwa maji bwawa hilo, wajuvi walipoingia, tukaambiwa, bwawa hilo halitajazwa ispokuwa kuagizwe kifaa ambacho nchini hakipo, sasa ni karibu mwaka toka kuagizwe kifaa hicho cha kusaidia kujazwa maji bwawa letu na bado mpaka sasa hakuna cha maji kujazwa na sina hakika kama hata hicho kifaa kilishagakuja!

Kiukweli, tunahitaji kuona kila kinachokuwa kimesemwa, kinafanyika na kinaanza kutumika!

JPM, (hayati) alikuwa akisema, tayari kitu kinafanywa na kinanza kutumika Kwa manufaa ya nchi, hakuwa mtu wa porojo,

Ukweli na matendo yake mengi ya kitendaji, yaliufunika uwingi wa udhaifu wake na kuanza kuaminiwa saana na wananchi hasa wale waliokuwa hawapati haki zao kwenye tawala zilizowahi kuwepo

mf, wamama ntilie, wamachinga, wafugaji na wakulima, waliiamini sana serikari yake! Migogoro mingi ya wafugaji na wakulima, migogoro ya aridhi ilidhibitiwa na kusababisha kutamalaki Kwa amani

JPM (hayati) alihakikisha kuwa, Rasilimali za nchi, zinalindwa Kwa nguvu zote na kwamba, ziwanufaishe wananchi na kwamba, nchi yetu inakuwa ni kituo cha mataifa mbalimbali kuja ama kuleta madini yao kuja kuuza na kununua hapa

JPM (hayati) alianzisha masoko ya madini kila eneo lnalochima madini nchini, Sielewi Kwa sasa ikiwa maono haya makubwa yanaendelezwa Kwa kasi ilelie

Tubayo mengi mazuri ya kujifunza Kutoka Kwa kiongozi huyu ambapo Kwa wengi wa watanzania hata sasa bado wanamnena kusema, laiti angelikuwepo?

Tusingeona tozo katikati ya mdoloro wa kiuchumi duniani,

Swali ni... Ikiwa kuna mdorolo wa uchumi duniani,

Je, Wananchi mdororo huu hauwaathiri? Kwa nini waongezewe tozo ili hali dunia inapitia uharibifu wa Uchumi?
" Watanzania mtanikumbuka,na Tena mtanikumbuka kwa mazuri na si mabaya kwasababu nime sacrifice maisha yangu kwa wananchi masikini"
 
Huyu mwamba, asingekubali wamaasai kufukuzwa pale ngorongoro, kwa sababu ya uhusika wao na namna wanavyoishi na wanyama
 
Huyu mwamba, asingekubali wamaasai kufukuzwa pale ngorongoro, kwa sababu ya uhusika wao na namna wanavyoishi na wanyama
Tena magu angewafukuza nakuwatoza faini juu angalia alichofanya kwasisi wavuvi ziwatanganyika uvuvi wakipe niuvuvi salama kabisa hufanyika usiku tena kwenye kinakirefu chamaji na tunatumia leseni lakini jamaa ametufirisi
 
Back
Top Bottom