Pre GE2025 Hayati Magufuli kuvunja Katiba haihalalishi uonevu wa 'kupapaswa' unaofanywa na Rais Samia. Hatufanyii hisani ni haki yetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Nawashangaa nyuki wa mama na utetezi wenu wa kipuuzi, oooh ameruhusu mikutano ya siasa, oooh amerusu vyombo vya habari kuongea vitakavyo, oooh wananchi wanajiachia watakavyo mtandaoni, oooh this ...oooh that, upuuzi mtupu!

Magufuli kuminya Katiba haimpi ruhusa Rais Samia kujifanyia atakavyo kwa jina la "Kuruhusu". Hatufanyii hisani, Rais Samia hayupo juu ya Katiba kwamba anaweza kujifanyia anavyotaka na kuvunja katiba atakavyo. Sisi ndio tumempa nafasi hiyo, anafanya kazi kwaajili yetu.

Akiboronga atapigwa spana, akifanya vizuri atapewa maua yake, lakini siyo anaambiwa ukweli mnakuja na visababu uchwara mbona hakusema hiki wakati wa Magufuli au mbona hamkufanya vile wakati wa Magufuli. Uozo na ukiukwaji wa haki wa Magufuli haufuti mapungufu ya mama (ambayo ni mengi), na akiboronga ataambiwa ili ajirekebishe, siyo kututupia vije mara umekuwa chura, mara usiguse uchumi wako. Uchumi wako kivipi wakati unatuwalikilisha sisi?

Wanaotokosoa wana lengo la kujenga, sio kuvimba na kureact na kujifanya wewe ni bora wakati hauna tofauti na mtangulizi wako, uchofanya ni 'kutupapasa' tu lakini ukiukwaji wa haki ni ule ule!

Nyuki wa mama povu liwe fupi fupi!
 
Hii nchi, raia wake ni kama haturuhusiwi kuwa na freedom of speech,, Kazi kweli kweli 🤒 😎
 
Chura kanyamaza!
Anaruka ruka kimya kimya. Hata tumtukane!
Hizo kura sijuwi wanaibaje kwa kweli?!
Anyway yetu macho na masikio....
 
Wakuu,

Nawashangaa nyuki wa mama na utetezi wenu wa kipuuzi, oooh ameruhusu mikutano ya siasa, oooh amerusu vyombo vya habari kuongea vitakavyo, oooh wananchi wanajiachia watakavyo mtandaoni, oooh this ...oooh that, upuuzi mtupu!

Magufuli kuminya Katiba haimpi ruhusa Rais Samia kujifanyia atakavyo kwa jina la "Kuruhusu". Hatufanyii hisani, Rais Samia hayupo juu ya Katiba kwamba anaweza kujifanyia anavyotaka na kuvunja katiba atakavyo. Sisi ndio tumempa nafasi hiyo, anafanya kazi kwaajili yetu.

Akiboronga atapigwa spana, akifanya vizuri atapewa maua yake, lakini siyo anaambiwa ukweli mnakuja na visababu uchwara mbona hakusema hiki wakati wa Magufuli au mbona hamkufanya vile wakati wa Magufuli. Uozo na ukiukwaji wa haki wa Magufuli haufuti mapungufu ya mama (ambayo ni mengi), na akiboronga ataambiwa ili ajirekebishe, siyo kututupia vije mara umekuwa chura, mara usiguse uchumi wako. Uchumi wako kivipi wakati unatuwalikilisha sisi?

Wanaotokosoa wana lengo la kujenga, sio kuvimba na kureact na kujifanya wewe ni bora wakati hauna tofauti na mtangulizi wako, uchofanya ni 'kutupapasa' tu lakini ukiukwaji wa haki ni ule ule!

Nyuki wa mama povu liwe fupi fupi!
Uko sahihi mkuu
Kama wanadhani samia ana mamlaka hiyo afanye ya mtangulizi wake tuone kama atadumu
 
Mimi sikuelewa alimaanisha nini kusema amekuwa chura. Yaani mwili wake wote ni chura kwa sasa au hawezi hawezi tena kufikiria maana kujifananisha na chura maana yake huna uwezo tena wa kuongoza.
 
Magufuli kuminya Katiba haimpi ruhusa Rais Samia kujifanyia atakavyo kwa jina la "Kuruhusu". Hatufanyii hisani, Rais Samia hayupo juu ya Katiba kwamba anaweza kujifanyia anavyotaka na kuvunja katiba atakavyo. Sisi ndio tumempa nafasi hiyo, anafanya kazi kwaajili yetu.
Kwanza kabisa. Ni Hayati Rais Magufuli. Heshima ni kitu ya bure

Hayati Rais John Pombe Magufuli, hatunaye. Kumwandika kana kwamba yupo hai ni kupuuzia kanuni za uandishi!

Acheni kukimbizana na wafu.
 
Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi muovu bila damu nyingi kumwagika.
 
Kitu ambacho una kipuuzia ni kuwa maisha yana ahadi mbili tu.

Kuzaliwa na Kufa.

Empirical reality.

Hayo mengine, wacha yakutese tu.

Yata kukuta na wewe.

Amani ikutawale
 
Back
Top Bottom