Kwani Samia anafanya nn Cha kufurugwa royally tour hkn kitu anafnya Ni ziara za kuwakumbuka ma babu zake tu hvyo Hakuna jipya jpm amefanya mamb mazito kuwai kutokea
Magu hatarii🥲🥲
1. JPM anajenga Reli ya Mwendo kasi – SGR.
2. JPM anajenga Bwawa la Umeme – Nyerere HydroPower.
3. JPM amenunua Ndege 13 aina tofautitofauti.
4. JPM amejenga Ikulu kule Dodoma na yale Magorofa ya Wizara kule Mji wa Serikali Dodoma ( Mtumba) Magufuli City
5. JPM amehamisha Makao Makuu ya Serikali na ameijenga Dodoma imekuwa Jiji
6. JPM amejenga FlyOver Dar es Salaam pale Ubungo na TAZARA
.
7. JPM amejenga daraja la Tanzanite pale Selander.
8. JPM ametengeneza huu Mfumo wa Kompyuta wa Malipo ya Serikali.
9. JPM alikuwa anaweka umeme hadi Vijijini (kwa Tsh. 27,000/= tu.)
10. JPM ameshawishi Bomba la Mafuta kutoka Uganda lipite Tanzania.
11. JPM anajenga daraja la Kingongo Ferry Busisi kule ziwa Victoria.
12. JPM amejenga Meli kubwa mbili mbili kila ziwa, yaani Ziwa Victoria 2, Ziwa Tanganyika 2 na Ziwa Nyasa 2.
13. JPM amejenga Hospital za Kanda kubwa nne… Dodoma, Mara, Mtwara, Geita na Songea
14. JPM amejenga Hospitali za Wilaya Zaidi ya 70
15. JPM amejenga Mradi Mkubwa wa Maji ya Victoria kule Tabora
16. JPM amejenga Mradi wa Maji Mkubwa Arusha
17. JPM amejenga Barabara ya Njia Nane Dar es Salaam hadi Kibaha
18. JPM alikuwa anajenga Mizani za Kisasa kabisa Kwenye Barabara zote kubwa
19. JPM amejenga Vituo vya Afya Zaidi ya 500
20. JPM amejenga na Kununua Rada 4 za AirPort
21. JPM amejenga Viwanja vya Ndege Mara, Iringa, Mbeya, Chato, Songea na Rukwa
22. JPM amejenga Masoko ya Madini kila Mikoa yenye migodi ya madini
23. JPM amejenga ukuta wa Mirerani na kuweka Camera za Ulinzi
24. JPM amejenga Bandari Kilwa, na kuzipanua Bandari Mtwara, Tanga na Dar es Salaam
25. JPM amejenga Masoko ya Kisasa zaidi, ya maana kama Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam
26. JPM amejenga Bus Stand za Kisasa Zaidi mikoani kama Dodoma, Mwanza, Dar es Salaam nk
27. JPM amenunua Vifaa Tiba kama MRI, CT Scan, Vifaa vya Kufanyia Oparations za Moyo pale JKCI Wagonjwa wanatoka nchi jirani kuja kutibiwa Tanzania
28. JPM amejenga Vivuko vya Majini sehemu mbalimbali kama Mafia, Kilwa, Ukerewe
29. JPM amejenga Barabara za Lami za adabu miji mingi sana, Barabara zina mifereji, Taa, na Taa za kuongozea magari.
30. JPM amejenga Shule za Msingi na Sekondari na kukarabati za zamani zikawa Bora kama Vyuo vikuu
31. JPM ametengeneza Vitanda kwenye mahospitali watu hawalali chini.
32. JPM ametengeneza Madawati karibia shule nyingi sana wanakaa kwenye Madawati.
33. JPM kajenga Hostel pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) uhaba wa vyumba umepungua.
34. JPM akasimamia mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu, na boom likawa linatoka kwa wakati (Migomo Vyuoni imeisha).
35. JPM aliamua kutusomeshea Watoto bila kulipa ADA ya Shule (Msingi na Sekondari)
36. JPM kafufua reli ya Kati na reli ya kwenda Moshi hadi Arusha.
37. JPM alikuwa anajenga kiwanda cha Sukari cha Magereza Morogoro.
38. JPM amejenga Kiwanda cha Viatu vya Jeshi – Lukaranga Moshi viatu haviagizwi tena nje ya nchi.
39. JPM anajenga Kiwanda cha Vifaa Tiba na Dawa huko Njombe.
40. JPM anajenga Barabara za Mwendo Kasi Mbagara hadi Gerezani Kariakoo
41. JPM amejenga FlyOvers pale Veta na Uhasibu Dar es Salaam.
42. JPM amejenga Vituo Vya Polisi, Nyumba za Askari Polisi na Magereza.
43. JPM amejenga yale Magorofa ya pale Magomeni na aliruhusu watu wakae bure kwa Miaka 5..
Hongera kwa jembe JPM.
Watu waache maneno ya ajabu, watu wafanye Yao tuyaone.
wasikae kutwa kumuongelea Hayati.. Rose Muhando aliimba Jifunze kwa waliofanikiwa..
📌📌