'Characters zako zifuatazo zitanifanya niendelee Kukukumbuka, Kukupenda na Kukuona ulikuwa Rais bora Tanzania kwa Kizazi cha sasa na hata Kijacho
1. Hukuwa Mnafiki na Mwizi
2. Uliiamini zaidi Akili yako Kubwa
3. Hukuwa Muoga wa Kufa / Kuuwawa
4. Ulikuwa ni Mzalendo wa Vitendo
5. Hukulea Upumbavu na Upuuzi
6. Hukupenda kuletewa Ripoti za wana Kitengo na Kuridhika nazo bali nawe pia ulikuwa na namna yako ya kuyajua mengi ya Ndani na Nje ya nchi pengine kuliko hata Wao.
7. Uliwapenda ( Ulitupenda ) zaidi Masikini ( akina GENTAMYCINE ) kuliko Matajiri Mafisadi walioko wengi sana Serikalini na hata katika Chama chako Tawala.
Magufuli binafsi nakukumbuka na nitakukumbuka na kama kuna 'Clip' yako ambayo Kila nikiisikiliza tu lazima Machozi yanitoke ni ile uliyosema ( uliyotuambia ) Watanzania wote kuwa Ukifa tutakukumbuka na kututaka tukukumbuke kwa Mazuri yako tu Kwetu Wananchi na nchi ya Tanzania.
Kama Kiongozi ulikuwa na Ubabe nilioupenda pamoja na Ukatili kwa Maadui wa Tanzania yetu ila kwa sasa Upole na Huruma ndiyo Umetawala Tanzania huku Mafia na Mafisadi wachache wakiyarudia yale yale ya 2005-2015 yaliyoiharibu Tanzania yetu Kimaadili na Kizazi cha wakati huo.
R.I.P Hayati Rais wangu Dk. Magufuli.
Subiri matusi kutoka kwa wenye mimba za chuki za Magufuli ambazo zimegoma kukomaa. Ila kadili siku zinavyo enda muda unaongea na utofauti unaonekana.
Unategemea nini unapowapa nafasi kubwa watoto wa vigogo ambao mpaka sasa washa dhihirisha hawana uwezo, ila kwa kuwa wazazi wao marafiki zake bado anawang'ang'ania na kuna watu Magu aliwatoa ila kwa sasa amewarudisha.Ila bora anavyo endelea kuwabeba kwani inadhihirisha Magu alikuwa sawa kuwatoa.
Kuna watu wanadai sasa hivi tuna uhuru wa kuongea Magu alikuwa anawabana kuongea, ila cha ajabu.
1.Bei ya mafuta imepanda tokea mwishoni kwa mwaka jana, wapo kimya.
2.Mgao wa maji kimya.
3.Mgao wa umeme kimya.Mgao ambao kila siku wanabadilisha nyimbo mara schedule maintenance, mara vituo chakavu sasa hivi wamejificha kwenye kichaka cha ukame.
4.Tozo kimya.
5.Tozo tuliambiwa zitasaidia mikopo ya wana vyuo,lkn juzi tu mliona huko mjengoni.
6.Kuna lile jiwe lililo nadiwa Dubai ambalo thamani yake ni zaidi ya bil 100,sijui wameishia wapi juzi kilo 53 za dhahabu zimekamata India kimya.
7.Wauza ngada na vijiwe vyao sasa hivi vinarudi kwa kasi.
8.Bei ya chakula imepanda sasa hivi wali maharage ni anasa, watu watakuambia ukame.2020 kulikuwa na ukame, eneo la EA lilikumbwa na nzige ,bahati nzuri huku hawakufika na mvua tulipata japo si nyingi na vilevile kulikuwa na issues ya Uviko dunia nzima bei ya vyakula ilapanda ila kwa Tanzania haikupanda.
Ila si washangai kukaa kwao kimya may be wapo na mabuyu yao ambayo Magu alibana wanalamba asali au may wapo Burundi.