Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 34,020
- 79,098
Hatimaye!
Baada ya sarakasi nyingi, Msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekata shauri la kumuoa mpenzi wake ambaye ni msanii ndani ya lebo yake ya muziki (WCB) Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’
Uamuzi huo umekuja huku kukiwa na sintofahamu nyingi juu ya mahusiano yao ambapo mwishoni mwa mwaka jana Zuchu alitangaza kwa mara nyingine kuachana kwao japo amekuwa akifanya hivyo mara nyingi na baadaye kurudiana.
Safari hii mambo yamekuwa tofauti kidogo baada ya majuzi kuibuka ugomvi ndani ya kampuni upande wa redio kwa Zuchu kuwashutumu wafanyakazi wa Diamond kumvunjia heshima.
Zuchu ameonekana ‘kukaza’, hajacheka na yeyote akiwemo Diamond mwenyewe na pengine hili limesogeza karibu ndoa yao.
Zuchu ameshinda vita iliyowashinda wengi?…
The mother in law from hell, Mama Diamond amekuwa mwiba mchungu takribani kwa kila mwanamke aliyetoka kimapenzi na Diamond.
Amesemekana kikwazo kikuu kwa Diamond kuoa, hivyo posa hii kwa Zuchu inatuacha njia panda kwamba Mama Dangote kapata kiboko yake? Je posa hii ina baraka za mama yake Diamond?
Ndoa ni kabla ya Ramadhani…
Mwezi uliopita Diamond akiwa na msanii mwenzie Nandy katika mkutano mkuu wa CCM, alionekana akisema atamuoa Zuchu kabla ya Ramadhani ya mwaka huu ambayo inategemewa kuanza mapema mwezi Machi.
Diamond amekuwa akitoa ahadi nyingi hivyo wengi hatukuchukulia tamko lile kwa uzito, nimeshtuka baada ya kupewa taarifa za uhakika kuwa ni kweli na posa hiyo itapelekwa nyumbani kwa Bi Khadija Kopa Ijumaa ya kesho kutwa tarehe 7.
Haya jamani, mambo ndio yako hivyo na hii ni habari endelevu nitakuwa hapa kuwajuza mapema kadiri nitakavyopokea taarifa.
Straight From The Horse’s Mouth,
Nifah.