Tetesi: Hayawi Hayawi, Diamond kumposa Zuchu Ijumaa!

Tetesi: Hayawi Hayawi, Diamond kumposa Zuchu Ijumaa!

Harusi ya taifa tunayo. Jamani mbona tutamkoma Bi Khadija?

Kubwa lao kataa ndoa limepatikana? Zuchu nimemvulia kofia.
Tujiandae kuimbiwa ngwinjii🤣🤣🤣🤣

Ila Da Zuu kanifunza kitu, kama boifrendi kamng'ang'ania hivo hadi kimeeleweka mie ni nani nisimng'ang'anie huyu baba hadi tuzeeke wote🤣🤣🤣

Zarina sijui yu hali gani?🤣🤣🤣🤣
 
wajumbe wa kataa ndoa, waki mshangaa mondi😃😂.

akati yeye ndo katibu wa chama hicho
FB_IMG_17387500707190018.jpg
 
Hapana Diamond ndio yuko kimaslahi zaidi. Atamuoa Zuchu kwa sababu ya pesa. Zuchu ni mgodi ambao Mondi anauchimba na kuutunza kwa pesa kidogo inayotoka kwenye pesa nyingi zinazotokana na mgodi huo.
Kwahiyo kumbe hadi wanaume mnaoa kwa maslahi? Si mmeshikilia bango la kataa ndoa kulinda mali zenu?
 
Atakuwa ameshampa mimba sasa anaogopa aibu ya kuizalishwa nje ya ndoa..

Mzazibar akizaa mtoto nje ya ndoa hata jina la baba hapewi..
Mtoto anapewa jina la mjomba...
Haya ni mapya, lakini sidhani kama iko hivyo na sipingani na hilo pia.
 
Mbona unachanganya sukari na shubiri?

Tumuombee mema huku itaisha kwa machozi tena?
Siku muziki wa Zuchu umeisha na akawa hamuingizii tena Dai pesa na hii ndoa itapumulia mashine.

Ila wazanzibari wanajua kuvumilia ndoa, anaweza kuendelea kung'ang'ana hivo hivo.
 
Hapa ndiyo unatimia ule usemi kwamba mwonja asali huchonga mzinga.

Kuna sehemu Wanaume huwa tunaingia na kujisemea pale naonja na kupita hivi

Kumbe ndiyo unanaswa mazima

Unakuta jamaa wanajiuliza huyu Mwamba ameona nini Kwa kile kibinti, kumbe mambo unayopewa Kwa bed, hadi unajilaumu kwanini hatukujuana mapema 🏃🏃🏃🏃
 
Back
Top Bottom