Tetesi: Hayawi Hayawi, Diamond kumposa Zuchu Ijumaa!

Tetesi: Hayawi Hayawi, Diamond kumposa Zuchu Ijumaa!

Hapa ndiyo unatimia ule usemi kwamba mwonja asali huchonga mzinga.

Kuna sehemu Wanaume huwa tunaingia na kujisemea pale naonja na kupita hivi

Kumbe ndiyo unanaswa mazima

Unakuta jamaa wanajiuliza huyu Mwamba ameona nini Kwa kile kibinti, kumbe mambo unayopewa Kwa bed, hadi unajilaumu kwanini hatukujuana mapema 🏃🏃🏃🏃
Sasa babu mengine nashindwa kukwambia ila nasikiaga Diamond kavua kofia kwa mtoto wa Bi Khadija, sio mchezo!
 
Hayo mambo ya kuonja onja hata yakitukuta sisi Wazee ndiyo mwanzo wa kumkabidhi Binti wa elfu 2 kadi na password ya Benki akajichotee Pension yote

Kuja kutahamaki unajikuta pension imeenda 🙌
mjomba ali muoa mkewe, ila mwanzoni ali ona mkewe ni mbwa mbea ila pisi.

aka sema nipige nisepe, Cha kushangaza ni aunt yangu Sasa hivi😃😂
 
View attachment 3225842

Hatimaye!
Baada ya sarakasi nyingi, Msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ amekata shauri la kumuoa mpenzi wake ambaye ni msanii ndani ya lebo yake ya muziki (WCB) Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’

Uamuzi huo umekuja huku kukiwa na sintofahamu nyingi juu ya mahusiano yao ambapo mwishoni mwa mwaka jana Zuchu alitangaza kwa mara nyingine kuachana kwao japo amekuwa akifanya hivyo mara nyingi na baadaye kurudiana.

Safari hii mambo yamekuwa tofauti kidogo baada ya majuzi kuibuka ugomvi ndani ya kampuni upande wa redio kwa Zuchu kuwashutumu wafanyakazi wa Diamond kumvunjia heshima.

Zuchu ameonekana ‘kukaza’, hajacheka na yeyote akiwemo Diamond mwenyewe na pengine hili limesogeza karibu ndoa yao.

Zuchu ameshinda vita iliyowashinda wengi?…
The mother in law from hell, Mama Diamond amekuwa mwiba mchungu takribani kwa kila mwanamke aliyetoka kimapenzi na Diamond.

Amesemekana kikwazo kikuu kwa Diamond kuoa, hivyo posa hii kwa Zuchu inatuacha njia panda kwamba Mama Dangote kapata kiboko yake? Je posa hii ina baraka za mama yake Diamond?

Ndoa ni kabla ya Ramadhani…
Mwezi uliopita Diamond akiwa na msanii mwenzie Nandy katika mkutano mkuu wa CCM, alionekana akisema atamuoa Zuchu kabla ya Ramadhani ya mwaka huu ambayo inategemewa kuanza mapema mwezi Machi.

Diamond amekuwa akitoa ahadi nyingi hivyo wengi hatukuchukulia tamko lile kwa uzito, nimeshtuka baada ya kupewa taarifa za uhakika kuwa ni kweli na posa hiyo itapelekwa nyumbani kwa Bi Khadija Kopa Ijumaa ya keshokutwa tarehe 7.

Haya jamani, mambo ndio yako hivyo na hii ni habari endelevu nitakuwa hapa kuwajuza mapema kadiri nitakavyopokea taarifa.

Straight From The Horse’s Mouth,

Nifah.
Hiyo ni NDOA YA UJI, Baada ya Ramadhan inavunjika, ni aibu sana kwa Wasanii kuoana ili kukidhi matakwa ya Ramadhan
 
Mkuu naamini Simba kakutana na wanawake wengi wazuri kuliko Zuchu hivyo inaniwia ugumu kuamini ya kuwa kuna mapenzi ya kweli kati yao.

Hatahivyo, sitaki kuonekana mchawi ila nawaombea mwisho mwema.
Hapa tumekubaliana.
 
Diamond anamuoa king’ang’anizi wake, huku Zuchu akiolewa na matatizo yake.

HUMJUI DIAMOND WEWE.

HUYO KIJANA AMETUMWA PESA KWELI KWELI..

APO ANATAKA ATINGISHE NCHI KWA KUTREND KILA SEHEMU ILI APIGE HELA SEHEMU

BIASHARA YA ENTERTAINMENT INATAKA UWE NA HEKA HEKA ZA KUTEKA INDUSTRY KILA BAADA YA MUDA FULANI
 
Back
Top Bottom