Tetesi: Hayawi Hayawi, Diamond kumposa Zuchu Ijumaa!

Tujiandae kuimbiwa ngwinjii🤣🤣🤣🤣

Ila Da Zuu kanifunza kitu, kama boifrendi kamng'ang'ania hivo hadi kimeeleweka mie ni nani nisimng'ang'anie huyu baba hadi tuzeeke wote🤣🤣🤣

Zarina sijui yu hali gani?🤣🤣🤣🤣
Mwenzangu hata mimi nimejifunza kwa Zuhura, siachani tena na mukaka wangu.

Zari lazima aje na drama mpya, huwa anajidai yuko cool kwa kudhani yataisha na Diamond hataoa atarudi kwake.

Ngoja tuone…
 
Hapa ndiyo unatimia ule usemi kwamba mwonja asali huchonga mzinga.

Kuna sehemu Wanaume huwa tunaingia na kujisemea pale naonja na kupita hivi

Kumbe ndiyo unanaswa mazima

Unakuta jamaa wanajiuliza huyu Mwamba ameona nini Kwa kile kibinti, kumbe mambo unayopewa Kwa bed, hadi unajilaumu kwanini hatukujuana mapema 🏃🏃🏃🏃
wajomba zangu wamesha nionya kujaribu jaribu.

maana pengine hapana comeback, zaidi ya kuomba extension of contract 😂😂
 
Waoane tu hakuna shida
View attachment 3225842

Hatimaye!
Baada ya sarakasi nyingi, Msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ amekata shauri la kumuoa mpenzi wake ambaye ni msanii ndani ya lebo yake ya muziki (WCB) Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’

Uamuzi huo umekuja huku kukiwa na sintofahamu nyingi juu ya mahusiano yao ambapo mwishoni mwa mwaka jana Zuchu alitangaza kwa mara nyingine kuachana kwao japo amekuwa akifanya hivyo mara nyingi na baadaye kurudiana.

Safari hii mambo yamekuwa tofauti kidogo baada ya majuzi kuibuka ugomvi ndani ya kampuni upande wa redio kwa Zuchu kuwashutumu wafanyakazi wa Diamond kumvunjia heshima.

Zuchu ameonekana ‘kukaza’, hajacheka na yeyote akiwemo Diamond mwenyewe na pengine hili limesogeza karibu ndoa yao.

Zuchu ameshinda vita iliyowashinda wengi?…
The mother in law from hell, Mama Diamond amekuwa mwiba mchungu takribani kwa kila mwanamke aliyetoka kimapenzi na Diamond.

Amesemekana kikwazo kikuu kwa Diamond kuoa, hivyo posa hii kwa Zuchu inatuacha njia panda kwamba Mama Dangote kapata kiboko yake? Je posa hii ina baraka za mama yake Diamond?

Ndoa ni kabla ya Ramadhani…
Mwezi uliopita Diamond akiwa na msanii mwenzie Nandy katika mkutano mkuu wa CCM, alionekana akisema atamuoa Zuchu kabla ya Ramadhani ya mwaka huu ambayo inategemewa kuanza mapema mwezi Machi.

Diamond amekuwa akitoa ahadi nyingi hivyo wengi hatukuchukulia tamko lile kwa uzito, nimeshtuka baada ya kupewa taarifa za uhakika kuwa ni kweli na posa hiyo itapelekwa nyumbani kwa Bi Khadija Kopa Ijumaa ya keshokutwa tarehe 7.

Haya jamani, mambo ndio yako hivyo na hii ni habari endelevu nitakuwa hapa kuwajuza mapema kadiri nitakavyopokea taarifa.

Straight From The Horse’s Mouth,

Nifah.
 
Kwa uzuri gani? Hivi unazijua pisi wewe?
Ila kwa kuwa we ni female huwezi jua mwanamke yupi mbovu na yupi mzuri.
Simba kaiacha pisi kama Zari unategemea awe na upendo na huyo Zuchu?
Kwamba wewe unaujua uzuri wa Zari na Zuchu kuliko Diamond aliyeishi nao wote kwa miaka mingi?

Kuwa serious basi Mkuu.
 
wajomba zangu wamesha nionya kujaribu jaribu.

maana pengine hapana comeback, zaidi ya kuomba extension of contract 😂😂
Hayo mambo ya kuonja onja hata yakitukuta sisi Wazee ndiyo mwanzo wa kumkabidhi Binti wa elfu 2 kadi na password ya Benki akajichotee Pension yote

Kuja kutahamaki unajikuta pension imeenda 🙌
 
Siku muziki wa Zuchu umeisha na akawa hamuingizii tena Dai pesa na hii ndoa itapumulia mashine.

Ila wazanzibari wanajua kuvumilia ndoa, anaweza kuendelea kung'ang'ana hivo hivo.
Wazanzibar nakubali. Kuna shoga yangu aliolewa mke wa pili tukalia balaa, akaondoka kabisa akarudi kwao.

Mbona alikuja kurudiana naye wanaishi uke wenza hadi leo? Na watoto anaongeza!
Nilikoma!
 
Kwamba wewe unaujua uzuri wa Zari na Zuchu kuliko Diamond aliyeishi nao wote kwa miaka mingi?

Kuwa serious basi Mkuu.
Mkuu naamini Simba kakutana na wanawake wengi wazuri kuliko Zuchu hivyo inaniwia ugumu kuamini ya kuwa kuna mapenzi ya kweli kati yao.

Hatahivyo, sitaki kuonekana mchawi ila nawaombea mwisho mwema.
 
View attachment 3225842

Hatimaye!
Baada ya sarakasi nyingi, Msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ amekata shauri la kumuoa mpenzi wake ambaye ni msanii ndani ya lebo yake ya muziki (WCB) Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’

Uamuzi huo umekuja huku kukiwa na sintofahamu nyingi juu ya mahusiano yao ambapo mwishoni mwa mwaka jana Zuchu alitangaza kwa mara nyingine kuachana kwao japo amekuwa akifanya hivyo mara nyingi na baadaye kurudiana.

Safari hii mambo yamekuwa tofauti kidogo baada ya majuzi kuibuka ugomvi ndani ya kampuni upande wa redio kwa Zuchu kuwashutumu wafanyakazi wa Diamond kumvunjia heshima.

Zuchu ameonekana ‘kukaza’, hajacheka na yeyote akiwemo Diamond mwenyewe na pengine hili limesogeza karibu ndoa yao.

Zuchu ameshinda vita iliyowashinda wengi?…
The mother in law from hell, Mama Diamond amekuwa mwiba mchungu takribani kwa kila mwanamke aliyetoka kimapenzi na Diamond.

Amesemekana kikwazo kikuu kwa Diamond kuoa, hivyo posa hii kwa Zuchu inatuacha njia panda kwamba Mama Dangote kapata kiboko yake? Je posa hii ina baraka za mama yake Diamond?

Ndoa ni kabla ya Ramadhani…
Mwezi uliopita Diamond akiwa na msanii mwenzie Nandy katika mkutano mkuu wa CCM, alionekana akisema atamuoa Zuchu kabla ya Ramadhani ya mwaka huu ambayo inategemewa kuanza mapema mwezi Machi.

Diamond amekuwa akitoa ahadi nyingi hivyo wengi hatukuchukulia tamko lile kwa uzito, nimeshtuka baada ya kupewa taarifa za uhakika kuwa ni kweli na posa hiyo itapelekwa nyumbani kwa Bi Khadija Kopa Ijumaa ya keshokutwa tarehe 7.

Haya jamani, mambo ndio yako hivyo na hii ni habari endelevu nitakuwa hapa kuwajuza mapema kadiri nitakavyopokea taarifa.

Straight From The Horse’s Mouth,

Nifah.
Kubwa la umbea kazini!! hahahha
 
Back
Top Bottom