Hayawi hayawi, Uwanja wa Bunju wa Simba FC, ujenzi wapamba moto

Hayawi hayawi, Uwanja wa Bunju wa Simba FC, ujenzi wapamba moto

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2016
Posts
2,282
Reaction score
1,252
Wakiokuwa wanabeza kuwa Simba Sports Club haitaweza kujenga uwanja wake nadhani sasa yamewashinda.Leo grader liliendelea kufanya kazi huko Bunju. Simba Sports Clubs imepania kuhakikisha uwanja huo unaanza mapema.

Ujio wa Mo in faraja kubwa kwa Klabu ya Simba.
13882697_283830418663410_1752157843617932561_n.jpg
Ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa Simba SC unaendelea katika eneo la Bunju jijini Dar es Salaam, Rais wa klabu hiyo Evance Aveva aliwaongoza baadhi ya viongozi na wanachama kufanya ukaguzi.

Mambo yanazidi kuonekana kwenda vizuri kwenye Uwanja wa Bunju unaomilikiwa na Simba, huku kukiwa na dalili za kikosi hicho kitaanza kufanya mazoezi kwenye uwanja wake mpya.

Uwanja huo wa klabu ya Simba, umeanza matengenezo na inaonekana yamekuwa yakienda kwa kasi kubwa.

Baada ya siku chache kuonekana tingatinga likikwangua, kuanzia juzi, mchanga maalum ambao huwa chini ya nyasi bandia umeanza kumwagwa.
13921126_543121659223617_4134310203998030597_n.jpg
13886302_543121762556940_6544490272414134028_n.jpg
13939527_1766878733577455_4803591174497926357_n.jpg
 
Yanga nayo ni wakati wa kujenga uwanja wao wa kisasa katika maeneo ya Mbezi-Morogoro road!
 
Hapa kuna dili linatafutwa, Baada ya siku 3 hilo greda halitakuwepo tena hapo uwanjani,
 
Yanga wao ni kuponda tuuu! Na kuonyesha kutokuwezekana kwa kila simba afanyalo.Kama ni rahisi mbona hata kifusi hamjaweka pale dimbwini.
 
HIV jamaani simba huo uwanja wao ni Ekali ngapi . Mimi ni shabiki wa simba napenda tu kujua ili kama hilo eneo linaweza kutosha kujenga uwanja Mkubwa wa kisasa na viwanja vingine vya academy na hostel za wachezaji
 
Back
Top Bottom