Hazina Haina Kitu: Wazabuni, Makandaradi, Madeni, ni taabu

Hazina Haina Kitu: Wazabuni, Makandaradi, Madeni, ni taabu

Wabongo muwe na kiasi,,

Sio kila kitu kujitia kujua, Kwa kawaida mwez July had August mifumo ya fedha serikalin inakuwa imefungwa Kwa ajili ya ukamilishaj wa maandaliz ya bajet mpya.

Utaona kuanzia September Mambo yanabadilika.

Ndio maana dola imekua adimu [emoji2369]
 
Sarafu yetu itazidi kushuka thamani hiyo mitambo na vifaa vyake wanavyotumia wakandarasi vinanunuliwa nje ya nchi kwa dola
Itakuwa ni suluhisho la mda mfupi, pia kwa mazingira hayo italazimu kuweka kizuizi kwa kuongeza kodi kwa baadhi ya vitu vinavyoweza kuzalishwa hapa ndani.
 
Bi mkubwa naona kama jua linazama asipokuwa makini sijui kama ataweza kuendelea na hii safari.Habari njema ni kwamba leo jamaa yangu mwenye duka kaniambia sukari mzigo mpya bei yake imepanda tena,soda takeaway za kampuni zote kaniambia mzigo mpya ni 1200(sielewi hizi ni bei elekezi au ni kila mtu sasa anafanya anavyotaka)

Anyway,kila la kheri kwake,tutafika tu.
Utabiri unaonyesha kamwe hatotoboa
 
Licha ya Serikali ya Tanzania kuwa na upungufu mkubwa wa Dolla ya kimarekani, haijatosha na bado serikali ya Tanzania Inaonekana kuwa na Uhaba mkubwa wa Fedha za ndani ambazo Ali maarufu wanaziita madafu yaani Tsh, Hali hii imepelekea maisha kuwa magumu mtaani Kwa minajili kwamba ajira nyingi za sekta binafsi zinategemea serikali, kwani nyingi zinapata flow ya pesa kutoka Kwa mwigulu nchemba na wizara yake kiujumla.

Hali ya Hazina ni mbaya sana, pesa hakuna, ila tujikumbushe kuwa serikali kamwe haiwezi kufeli, na hiki ni kipindi cha mpito.

Hata wote tunakumbuka serikali ya Ugiriki ilivyodondoka kiuchumi, na kuokolewa na serikali ya ujerumani Kwa kuingiza Fedha kiasi Cha Dolla bilioni 100, kama Mkopo Kwa Greece , ambapo mpaka Sasa Mkopo huo uliweza kulipwa kupitia staili ya mabeberu ya magharibi ya kutumia ukoloni mamboleo.

Hali hii pia tunashukuru tumeweza kuijua kwakuwa serikali iliyopo madarakani imeruhusu uhuru wa kuongea , kwani ingekuwa enzi zile habari hii ingekuwa ni Siri kubwa

Hoja mbovu kabisa kuna eneo gani limekwama kama mpaka nyongeza za mishahara zinatolewa madaraja ya utumishi yanapanda , huduma za bure zimeendelea , miradi inaendelea , Seminars zinaendelea na watu wanalipwa ! [emoji1241] labda sehemu gani tumekwama ?

Binafsi nampongeza Mh Mwigulu Nchemba kwa kusimamia Uchumi wa Nchi hii kwani kama Nchi na Dunia tumepitia katika nyakati ngumu sana tumeshuhudia mpaka mataifa ya jirani yakishindwa kulipa watumishi wake lakini hapa kwetu hakijatokea hicho !

Budget ya Nchi imepanda kwa mara ya kwanza Nchi yetu Inamchango wa Asilimia 70 kwenye budget yetu hayo yakiwa ni makusanyo ya ndani nina Imani mda sio mrefu tutamalizia hizo Asilimia 30 !

Sijui ulisimama wapi na hoja yako ama unautazama uchumi kwa namna gani ? Mwigulu Nchemba ndo Waziri wa kwanza wa Fedha kukusanya kiasi kikubwa cha mapato yetu ya ndani hakujawahi kutokea before !

Mwigulu Nchemba apewe maua yake tu jamaa ni anaweza sana taaluma yake ya Uchumi ndio kuendelea kwa uchumi wa Taifa letu .

Karibu kwa hoja
 
Back
Top Bottom