Hazina Haina Kitu: Wazabuni, Makandaradi, Madeni, ni taabu

Wabongo muwe na kiasi,,

Sio kila kitu kujitia kujua, Kwa kawaida mwez July had August mifumo ya fedha serikalin inakuwa imefungwa Kwa ajili ya ukamilishaj wa maandaliz ya bajet mpya.

Utaona kuanzia September Mambo yanabadilika.

Ndio maana dola imekua adimu [emoji2369]
 
Sarafu yetu itazidi kushuka thamani hiyo mitambo na vifaa vyake wanavyotumia wakandarasi vinanunuliwa nje ya nchi kwa dola
Itakuwa ni suluhisho la mda mfupi, pia kwa mazingira hayo italazimu kuweka kizuizi kwa kuongeza kodi kwa baadhi ya vitu vinavyoweza kuzalishwa hapa ndani.
 
Utabiri unaonyesha kamwe hatotoboa
 

Hoja mbovu kabisa kuna eneo gani limekwama kama mpaka nyongeza za mishahara zinatolewa madaraja ya utumishi yanapanda , huduma za bure zimeendelea , miradi inaendelea , Seminars zinaendelea na watu wanalipwa ! [emoji1241] labda sehemu gani tumekwama ?

Binafsi nampongeza Mh Mwigulu Nchemba kwa kusimamia Uchumi wa Nchi hii kwani kama Nchi na Dunia tumepitia katika nyakati ngumu sana tumeshuhudia mpaka mataifa ya jirani yakishindwa kulipa watumishi wake lakini hapa kwetu hakijatokea hicho !

Budget ya Nchi imepanda kwa mara ya kwanza Nchi yetu Inamchango wa Asilimia 70 kwenye budget yetu hayo yakiwa ni makusanyo ya ndani nina Imani mda sio mrefu tutamalizia hizo Asilimia 30 !

Sijui ulisimama wapi na hoja yako ama unautazama uchumi kwa namna gani ? Mwigulu Nchemba ndo Waziri wa kwanza wa Fedha kukusanya kiasi kikubwa cha mapato yetu ya ndani hakujawahi kutokea before !

Mwigulu Nchemba apewe maua yake tu jamaa ni anaweza sana taaluma yake ya Uchumi ndio kuendelea kwa uchumi wa Taifa letu .

Karibu kwa hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…