TANZIA Head Master wa Bwiru Boys, Elias Kaboja afariki dunia

TANZIA Head Master wa Bwiru Boys, Elias Kaboja afariki dunia

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Habari wanajukwaa,

Shule kongwe ya ufundi ya Bwiru boys imepoteza mwalimu wake mkuu, mwalimu Elias Kaboja.

Taarifa zinadai Mwalimu Kaboja alienda kumsalimu mwalimu wake hospitali ya Bugando na alipotoka naye akaugua na alipopelekwa hospitali hakuweza kurejea tena nyumbani.

photo_2021-02-01_09-18-06.jpg
 
Hivi jamani kwanini tunashindwa hata kuvaa mask na kunawa mtu unaenda Hosp haijalishi anaumwa nini.

Sasa kama walimu sasa sijui usalama wa wanafunzi na labda wanafunzi kwa kuwa wana nguvu ya kupambana na huu ugonjwa ila je wakiwapelekea wazazi wao au bibi na babu majumbani.

Hatari sana.
 
Tatizo kuna sisi tunategemea sana matamko ya wanasiasa badala ya uwezo wetu wa kufikiri.

Naamini leo hii ikitamkwa kampeni ya kunawa mikono na kuvaa mask mambo yatakuwa poa katika kupunguza maambukizi kama kweli dude liko mjini.
 
Hivi kwanini tuendelee kupuuzwa kama watoto wadogo?

Katoliki wamesema, Anglican wamesema. Wengine mko wapi?

Aambiwe mzee baba "we can't breathe."

Tupaze sauti. Atambue si kila mtu anaamini kwenye ushirikina zikiwamo nyungu.
 
Primary ndio kuna Mwalimu Mkuu ila Secondary ni Mkuu wa Shule.
Siku hizi wote wanaitwa wakuu wa shule kwa kigezo cha wote wanakuwa na kiwango kinachofanana cha elimu. Zamani mwalm mkuu alikuwa ana ngazi ya cheti na mkuu wa shule alikuwa na stashahada au shahada, lakini sasa hivi shule zote zina wakuu wa shule kwa kuwa elimu ni stashahda au shahada ndoo maana wqmebadilisha.
 
Back
Top Bottom