TANZIA Head Master wa Bwiru Boys, Elias Kaboja afariki dunia

TANZIA Head Master wa Bwiru Boys, Elias Kaboja afariki dunia

Apumzike kwa amani mwalimu huyu. Hakika maisha haya yalikuwa ya kuokolewa kwa kuchukua hatua fulani tu. Ambazo ziko mikononi mwa wenye mamlaka.

Hawakufanya hivyo na sasa wanamsingizia Mungu.

Hatajibu nini kwa Mungu hawa?
 
Huenda ni kale kaugonjwa ka kiitaliano "Deportivo De Coronya"
 
Kwanini dude alipiga chato kwa huyo anayesema hakuna korona ile naye adabu imshike?
 
Mungu amlaze mahali pema peponi.
Nilisoma hapo Bwiru around 2004 - 2007
 
ina maana dude la sasa hivi ni kali kiasi kile - yaani dk 30 tu alizo kaa na mgonjwa pale hosp tayari likawa llimeshaanza kujaza mapafu maji - RIP ticha !!

Tutaonana huko ndiko kwenye makazi yetu ya milele - tangulia chief
 
Kimya kimya tu wanaondoka inabaki tahadhari ya mtu mmoja mmoja
 
RIP sir,
Tahadhari ni muhimu, Afya sio mali ya serikali.
 
Siku hizi wote wanaitwa wakuu wa shule kwa kigezo cha wote wanakuwa na kiwango kinachofanana cha elimu.Zamani mwalm mkuu alikuwa ana ngazi ya cheti na mkuu wa shule alikuwa na stashahada au shahada ,lakini sasa hivi shule zote zina wakuu wa shule kwa kuwa elimu ni stashahda au shahada ndoo maana wqmebadilisha.

Nimejibu kama mdau alivyotaka kujua.......Swala la kuwa sawa kwasababu ya elimu ni mada nyingine mkuu.
 
Akili za kuambiwa na wanasiasa...changanya na za kwako! Usisubiri uambiwe ukwepe mikusanyiko....wewe ikwepe!
Siyo jinai kuvaa mask.....vaa.
Siyo kosa kutumia sanitizer....tumia.
Kama kwenda kanisani au msikitini kutakuletea maambukizi, acha. Hata Mungu anafahamu hilo.
 
Habari wanajukwaa,

Shule kongwe ya ufundi ya Bwiru boys imepoteza mwalimu wake mkuu, mwalimu Elias Kaboja.

Taarifa zinadai Mwalimu Kaboja alienda kumsalimu mwalimu wake hospitali ya Bugando na alipotoka naye akaugua na alipopelekwa hospitali hakuweza kurudi tena nyumbani.

Daaah upumuaji unaua balaa
 
Kundi linaloathitika zaidi na corona ni kuanzia miaka 50 kwenda mbele, chini ya miaka hiyo hawaathirki zaidi kwa maana kufariki ila wanakua ni wasambazaji tu wa hivyo virusi kwa hiyo kuna ulazima wa sisi sote kuchukua tahadhari zaidi iki kulilinda kundi hili ambalo wengi ni wazazi wetu.

Haya ni maoni yangu binafsi hayahusiani na hiki kifo ila tukumbuke kauli ya mbayuwayu
 
Habari wanajukwaa,

Shule kongwe ya ufundi ya Bwiru boys imepoteza mwalimu wake mkuu, mwalimu Elias Kaboja.

Taarifa zinadai Mwalimu Kaboja alienda kumsalimu mwalimu wake hospitali ya Bugando na alipotoka naye akaugua na alipopelekwa hospitali hakuweza kurudi tena nyumbani.

Too sad. Namfahamu. Nilisoma naye Nsumba Sekondari. Alikuwa mbele yangu mwaka mmoja
 
Back
Top Bottom