TANZIA Head Master wa Bwiru Boys, Elias Kaboja afariki dunia

Mwalimu mkuu na mkuu wa shule kuna tofauti yoyote?
Mwalimu mkuu ni mkuu wa taaluma wa shule, hahusiki na uendeshaji wa shule. Mara nyingi hutumika kwa shule za msingi. Mkuu wa shule ni msimamizi wa shughuli zote za shule na hutumika kwa shule za sekondari.
 
Umenena vizuri sana. Watu wanashabikia lockdown, hawajui kuwa jambo hili ni la kibinafsi zaidi. Oooh serikali, serikali, Serikali ije ikusafishie choo chako?
 
R.I.P mwalimu, mwezi jana tu tumeonana du ama kweli kazi ya Allah haina makosa, pumzika kwa man.
 
Haya yote ni matokeo ya bichwa kubwa kucheza sengeli badala ya kwaito!
 
Dah..Mungu awajalie wepesi walioguswa na msiba huu. Na amjalie Marehemu pumziko la amani
 
Kwani huko wanapocheza kwaito hawafi mkuu? Cheki Rwanda pamoja na maangalizo yote wamepigwa marufuku uingereza kisa corona
Umesoma jinsi huyo mwalimu alivyofariki? Alienda kumtembelea mwenzake hospitali then aliporudi nae akaanza kuumwa na kufa.

Maana yake kama tungekuwa tunacheza kwaito ya WHO huyu mwalimu asingeruhusiwa kuingia hospitali bila ya tahadhari zote na pengine hata asingeruhusiwa kuingia kwenye wodi ya wagonjwa wa Corona na leo angekuwa hai.

Lakini kwa sababu tumechagua kucheza sengeli huyu mwalimu aliingia wodi ya wagonjwa wa corona kwa madai kuwa mgonjwa anaumwa pnemonia kwa hiyo hana haja ya kuchukua tahadhari yoyote na matokeo yake ndiyo hayo!
 
R.I.P mwalimu. Tuchukue tahadhari.
 
kila mtu ashinde mechi zake.
 
Mkuu Bugando bila barakoa hauingii na maji getini yapo. Halafu tunapenda sana kulalamika enzi zile serikali ilifata kila hatua bado malalamiko yakawepo, waliruhusu hadi barakoa za vitenge watu mkatukana ila leo kule wanaposifia who pana barakoa za kushona nyingi.

Hatuwezi kuhukumu kuwa mgonjwa wa mwalimu mkuu alikua na korona. Kujikinga muhimu ila lockdown hapana. Wakitangaza sahiv kuna corona watu mtaanza kulilia lockdown. Tutakula wapi.

Wameleta nyungu season 3 mnadhihaki
 
Wapi wamesema kaingia kwenye wodi ya wagonjwa wa corona?. Hivi huwa mnalipwa shilingi ngapi kuupigia debe ugonjwa wa corona?

Watu wanakufa sana kila siku kwasababu mbalimbali toka zamani. Sema tu usambaaji wa taarifa kwa siku za hivi karibuni umekuwa rahisi kutokana na teknolojia ya mawasiliano.

Mna ukuza sana huu ugonjwa.
 

Tunajisahau sana wana nzengo
 
Lala salama mwalimu Elias Kaboja
Pole kwa familia na wote walioguswa na msiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…