Nadhani umefika wakati serikali itamke bayana kuwa katiba ya nchi inasemaje kuhusu dini. Katiba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inasmea kuwa serikali hiyo haina dini. Ina maana kwamba shughuli zote zinazohusu serikali hazifuati misingi ya dini yoyote ile. Hivyo basi itikadi, imani na viashiria vingine vya kidini kama mavazi, alama n.k visihusishwe kwenye shughuli zake. Kwa mantiki hiyo basi, ina maana kwamba katika shule zote ambazo ni za serikali, katiba ya Jamhuri ifuatwe. Kama wanafunzai wanavaa sare, ziwe ni sare ambazo hazihusishi dini. Kama kutakuwepo na jamii fulani ambayo inakerwa na jambo hilo, wako huru kabisa kuanzisha shule zao ambazo itikadi za jamii hiyo zitazingatiwa, ili mradi hawavunji sheria.