Poleni sana, ingawa hatutakiwi kujuana hapa JF ni vyema wakati mwingine kama mtu akipatwa na madhira kama haya, ajitokeze na baada ya haya majanga abadili identity. Binafsi ningependa nije huko Bongo nimjulie hali maana anachangamsha JF na ni haki yake kujuliwa hali. Nadhani nitapata nauli kutoka kwa mama sukari wangu miss chaggaNdugu Jamaa na Marafiki.
Nasikitika kutoa taarifa juu ya madhira aliyokutana nayo dada na ndugu yetu HEAVEN ON EARTH jana usiku.
Akiwa anaelekea nyumbani kwake jana usiku alivamiwa na vibaka/majambazi na kumjeruhi vibaya sana.
Toka alipopatwa na madhira hayo mpaka mchana huu bado hawajeza kuongea, naomba tushirikiane kumuombea ili matibabu anayopata yaweze kumrejeshea nguvu na afya yake.
Nitakapopata taarifa za ziada nitawajuza.