Hebu soma dialogue hizi za wanandoa vijana wa hapa uswazi kwetu.

Hebu soma dialogue hizi za wanandoa vijana wa hapa uswazi kwetu.

Nakapanya

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
2,096
Reaction score
709
Hawa ni wanandoa wawili vijana wanaoishi pamoja though hawana mtoto,bwana ni konda kwenye magari makubwa na bibi ni mama wa nyumbani tuu.Sasa soma kidogo moja ya maongezi yao asubuhi moja;
Bibi: naomba hela ya matumizi ya leo,kila kitu kimeisha ndani.
Bwana:mimi sina hela
Bibi:sasa kama huna hela unadhani mimi nitakula nini leo na wewe ukienda kazini unakula hukohuko?
Bwana:nishakwambia sina hela,kama unaona mimi huwa nakula kazini twende na wewe ukale huko kazini.
Bibi:lakini jana umekuja umelewa,sasa kama huna hela hiyo ya kunywea umepata wapi?
Bwana:we mwanamke acha kunisumbua,nitakuchenjia sasa hivi ohooo
Bibi:mi bora unichenjie lakini lazima uniachie hela ya matumizi.
Bwana:we mshenzi kweli,unajua hela inavyotafutwa,SI UENDE UKATO*** HIYO K***A YAKO ILI UPATE HELA YA KULA.
Bibi:anakuwa mpole huku machozi yanamtoka.
Baada ya mume kuondoka kwenda kazini,bibi huku nyuma kweli na yeye akajiremba safari huyo kutafuta pesa kwa njia aliyoambiwa na mumewe.
MY TAKE:
Hivi ndivyo maisha ya ndoa yalivyo jamani?kama watu hamko tayari kuoa kwann uharakie?na kama umemchoka mwenzakao si umuambie ukweli tuu kuliko vituko na dharau zote hizi kwa mwenzio.
 
Hata kama hupendi, ila huo ndio ukweli halisi. Huyo jamaa alizoea kuishi bora liende, baada ya kuingia kwenye ndoa kila kitu anahojiwa kama hela ya matumizi au muda wa kurudi n.k
 
Nadhani kuna vitu viwili. Ndoa na Kuishi pamoja.

Hao wanaishi pamoja sio wanandoa.
 
Wewe ni muongo, hakuna konda wa malori mwenye tabia hizo........................
halafu mbona mnapenda sana kutusengenya sisi watu wa uswazi............. Nitapiga mtu hapa siku moja..! ooohooo nyie endeleeni tu.....................LOL
 
"Kama unataka kupoteza sehemu ya uhuru wako ingia kwenye ndoa"
AMANI IWE NASI...

kuwa katika ndoa si kupoteza uhuru,makubaliano na uelewano baina ya wanandoa ndio msingi mkubwa wa jinsi mtakavyoyaendesha maisha yenu.
 
Jambo hili liko mahakamani lisijadiliwe hapa mpka pilato werema atoe hukumu
 
Hata kama hupendi, ila huo ndio ukweli halisi. Huyo jamaa alizoea kuishi bora liende, baada ya kuingia kwenye ndoa kila kitu anahojiwa kama hela ya matumizi au muda wa kurudi n.k

lakini angekuwa mstaarabu na si kumtupia maneno ya kejeli kiasi hicho.
 
Wewe ni muongo, hakuna konda wa malori mwenye tabia hizo........................
halafu mbona mnapenda sana kutusengenya sisi watu wa uswazi............. Nitapiga mtu hapa siku moja..! ooohooo nyie endeleeni tu.....................LOL

uongo kwangu mwiko,jamaa ni kondakta/utingo kama nilivyokuambia na hizo ndio tabia zake na uswazi ndio tunapoishi nae.
 
Huyu jamaa ana mambo ya ajabu sana,ni takribani miezi mitatu toka ampige/wapigane na mkewe hadi kufikia hatua ya kugawana mali na kuachana kabisa,baada ya siku tatu tukaona wamerudiana tena,kifupi jamaa bado ana utoto mwingi.
 
uongo kwangu mwiko,jamaa ni kondakta/utingo kama nilivyokuambia na hizo ndio tabia zake na uswazi ndio tunapoishi nae.
Heading yako imewajumuisha wanaume wote wa uswazi, mimi nakaa uswazi Mwananyamala kwa Ali Manjunju, mbona sina tabia hizo, na hata wanandoa vijana wanaonizunguka wengi hawana tabia hizo...
Tatizo lenu kila jambo baya basi ni la uswazi, mnakosea bana...............
 
Wewe ni muongo, hakuna konda wa malori mwenye tabia hizo........................
halafu mbona mnapenda sana kutusengenya sisi watu wa uswazi............. Nitapiga mtu hapa siku moja..! ooohooo nyie endeleeni tu.....................LOL

Bora umenisaidia,we ngoja waendelee!
 
Unatusema vibaya sana sie Waswazi.....tatizo mnatuonea gere: Disco la bure, story mpya za kumwaga, ngumi bwerere, chumvi na mboga tunaazimana n.k n.k ..........ongezea
 
Heading yako imewajumuisha wanaume wote wa uswazi, mimi nakaa uswazi Mwananyamala kwa Ali Manjunju, mbona sina tabia hizo, na hata wanandoa vijana wanaonizunguka wengi hawana tabia hizo...
Tatizo lenu kila jambo baya basi ni la uswazi, mnakosea bana...............

Mkuu Mtambuzi,tukubaliane tu kuwa uswazi ustaarabu ni mdogo.Tena hakuna uchaguzi wa maneno mtu anapozungumza!Tena ukikutana na mtoto wa uswazi ndiyo utajua uswazi maana yake nini.
 
Gwangambo, hayo si maneno yangu, bali maneno ya wakwongwe kwenye ndoa. Huwa nawasilikiza ili kupata picha ya ndoa. Ila nayatumia ili kutoa tahadhari kwa junior bchelors kama mimi.
 
Mkuu Mtambuzi,tukubaliane tu kuwa uswazi ustaarabu ni mdogo.Tena hakuna uchaguzi wa maneno mtu anapozungumza!Tena ukikutana na mtoto wa uswazi ndiyo utajua uswazi maana yake nini.
Kwani ni nini maana ya demokrasia...?
 
Back
Top Bottom