Hebu tuanzie hapa: Ben Saanane alitoka kwao saa mbili asubuhi ila hakurudi mpaka leo. Yupo hai? Kuna huu ujumbe aliotuambia

Hebu tuanzie hapa: Ben Saanane alitoka kwao saa mbili asubuhi ila hakurudi mpaka leo. Yupo hai? Kuna huu ujumbe aliotuambia

Mkuu sijui wewe ni wa nchi ipi lakini kwa mujibu wa katiba yetu uhai wa raia wote unadhamani sawa. Hakuna mwenye uhai wa thamani kuliko mwingine. Kuhusuu wachunguzi kutoka nnje serekali hakuambiwa igharamie walichoombwa ni kutoa kibali. Mheshimiwa kuhusu Lisu si anatibiwa kwa gharama isiyohusisha serekali. Pamoja na serekali kupewa ripoti lakini walio waita wangepewa yao pia.
Wewe naona huelewi kabisa!! Unanisimulia theory za katiba. Katiba inasema hivyo nawe unavyoona unapewa haki sawa na ya Tundu Lissu? Unataka Lissu apewe haki sawa na waziri mkuu? Serikali gani duniani inatoa haki kwa mtindo huo? Hukona Kikwete, tezi dume linampeleka US wakati wewe unaambiwa hospitali ya rufaa inakutosha?

Using'ang'anie katiba inasema hivi na vile, angalia uhalisia ukoje kote duniani.
 
Huyo aliyenyoosha ni mtu wa usalama na alikua anamuamuru aingie ndani ya gari.Je kuna sheria inakataza afsa usalama kumnyooshea siraha mkaidi wa amri halali?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama afisa usalama anaonyesha kitambulisho kama kweli anachofanya ni halalii... Sasa kitambulisho hataki kuonesha anatoa tu bastola Je kama ndo wale watu wa msumbiji waliomteka MO..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Tanzania bhana vituko haviishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe naona huelewi kabisa!! Unanisimulia theory za katiba. Katiba inasema hivyo nawe unavyoona unapewa haki sawa na ya Tundu Lissu? Unataka Lissu apewe haki sawa na waziri mkuu? Serikali gani duniani inatoa haki kwa mtindo huo? Hukona Kikwete, tezi dume linampeleka US wakati wewe unaambiwa hospitali ya rufaa inakutosha?

Using'ang'anie katiba inasema hivi na vile, angalia uhalisia ukoje kote duniani.

Mkuu wewe unamawazo ya kibaguzi ya hali ya juu. Haki zangu za kikatiba hazipaswi kuwa tofauti na za Lisu. Tiba za nnje mbona raia kadhaa wanapelekwa nnje kwa tiba. Kuna wanapelekwa India Kenya hata SA. Hii mkuu inanipa picha kuwa ndani ya CCM kuna watu mnatamani mpewe upendeleo kwa ajili ya nafasi mlizonazo ndani ya serekali yenu ama ndani ya chama. CCM mnalea ubaguzi. Na sasa hivi mbaya zaidi mnapanda mbegu za ubaguzi wa kichama, kubagua wanachama wa vyama pinzani.
 
Nilikua mmoja wa watu walio pendezwa (like) post au jumbe za Ben Rabiu wa saanane huko Facebook. Hakika kijana alitiririka kwenye ukosoaji hasa ule uliohusu elimu ya juu ya bwana mkubwa.
Japokua nili like zile post, moyoni nilisikita juu ya kile kitachompata ben, na kweli baada ya mda si mrefu yalitokea yale ambayo wengi tuliyahisi.

Naionea huruma sana familia ya mzee saanane, najua uchungu walionao hakuna mwenye uchungu kama walionao wao. Ben alishangiliwa na weng Facebook lakini huko aliko analia peke yake. Chama alichokipigania kipo na ruzuku mwenyekiti anasaini.

Makamanda mtandaoni still wapo, wanasogeza maisha kimtindo kupitia chama. Ben alitumika tu.....
Kuna dogo mwingine anakuja kwa kasi sana anajiita Mdude.... kila nikiona picha yake mitandaoni natamani nimuambie kitu, siasa za bongo ni ngumu sana



Sent using Jamii Forums mobile app
ahahaha mdude chadema huwa ananifrahishaga sanaa
sema ana majibu na vituko sanaa.
hivi bado hajajulikana ni nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi unapata wapi ujasiri wa kuchangia ujinga katika mambo magumu kama haya?
mkuu huyu kila siku namwambia hapa. naliiba mitihani na hao wanaomtuma wana akili kama zake tu. hawa na kina sijui magonjwa ya akili mtambuka ni wakupuuzwa tu. hana hata uwezo wa kufikir nje ya ccm na chadema
 
Ben Saanane alitumwa na Mbowe Afrika Kusini, kumbe ilikuwa janja ya kumuuwa ili kuficha wizi wa ruzuku ya chama.

Ni kama Chacha Wangwe tu alichofanyiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi chacha wangwe alifanuyiwa nini? Nijuavyo Mimi ni kwamba alifariki kwa ajali kule gairo akitokea Dodoma kwenda Dar.ina maana tulipigwa changa la macho?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto alishaeleza waliomteka Ben na Kumuua ni kina nani,walifatilia kote kuanzia vodacom lakini ushirikiano ulikuwa sifuri mwisho wa siku polisi wazalendo wakamwambia "aisee tumefatilia sie tumeishia hapa na waliomchukua ben ni wazee wa kitengo".

Ukiona tukio kubwa limetokea na hakuna aliyekamatwa na wenye mamlaka wanatoa majibu ya "FUTUHI" wewe endelea kufanya shughuli zako
 
Kuandika siyo tatizo ila huenda mkono wako uliokusaidia kuandika haya ukawa na kilema kama syo mkono basi kutakuwa na tatizo kwenye kokonatia!!

Kwakuwa tunapenda vitu vya uongo uongo ,,umbea, uhayawani, na masuala ya kumkandamiza mwanadam mwenzako kwa mambo ambayo nafaham nafsi inakusuta ila kwa sabab tu ya Visa vya wanadam unaweza kuongea yote Haya!!

Sina Hakika kisheria kama hata ww unaweza ama mie ninaweza kuhoji ama kutaka uhalali Wa elimu yangu!! Taasisi husika nadhani ndo zina authority hiyo nikiamni kwamba they are legalised and recognized institutions!!

You /I sina hakika kbsa kwamba you /I can question my or ur education and expecting to get a genuine answer may be according to the context of inquiry!!

Mengine haya ni kukosa tu kufikiri na kuendeleza hla tu!!!

Haya hayajaanza leo hata mataifa makubwa na yenye uwezo mkubwa kijeshi na kiusalama haya yanatokea na tusivyo na akili tunaenda ati kushtaki utafiki ni Baba zetu!!! Au kuongoza taifa la watu zaidi ya mil 50 tunalinganisha na familia zetu ambazo zinawatoto watatu lakn hata kuzi control zatushinda sembuse mamilion haya ya watu!!!!!

Mtalalamika lkn wenzenu wanatenda!!! Mtashtuka kumekucha mnaendelea kulia lia ila muda huo wenzenu watakuwa wame win!!

Heri ya mwaka mpya!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungekuwa na hekima usingeandika huu upumbavu wako, wewe ni mpumbavu wa wapumbavu, unayedhani ilivyo leo ndo itakavyokuwa kesho.
 
Juzi niliona picha ya Rais Magufuli akimuombea mama yake mzazi ambaye amepatwa na maswahibu kama yaliyokatisha uhai wa binti yake ambaye alizikwa hivi karibuni.Nilipomuona nilijikuta nikiwaza sana!

Turudi kwenye mada. Ben Saanane mara ya mwisho kabla hajapotea alitoka kwao asubuhi kama kawaida kwenda kwenye mihangaiko ila hakurudi tena hadi leo. Siku chache baada ya kupotea namba yake ikaondolewa kwenye makundi yote ya WhatsApp naamini alikuwa akishurutishwa fanya hili...fanya hili...Siku baada ya siku hadi alipomaliza yote. Mbaya zaidi kuna ujumbe aliotuachia "Tuutafakari" ambapo alikuwa akilalamika kuwa yupo mtu mmoja alikuwa akimtumia ujumbe kila alipokuwa akiishambulia elimu ya mfalme kule kisiwani kwenye mitandao ya kijamii kuwa "mara umebakiza post tatu mara mbili" na mwisho kabisa akamwambia "Naamini sasa hutapost tena" Ujumbe zaidi aliambiwa "Baba yako atajilaumu sana kwa kukusomesha na sasa hatayafaidi matunda ya elimu yako,Ben wewe bado ni kijana mdogo sana kufa"

Ninachoamini ni kuwa dola inajua kabisa yaliyomkuta Ben. Kama sivyo basi wangeshachukua hatua stahiki. Emb fikiria watu wote waliokuwa wamekithiri kwa ukosoaji kipindi kile walifanywa nini? Tundu Lissu mbunge na mwanasiasa maarufu sana alishambuliwa kwa risasi nyingi mchana kweupe tena mbele ya makazi yenye ulinzi mkali na hakuna chochote mpaka leo. Njoo kwa kuke kwa ofisi za Fatuma Karume hadi bomu likarushwa kwenye ofisi zao. Kina Roma walivyopigwa kwenye majumba yasiyojulikana! Itakuwaje kwa Ben aliyekuwa naye amekithiri kwa ukosoaji?

Mimi naweza kufikiria haya na huenda moja wapo likawa sahihi
1. Huenda Ben kapigwa ban labda kwa kipindi fulani....Ila hapana, siku wakimtoa huko je? Si wataaibika?
2. Huenda walidhamiria kumpiga kisha wamuachie ila wakazidisha kipigo na ikawa bahati mbaya jumla!
3. Au moja kwa moja walimmaliza.
4. Au labda walimpa ofa ya kwenda nchi za watu kukaa tu huko ili asiwe tena anashambulia....Thubutuuu yani mfalme umkosoe, uwe mfuasi wa "mabeberu" halafu akupeleke kula bata?

Wazo namba 2 linanishawishi nikubaliane nalo zaidi kwakuwa naamini hata kina Roma Mkatoliki na wenzake walipokuwa wanapigwa kama ingetokea bahati mbaya iwe jumla basi nao wasingeonekana mpaka leo.Linanishawishi nikubaliane nalo kwakuwa wote waliokosoa walielekezwa kwenye mfumo huu wa kupotezwa ila baadhi yao Mola akawanusuru!

Kuna kile kipindi maiti zilikuwa zinaokotwa kiholela sana kule baharini mara mto Ruvu huku zikiwa zimefungwa kwenye viroba. Hiki ndicho kipindi kile cha kukamatwa watu kule MKIRU na kwenda kuona joto la motoni kule Stakishari! hiki ndicho kipindi kilichokuwa muda mfupi tu tangia Ben atoweke. Ndicho kipindi alichopotea Azory.........Mbona siku hizi zile maiti za "wahamiaji haramu" hazipo tena? Kwanini kipindi kile ziliibuka sana zikiwa zimefungwa kwenye mifuko huku sisi wengine tukielewa kuwa kule Stakishari kulikuwa na kwata la kufa mtu likiendelea? Hadi watu wakawa wanatambaa kama nyoka? Kwanini kwanini kwanini?

Ukweli wa haya naamini kuwa hautajulikana kama tutaujenga "mfumo mfalme wa kisiwa" kama tulivyotahadharishwa humu Jf......"Mfumo mfalme huyu" ni hatari kwa afya yetu hivyo tuchukue tahadhari mapema sana.
kila ninapoisoma post hii naichukia ccm na serikali yake
 
Back
Top Bottom