Hebu tuijadili hii tabia ya kunyolewa ndevu na mwanaume mwenzio!

WhoWeBe

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
2,299
Reaction score
4,282
Nimezaliwa kijijini ambako maadili ya 'kiuanaume' yanalindwa sana. Moja kati ya meeengi ya kiuanaume ni kwamba ndevu unanyolewa na mkeo tu au mpenzi wako. Kwa maneno mengine ni kwamba unyoaji wa ndevu ni kazi ya wanawake.

Sasa siku hizi imekuwa kawaida kumkuta dume ananyolewa ndevu na mwanaume mwenzie. Tena mwingine asivyo na adabu unamkuta amefumba macho kabisa (kama vile kuvuta hisia za raha ya kuchezewa na kugeuzwa geuzwa kwa kidevu chake) wakati ananyolewa.....huu udhalilishaji.

Msimamo wangu ni kwamba kamwe siruhusu ndevu zangu kunyolewa na mwanaume mwenzangu.

Ahsanteni..
 
Ungeendelea tu kukaaa kijijini kwenu hamna shida,umekuja miji ya watu usipangie taratibu za kuishi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…