- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu naomba kupata ukweli, hii kauli imetolewa na Heche?
- Tunachokijua
- Novemba 18, 2025 Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka alitoa taarifa kwa umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, aliunda Tume ya kufanya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.
Aidha kupitia makamu mwenyekiti wake John Heche, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ilitoa msimamo wake kuhusu tume iliyoandaliwa kuchunguza “matukio ya uvunjifu wa amani” baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.
Madai
Kumekuwepo na grafiki yenye utambulisho wa Jambo TV inayosambazwa mtandaoni kuwa John Heche amesema 'yale hayakuwa maandamano bali uharibifu uliojificha kwenye maandamano'
Je, uhalisia ni upi?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia marejeo ya video imebainika kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani Kauli hiyo haikutolewa na Heche alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Aidha msimamo wa CHADEMA ulisisitiza kwa kusema "haiitambui Tume ya Uchunguzi iliyoteuliwa na Ndg. Samia Suluhu Hassan, aliyejisimika madarakani bila ridhaa ya wananchi inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed Chande Othman, akiielekeza kuchunguza “matukio ya uvunjifu wa amani” yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025."
Vilevile grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo ni ya kughushi kwani haijachapishwa katika kurasa rasmi za Jambo TV.