Ndo katiba inasema mbunge ajue kusoma na kuandika, katiba mpya muhumu sanaa
Kidemokrasia kabisa ubunge hautakiwi kuwa na kikwazo cha elimu kubwa.
Mimi kila siku nikisikia watu wanapinga kigezo cha mbunge kujua kusoma na kuandika, naona kuwa hawaelewi demokrasia na wanaliangalia jambo hili kutoka upande mbaya.
Wagombea ubunge hawatakiwi kuwa na kikwazo cha elimu kikubwa, kujua kusoma na kuandika ndiyo kigezo kizuri kabisa cha kumuwekea mbunge.
Kwa sababu, kinachotakiwa kumpa mtu ubunge si kujua kusoma na kuandika. Kinachotakiwa kumpa mtu ubunge ni kura za wananchi.
Marekani hawana kigezo cha elimu kuwa Senator au Member of the House, kuwa mbunge. Lakini sifikiri kuwa kuna wabunge wengi ambao hawana degree.
Kwa nini? Jamii imeongeza access to education. Degree ni kitu cha kawaida tu. Tena wengine wanaziona hazina maana wanaenda kwenye trades huko na kutoa huduma jeshini.
Ukiweka kiwango cha degree kwa mfano, kama sharti la kuwa mbunge, katika nchi ambayo wapiga kura wenye degree hawafiki 10%, hiyo maana yake umewanyima 90% ya nchi nafasi ya kuwa wabunge na kuwawakilisha wananchi.
How democratic will that be?
Tatizo letu si kwamba tuna kiwango kidogo sana cha elimu kwa wabunge, kujua kusoma na kuandika. Hiki si tati,o, Marekani hawana kabisa kiwango. Tatizo letu wananchi hawana elimu ya kuchuja nani anafaa kuwa mbunge na nani hafai.
Ukielimisha wananchi wengi, automatically wagombea ubunge wote watakuwa wana degree bila ya sharti la degree. Hili ndilo limetokea Marekani.
Tatizo sisi tunataka viongizi wasomi badala ya kutaka jamii ya wasomi.
Ukiwa na viongizi wasomi lakini wananchi hawajasoma haikusaidii sana, utapata bunge lililojaa ma profesa wap9gaji kwa sababu hawana wananchi wa kuwafuatilia. Mfano mzuri ni serikali za CCM mpaka hii yetu ya sasa ambayo imejaa wasomi wa madegree ambao hawana maadili. Mtu kasoma mpaka Harvard, anakuibia, unamshika, anakwambia hivi ni vijisenti tu.
Tunapigia kelele wabunge na viongozi kwa sababu hiyo ni sehemu rahisi kukaumu. Na kwa kweli kwa kiasi fulani ukiwa kiongozi kawama ni zako, maana wewe ndiye kiongizi. Nobkesse Oblige, yo whom much is given, much shall be required. Lakini, viongozi wanatokana na wananchi.
Hutakiwi kuwa na nchi ambayo watu walio na degree hawafiki 10% halafu sharti la kuwa mbunge ni degree.
That is vwry undemocratic and anti-inckusivity. Kuna watu wengine hawana degree kwa sababu walianza kufanya kazi kwenye trade unions zamani huko wana uzoefu sana wa trade unions uliozidi degree.
Rais wa Brazil Luis Lula Inacio daSilva hana degree, lakini wa Brazil wamemchagua kuwa rais mara tatu.
Angewekewa kikwazo cha elimu, Brazil ingekosa uziefu wake.
Chujio la wabunge na viongozi wengine wa kuchaguliwa liwe kura za wananchi, si viwango vya elimu rasmi ambavyo vitawaondoa wengi kwa namna isiyo ya kidemokrasia.
Tatizo mfumo wa uchaguzi nao mbovu na watu wanaochagukiwa hata hatujui kuwa wamechagukiwa au wamepachikwa tu.
Ndiyo maana watu wanasema "No Reforms, No Election".