SI KWELI PreGE2025 Heche Asema CHADEMA haileti wanaharakati kutoka nje, LHRC ndio inawaleta

SI KWELI PreGE2025 Heche Asema CHADEMA haileti wanaharakati kutoka nje, LHRC ndio inawaleta

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
photo_2025-05-28_09-22-19.jpg
 
Tunachokijua
John Heche ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo Januari 21, 2025 akichukua nafasi ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Tundu Lissu ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho aliyeko mahabusu akituhumiwa kwa kesi ya uhaini na uchochezi ambapo kesi yake inatarajiwa kuendelea tarehe 02 Juni, 2025.

Mwezi Mei 23, 2025 Heche aliongoza kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kujadili mambo mbalimbali, ambapo moja ya ajenda zilizoainishwa kujadiliwa na kikao hicho ni pamoja na hali ya Kisiasa Nchini, oparesheni ya 'No Reform No Election' (Bila Mabadiliko Hakutakuwa na Uchaguzi) pamoja na uvunjani wa Haki za Binadamu na Ukandamizaji wa demokrasia nchini.

Mtumiaji wa mtandao wa TikTok kwa jina la 'Mapinduzi 64' alichapisha taarifa iliyotumia utambulisho wa machapisho ya Millard Ayo ikiwa na kichwa cha habari 'Heche asema Heche asema CHADEMA haileti wanaharakati kutoka nje, LHRC ndio inawaleta'


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Kupitia ufuatiliaji wa kimtandao uliotumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) pamoja na marejeo ya video hotuba ya Heche Mei 23, 2025 JamiiCheck imejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

Chapisho lililotumika kusambaza taarifa hiyo likitumia utambulisho wa Millard Ayo si la kweli ni la kutengenezwa na wapotoshaji kwani halijachapishwa na Millard Ayo kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

Pia kwenye hotuba yake Heche hakutoa kauli yoyote iliyohusisha ujio wa wanaharakati kutoka nje ya nchi na kuwataja LHRC kuhusika kuwaleta nchini.

Aidha taarifa pekee iliyoripotiwa na Millard Ayo kutokana na hotuba hiyo, ni ile iliyoeleza kuwa Heche alisema kumekuwapo na kelele kila kona za kutaka kuonesha CHADEMA imepasuka lakini aliweka wazi kuwa CHADEMA haijapasuka, ipo imara na kwamba waliondoka ni wachache kuliko waliobaki na Chama kinasonga mbele.

“Kumekuwa na kelele kutaka kuonesha Dunia kwamba CHADEMA imepasuka, CHADEMA haipo na ukiangalia magazeti Mimi najua habari ambazo zipo pushed na Serikali kwasababu haiwezekani TV, Magazeti yote yanaandika habari inayofanana Mimi najua ni kanyaboya tu, kati ya Wajumbe wote wa Kamati Kuu ameondoka Mjumbe mmoja tu, Baraza Kuu lina Wajumbe 456 kati yao waliiondoka ni 20, Mkutano Mkuu wetu una Wajumbe 1194 kati yao wameondoka Wajumbe 34”

“Tulikuwa kwenye ziara Kanda mbalimbali Watanzania kwa maelfu wamejitokeza kutupokea, kutuchangia, kutuunga mkono, kwahiyo nataka kuwaambia Chama kipo imara, kimetulia na kinachapa kazi, waliiondoka tunawatakia safari njema tukutane kazini“
​
Back
Top Bottom