SI KWELI PreGE2025 Heche asema wamemuandikia barua Mwenyekiti Tume ya uchaguzi wakiomba mazungumzo

SI KWELI PreGE2025 Heche asema wamemuandikia barua Mwenyekiti Tume ya uchaguzi wakiomba mazungumzo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
SIKWELI_HECHE_CHANZO26.jpg
 
Tunachokijua
John Heche ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo Januari 21, 2025 akichukua nafasi ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Tundu Lissu ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho aliyeko mahabusu akituhumiwa kwa kesi ya uhaini na uchochezi ambapo kesi yake inatarajiwa kuendelea tarehe 02 Juni, 2025.

Mwezi Mei 23, 2025 Heche aliongoza kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kujadili mambo mbalimbali, ambapo moja ya ajenda zilizoainishwa kujadiliwa na kikao hicho ni pamoja na hali ya Kisiasa Nchini, oparesheni ya 'No Reform No Election' (Bila Mabadiliko Hakutakuwa na Uchaguzi) pamoja na uvunjani wa Haki za Binadamu na Ukandamizaji wa demokrasia nchini.

Mtumiaji wa mtandao wa TikTok kwa jina la 'Mapinduzi 64' alichapisha taarifa iliyotumia utambulisho wa machapisho ya The Chanzo ikiwa na kichwa cha habari 'Heche asema tumemuandikia barua mwenyekiti tume ya uchaguzi tunaomba mazungumzo'

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Kupitia ufuatiliaji wa kimtandao uliotumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) pamoja na marejeo ya video hotuba ya Heche Mei 23, 2025 JamiiCheck imejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

Vilevile Chapisho lililotumika kusambaza taarifa hiyo si la kweli bali ni la kutengenezwa na wapotoshaji kwani halikuchapishwa na The Chanzo kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

Hata hivyo katika kikao cha kamati kuu ya CHADEMA kilichofanyika tarehe 23 Mei, 2025 Heche hakutoa kauli yoyote kwamba Chama hicho kimemuandikia barua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kuomba mazungumzo.

Aidha Makamu mwenyekiti huyo katika hotuba yake alieleza ni kwanini wanaendelea kusimamia msimamo wao wa 'No reforms No election' akiyataja madhaifu yanayojitokeza nyakati za uchaguzi wakihitaji yapatiwe ufumbuzi.

"Mambo yote haya tunayopigania, ni ya kweli, tufanyeje?, tukubaliane na siasa za ulaghai za kuambwia tugawiwe majimbo kwa hiyo tuingie kwenye uchaguzi kwa kugawiwa majimbo na sio kupiga kura? au tusimamie msimamo wa wananchi kwa kuhakikisha hii nchi inaondolewa kwenye mikono ya mafisadi kwa kura za wananchi?, Msimamo wa chama chetu ni kusimama na msimamo wa wananchi na kukataa siasa za ulaghai, tumekataa siasa za ulaghai"

Rejea hapa hotuba ya Heche

View: https://www.youtube.com/live/1-31t9-HSUM?si=X7XBlYx10tZL7B8A&t=1531​
Back
Top Bottom