PostGE2025 Heche: Hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila Mwenyekiti kuwa Nje

PostGE2025 Heche: Hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila Mwenyekiti kuwa Nje

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, ametoa msimamo wa chama hicho akisema hakutakuwa na mazungumzo yoyote na Serikali iwapo Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu, atakapoachiwa huru na vikao halali vya Chama kuketi na kutoa uamuzi kuhusu hatua zinazofuata.

JOHN HECHE.jpg

Heche ametoa msimamo huo Julai 22, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, akisisitiza kuwa CHADEMA haitakubali kushiriki kwenye meza ya mazungumzo bila kuwepo kwa mpatanishi huru atakayesimamia mazungumzo kati ya pande husika.

Soma: Wasira: Kila siku Lissu anaweka mapingamizi, ndio maana inachukua muda mrefu

Amesema kwa mtazamo wa Chama hicho, mazungumzo ya kweli yanapaswa kufanyika katika mazingira ya haki, uwazi na usawa, huku wahusika wakuu wakipata nafasi ya kushiriki kikamilifu.

“Hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila Mwenyekiti kuwa nje, hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila watu kuwajibika, na hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila mpatanishi ambaye atakuwa katikati. Hayo ndiyo mazungumzo ya maana,” amesema Heche.

Kuhusu Kesi ya Lissu: Bwana Jela wa Ukonga, Andrew Ntamamiro akifanyiwa dodoso na Tundu Lissu

​
 
Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, ametoa msimamo mkali wa chama hicho akisema hakutakuwa na mazungumzo yoyote na Serikali iwapo Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu, hatakuwa nje ya gereza.

Kuna kitu sijakielewa.
Kwani hawa ccm lazima wafanye maridhiano na Chadema. Afterall huwa wanasema Vyama vipo vingi sana, sio Chadema peke yao wenye umuhimu.

Wamekatazwa kuridhiano na Act au Chauma au cuf au Udp?
 
Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, ametoa msimamo mkali wa chama hicho akisema hakutakuwa na mazungumzo yoyote na Serikali iwapo Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu, hatakuwa nje ya gereza.

Safi sana. Hakuna haja ya mazungumzo wala maridhiano. Tuendelee hv hv mpk 2030
 
maridhiano ya hiyari ni ya waTanzania wote gentleman regardless ya chama au dini yako na sio lazima wewe au mimi tuhusike. waTanzania wengine wanaweza kutuwakilisha pia 🐒
Sikia we LB7 Kama ingekuwa rahis si mngekuwa tayar mshafanya hayo maridhiano

Siyo rahis hvyo mambo kwa ground n magumu ndio maana mmeanza propaganda za kuifreeze chadema ili muweke WATU wenu uzur uongozi uliopo n kama twaha kiduku

Yaan BENDERA CHUMA MLINGOTI CHUMA
 
hakuna wa kushinikiza hilo la maridhiano kufanyika atakavyo yeye binafsi gentleman bali waTanzania watakapokua tayari.

Maridhiano hayo ya hiyari ya kitaifa yanaweza kufanyika leo au kesho, lakini pia yanaweza kufanyika 2030 bili kujali mihemko au makasiriko useless ya maadui wa umoja, amani na usalama wa waTanzania 🐒
 
Back
Top Bottom