Huko nyuma wakati Tanzania ikiitwa kisiwa cha amani, kija Nyerere, Mkapa nk walikuwa wakienda nje ya nchi kusuluhisha migogoro kama wapatanishi ambao wanakuwa katikati. Kwa nini CCM ya leo ikatae kusuluhishwa na watu wa kati? Ama kweli siku zinakimbia sana.Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, ametoa msimamo mkali wa chama hicho akisema hakutakuwa na mazungumzo yoyote na Serikali iwapo Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu, atakapoachiwa huru na vikao halali vya Chama kuketi na kutoa uamuzi kuhusu hatua zinazofuata.
Heche ametoa msimamo huo leo Julai 22, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, akisisitiza kuwa CHADEMA haitakubali kushiriki kwenye meza ya mazungumzo bila kuwepo kwa mpatanishi huru atakayesimamia mazungumzo kati ya pande husika.
Kuhusu Kesi ya Lissu: Bwana Jela wa Ukonga, Andrew Ntamamiro akifanyiwa dodoso na Tundu Lissu
Amesema kwa mtazamo wa Chama hicho, mazungumzo ya kweli yanapaswa kufanyika katika mazingira ya haki, uwazi na usawa, huku wahusika wakuu wakipata nafasi ya kushiriki kikamilifu.
“Hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila Mwenyekiti kuwa nje, hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila watu kuwajibika, na hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila mpatanishi ambaye atakuwa katikati. Hayo ndiyo mazungumzo ya maana,” amesema Heche.
CCM wakikubali tu kuweka msuluhishi wa kati hapo ndipo masuala muhimu ya nchi yatashughulikiwa kwa shinikizo ikiwemo katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
CCM wakijiongoza wenyewe kusuluhisha maana yake wataleta ulaghai!
Ngoja tuone