PostGE2025 Heche: Hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila Mwenyekiti kuwa Nje

PostGE2025 Heche: Hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila Mwenyekiti kuwa Nje

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, ametoa msimamo mkali wa chama hicho akisema hakutakuwa na mazungumzo yoyote na Serikali iwapo Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu, atakapoachiwa huru na vikao halali vya Chama kuketi na kutoa uamuzi kuhusu hatua zinazofuata.

Heche ametoa msimamo huo leo Julai 22, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, akisisitiza kuwa CHADEMA haitakubali kushiriki kwenye meza ya mazungumzo bila kuwepo kwa mpatanishi huru atakayesimamia mazungumzo kati ya pande husika.

Kuhusu Kesi ya Lissu: Bwana Jela wa Ukonga, Andrew Ntamamiro akifanyiwa dodoso na Tundu Lissu

Amesema kwa mtazamo wa Chama hicho, mazungumzo ya kweli yanapaswa kufanyika katika mazingira ya haki, uwazi na usawa, huku wahusika wakuu wakipata nafasi ya kushiriki kikamilifu.

“Hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila Mwenyekiti kuwa nje, hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila watu kuwajibika, na hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila mpatanishi ambaye atakuwa katikati. Hayo ndiyo mazungumzo ya maana,” amesema Heche.

Sahihi,hata Afrika ya kusini,Mazungumzo ya muafaka yalifanyika Nelson Mandela akiwa huru/nje .
 
hakuna wa kushinikiza hilo la maridhiano kufanyika atakavyo yeye binafsi gentleman bali waTanzania watakapokua tayari.

Maridhiano hayo ya hiyari ya kitaifa yanaweza kufanyika leo au kesho, lakini pia yanaweza kufanyika 2030 bili kujali mihemko au makasiriko useless ya maadui wa umoja, amani na usalama wa waTanzania 🐒
Usipende kutuita Watanzania,kama vile tuna Hoja sawa na zako,sema Wana CCM Tena baadhi! Maana mmechokwa na wengi!
 
hakuna wa kushinikiza hilo la maridhiano kufanyika atakavyo yeye binafsi gentleman bali waTanzania watakapokua tayari.

Maridhiano hayo ya hiyari ya kitaifa yanaweza kufanyika leo au kesho, lakini pia yanaweza kufanyika 2030 bili kujali mihemko au makasiriko useless ya maadui wa umoja, amani na usalama wa waTanzania 🐒
Naunga mkono Kuna vyama 18 wakafanye navyo
 
Hii CHADEMA ya sasa iko very serious. I love it. Amesema Heche vizuri sana. hatutaki kuwa na siasa za ulaghai laghai ambazo CCM na vichama pandikizi ndo wanazitaka na kuzifurahia.
Na CHADEMA tunataka mazungumzo yasiyo na kificho wananchi wajue tumezungumza nini. That is what we want as a country. Harafu anatokea mtu eti anawapinga CHADEMA,unajiuliza hivi huyu mtu ana akili kweli. NARUDIA KUSEMA NA NINAUHAKIKA ASILIMIA 100% WOTE WANAOIPINGACHADEMA WAKO CONNECTED NA MAMBO YA RUSHWA RUSHWA, UDANGANYIFU, DHULUMA NA MAMBO MENGINE MACHAFU YA NAMANA HIYO. HAIWEZEKANI MTU AMBAYE YUKO VERY CLEAN ETI AKAWA ANAISAPOTI CCM. NO WAY

Umeandika kwa hisia kali sana mkuu. Kwa kweli tujipe pole!

Ni hivi,almost everything has been CCM-lized in this kantri.Watu wamejengewa mentality kwamba ili ufanikiwe kwenye ajira,biashara n.k lazima uwe mwanakijani,vinginevyo hutoboi.

Kwenye dini nako unatakiwa uwe unaimba wimbo wa Amani tu ili raia wazidi kupumbazika wasizijue HAKI zao. Ukiimba wimbo wa HAKI tu,unakutana na kilichomkuta Gwajima.Na hili ndilo chimbuko la uchawa hususani kwa watu wenye low Emotional and Adversity Quotient!

Bahati nzuri katika mikakati yao walisahau kuzuia smartphones zisiingie nchini(hapa wanaharakati wanapita nao jumla jumla). Wamejichanganya kusambaza shule za kata nchi nzima. Kuna lundo kubwa la vijana wasomi wanazurura tu mitaani bila matumaini(Hili hayati Edo alilisemea mjengoni na nadhani alipuuzwa).

Ogopa sana mnyonge akijua namna anavyodhulumiwa HAKI zake!
Ogopa sana mjinga akijua namna alivyotengenezwa kuwa mjinga makusudi ili adhulumiwe HAKI zake!

Ogopa sana kijana mwenye nguvu akipoteza matumaini ya Kesho yake.

1 YOHANA 2
14 (b) Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.

Uzuri ni kwamba Nyakati hazipo upande wao kabisa na bahati nzuri ni kwamba wanachokihofia ndicho kitakachowapata!. Watajifunza kwa njia ngumu sana kwamba Maisha ya mwanadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu sio ya kuyachezea!.

God's eye is widely open and his mighty hand is in charge!
 
hakuna wa kushinikiza hilo la maridhiano kufanyika atakavyo yeye binafsi gentleman bali waTanzania watakapokua tayari.

Maridhiano hayo ya hiyari ya kitaifa yanaweza kufanyika leo au kesho, lakini pia yanaweza kufanyika 2030 bili kujali mihemko au makasiriko useless ya maadui wa umoja, amani na usalama wa waTanzania 🐒
Wajiri wako wanakesha wakiomba hawa wahuni walegee maridhiano yafanyike hata kesho
 
Kesi ya Lissu iende haraka mahakama imuachie huru maisha yaendelee, mtaiishi na visasi mpaka lini? Maisha ni mafupi sana hapa duniani tusijidanganye na mali tukafikiri ni zetu hapana, tujitathimini kama Taifa.
 
Kuna kitu sijakielewa.
Kwani hawa ccm lazima wafanye maridhiano na Chadema. Afterall huwa wanasema Vyama vipo vingi sana, sio Chadema peke yao wenye umuhimu.

Wamekatazwa kuridhiano na Act au Chauma au cuf au Udp?
Kufanya maridhiano na hivyo vinavyoitwa vyama ni sawa na mtu kujisemea mwenyewe kama chizi.

Hivyo vinavyojiita vyama ni vyama vyao na vinaunga mkono kwa dhati manyanyaso yanayofanywa na ccm na serikali yake kwa wananchi wa Tanzania.
 
Kama ccm itaendelea na huu ubabe kwamba piga ua lazima waendelee kuitawala hii nchi watanzania wapende wasipende basi Tanzania sio miaka mingi inaenda kuingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe Civil War.
 
Kama kweli wana nia ya dhati na maridhiano, wafute matokeo ya uchaguzi wa 2025
 
hawa si walishinda kwa 98%,hii ni ishara kwaba wanakubalika,wafanye maridhiano wenyewe kwa wenyewe
 
Anayezungumziwa hapa ni Samia, siyo mimi.
Samia hafiki 2030.
Yaani kwa uwezo ulionao mpk kujua Samia hafiki 2030 haiwezekani ikawa hujui na wewe utafika mwaka gani. Sema tu...
 
Kama ccm itaendelea na huu ubabe kwamba piga ua lazima waendelee kuitawala hii nchi watanzania wapende wasipende basi Tanzania sio miaka mingi inaenda kuingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe Civil War.
Uhakika uliopo sasa ni huu: CCM hawawezi kuachia madaraka bila ya matumizi ya nguvu kuwaondoa.
Hili wamekwishaliweka wazi kabisa.
 
Back
Top Bottom