Huyu mkurya aliye na wajomba na baba wadogo Kenya, aliyesoma SAUT kwa kulipiwa na Barrick North Mara na mkopo wa bodi ya elimu anajiona msafi kuliko watanzania wengine.
"Cha kwanza ni kwamba huyu Mama hawezi kushinda uchaguzi Lissu akiwa mgombea, wala sisi tukikiwa tunaongoza Chama. Kwasababu kwanza ni Mzanzibar—hilo sio favour kwake. Pili ni Mwanamke—sio favour kwake. Tatu hana hoja, ameongoza watu wameona. Kwa hiyo wanachotaka ni watumie huu uchaguzi wa CHADEMA kumzaliza Uchaguzi Mkuu mapema. Kwamba CHADEMA ikifa sasa hivi, tarehe 21 Januari, wao hawana Uchaguzi."
"Walikuwa wamepanga watumie labda bilioni 400 kwenye Uchaguzi. Kama wanaweza wakachukua bilioni 5, wakampa Freeman Mbowe akaua Chama kisiwepo na Uchaguzi usiwepo, wao watakuwa wamepata nafuu ya bilioni karibia mia ngapi? Uchaguzi ni wakufa na kupona kwenye Chama chetu. Sasa hao watu wanakupigieni simu, hao watu wanaongea na nyie, wanakuja kwenye vikao, kwanini hamuwarekodi tupate huo ushahidi?"
"Kwa mfano, pale Mwenyekiti alipokuwa anazungumza kwamba mtachukuliwa malazi... (hiyo ni kitu kizuri sana). Mara ngapi watu wetu wamesafiri kwa shida kwenye mikutano mikuu yote?"
"Milikuwa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, watu wanahangaika hawana hata hela ya kujazia fomu, hela za kuchonga mihuri, watu wanajichangisha wenyewe, hizo hela zote wanazosema wanazo zilikuwa wapi.? Hao watu wasifufanye sisi hatuna akili tafuta huo Ushahidi, rekodini hao watu mazungumzo yao, tunahitaji Ushahidi kisha tutaufanyia kazi"