Pre GE2025 Heche: Huyu mama hawezi kushinda uchaguzi Lissu akiwa mgombea na sisi tukiongoza chama sababu ni mwanamke, Mzanzibar na hana hoja

Pre GE2025 Heche: Huyu mama hawezi kushinda uchaguzi Lissu akiwa mgombea na sisi tukiongoza chama sababu ni mwanamke, Mzanzibar na hana hoja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
Huyu mkurya aliye na wajomba na baba wadogo Kenya, aliyesoma SAUT kwa kulipiwa na Barrick North Mara na mkopo wa bodi ya elimu anajiona msafi kuliko watanzania wengine.

"Cha kwanza ni kwamba huyu Mama hawezi kushinda uchaguzi Lissu akiwa mgombea, wala sisi tukikiwa tunaongoza Chama. Kwasababu kwanza ni Mzanzibar—hilo sio favour kwake. Pili ni Mwanamke—sio favour kwake. Tatu hana hoja, ameongoza watu wameona. Kwa hiyo wanachotaka ni watumie huu uchaguzi wa CHADEMA kumzaliza Uchaguzi Mkuu mapema. Kwamba CHADEMA ikifa sasa hivi, tarehe 21 Januari, wao hawana Uchaguzi."

"Walikuwa wamepanga watumie labda bilioni 400 kwenye Uchaguzi. Kama wanaweza wakachukua bilioni 5, wakampa Freeman Mbowe akaua Chama kisiwepo na Uchaguzi usiwepo, wao watakuwa wamepata nafuu ya bilioni karibia mia ngapi? Uchaguzi ni wakufa na kupona kwenye Chama chetu. Sasa hao watu wanakupigieni simu, hao watu wanaongea na nyie, wanakuja kwenye vikao, kwanini hamuwarekodi tupate huo ushahidi?"

"Kwa mfano, pale Mwenyekiti alipokuwa anazungumza kwamba mtachukuliwa malazi... (hiyo ni kitu kizuri sana). Mara ngapi watu wetu wamesafiri kwa shida kwenye mikutano mikuu yote?"

"Milikuwa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, watu wanahangaika hawana hata hela ya kujazia fomu, hela za kuchonga mihuri, watu wanajichangisha wenyewe, hizo hela zote wanazosema wanazo zilikuwa wapi.? Hao watu wasifufanye sisi hatuna akili tafuta huo Ushahidi, rekodini hao watu mazungumzo yao, tunahitaji Ushahidi kisha tutaufanyia kazi"

Huyu mkurya aliye na wajomba na baba wadogo Kenya, aliyesoma SAUT kwa kulipiwa na Barrick North Mara na mkopo wa bodi ya elimu anajiona msafi kuliko watanzania wengine

View: https://x.com/i/status/1878408254025261429

Watanzania wana haki kikatiba ya kutoa maoni yao juu ya yeyote na chochote kuhusu nchi yetu na nchi nyingine duniani. Wewe ni nani hata uthubutu kuwanyooshea kidole watanzania wanaotumia haki yao kikatiba?
 
Huyu mkurya aliye na wajomba na baba wadogo Kenya, aliyesoma SAUT kwa kulipiwa na Barrick North Mara na mkopo wa bodi ya elimu anajiona msafi kuliko watanzania wengine

heche ni mraibu wa kubeti lakini pia anatuamia vitu vya kusisimua akili,

huenda dishi linaendelea kubaya zaidi :NoGodNo:
 
Watanzania wana haki kikatiba ya kutoa maoni yao juu ya yeyote na chochote kuhusu nchi yetu na nchi nyingine duniani. Wewe ni nani hata uthubutu kuwanyooshea kidole watanzania wanaotumia haki yao kikatiba?
Hawana haki ya kutoa maoni ya kibaguzi na yanayo hatarisha umoja wa kitaifa kama wapi Rais anatoka, mwanamke n.k.
 
Chukua Clips kumi za John Heche msikilize utagundua uwezo wake ni mdogo sana
Watu wenye uwezo mdogo hujificha kwa kutukana Viongozi na Serikali
Huwezi kumfananisha na kizazi cha akina Ester Bulaya, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Kafulila, John Mnyika wakijenga hoja bungeni
Heche ni mtupu sana
Labda waliosoma nae waje watupe ufafanunuzi zaidi
Heche huishia kutoa / ku-address challenges bila kuja na Solutions/ Way forward!!
 
Uko sahihi mkuu tafuta K vant usindikize mwisho wa wiki
 
Back
Top Bottom